SHERIA iliyodumu miaka 36 sasa inatajwa kutokuwa rafiiki na uhuru
wa habari, ni ile nambari 5 ya mwaka 1988 ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa
Habari Zanzibar.
Ni
miaka 36 sasa, sheria hii inaendelea kutumika Zanzibar, na kutajwa kuathiri na
kutishia utendaji kazi wawaandishi wa habari na vyombo vyao hapa visiwani.
Maana
wadau na waandishi wa habari, wanakubali kuwa, upatikanaji, usambaaji wa habari
ni haki ya kikatiba.
Kwa
Katiba ya Zanzibar yam waka 1984, kwenye kifungu cha 18, kimebainisha hilo
sambamba na ile ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania yam waka 1977, kwenye Ibara
kama hiyo nayo, imewekwa.
HISTORIA YA UPATIKANAJI SHERIA MPYA ZANZIBAR
Sheria
hiyo tokea mwaka 2010, ilianziwa harakati za kutaka kufutwa, kwa wadau wa
habari kujikusanya pamoja, ili sasa iwe na sheria moya ya habari.
Kwa
wakati huo, tasisi za Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ –ofisi ya Zanzibar, vyama
vya waandishi wa habari, taasisi za haki za binadamu na wizara husika, zilianza
harakati hizo.
Mara
kadhaa, kulikuwa na taarifa kuwa, mwaka ujao au mwakani Zanzibar itapatikana
sheria mpya ya habari, ambayo itakuja kufuta sheria ya Magazeti nambari 5 ya
mwaka 1988 na ile ya Tume ya Utangaazji nambari 7 ya mwaka 1977.
Ilikuchakua
takriban miongo miwili na nusu hivi kupita, bila Zanzibar kuwa na sheria mpya,
ingawa kwa Tanzania bara, wao walifanikiwa kufuta sheria ya Magazeti ya mwaka
1976, na kuwa na sheria ya Huduma ya vyombo vya habari ‘MSA’ ya mwaka 2016.
Aliyewaji
kuwa Katibu mkuu wizara ya Habari Ali Mwinyikai, alisema iko siku Zanzibar,
itakuwa na sheria bora na iliyorafiki kwa waandishi wa habari.
Hata
aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa shirika la Magazeti ya serikali Zanziba Abdalla
Mohamed Juma, aliwahi kusema, sheria ya magazeti, iliyopo sasa, haiendani na
upevukaji demokrasia.
Kwa
miongo miwili na nusu, wadau wa habari juhudi zao za kuwa na sheria mpya ya
habari ziligonga ukuta, na harakati hizo zikaanza tena miaka ya 2018/2019.
YANAYOWASKUMA WADAU KUFUTWA KWA SHERIA YA MAGAZETI, VITABU NA
MAWAKALA WA HABARI NO 5, 1988.
Sheria hii yenye
vifungu 81 na sehem 10, sasa inatimiza miaka 36, tokea kutungwa kwake, na kwa
maana nyingine, vipo vifungu zaidi ya 40, ambavyo vyengine vinahitaji kufutwa.
Vifungu
vyengine vikihitajika kufanyiwa marekebisho na vyingine, vilivyobeba maneno
makali kama uwezo wa waziri, waandishi kudhibitiwa na kufanya
uchochezi.
Kwenye
sheria hii, ambayo kwa sasa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania
TAMWA-Zanzibar, wanaharakishwa kufutwa kwa sheria hiyo.
Maana
Afisa Progamu hiyo Zaina Mzee, anakuwa hasikii la muadhini wala mteka maji kisimani,
kama siku moja Zanzibar haijakuwa na sheria yake.
VIFUNGU KANDAMIZI KWA UHURU WA HABARI
Moja
ya kifungu ambacho, kwa sasa wadau wanataka kifutwe ni kile cha 43, ambacho
chenyewe, kinaeleza ‘uwezo wa ofisa aliyeidhinishwa’.
Ambapo
kwa mujibu wa sheria hiyo, ofisa aliyeidhinishwa ni Polisi mwenye cheo cha
Msaidizi Ofisa Mkaguzi au mwenye cheo cha juu ya hapo.
Mchambuzi
wa sheria za habari Zanzibar Hawra Shamte anasema, kwa sasa sheria hiyo na hasa
kifungu cha 43 wanakiona, hakina mantiki.
‘’Makosa
yote yanayotokana na waandishi wa habari yana sura ya madai na sio jinai, sasa
iko wapi nafasi ya Polisi kuingia, kupekua kwenye vyombo vya habari,’’anahoji.
Ukali
wa mchambuzi huyu wa habari, unajidhihirisha kwenye kifungu hicho cha 43 (1) na
(2) ambavyo vimeeleza wazi mamlaka ya ofisi huyo wa Polisi.
‘’Mfano
kifungu (2) (a), kinaeleza uwezo wa ofisi huyo kuwa ‘anaweza kuingia
sehemu yoyote, jengo, chombo cha ardhini, angani ambamo anaamini kwa maoni yake
tu kuwa, mna vifaa vya habari, vilivyopangwa au vitakavyopangwa kukusanyia
habari,’’
Hata
kifungu kidogo cha 2 (b) kikaongeza kuwa, ofisi huyo anaweza ‘kuchunguza
mchakato wowote ambao unaonekana kuelekea kukusanya au kutoa habari yoyote’.
Kubwa
zaidi ambalo ni ukiukwaji wa uhuru wa habari, kifungu cha (c) kinampa uwezo
ofisi hiyo ‘kumtaka mwandishi wa habari yeyote, kutoa vitendea kazi
vyake, gazeti au waraka ambao, uko chini yake kukabdhi kwake’.
Kifungu
2 (d) ofisi huyo amepewa mamlaka ya ‘kunakili sehemu yoyote ya
vitendea kazi vya waandishi wa habari au akiamiani tu kufanya
hivyo, kuna uhusiano na uchunguuzi wake juu ya kosa chini ya sheria hii’.
Kubwa
zaidi, pia ofisi hiyo kwenye kifungu hicho cha 43 (2) (e) anaweza ‘kuagiza
taarifa zenye uhusiano na uchunguuzi wake kutoka kwa mtu yeyote, ambae anaamini aliajiriwa
au ataajiriwa, katika jengo alilokuwa akitunza kumbu kumbu’.
Pamoja
na uwezo huo, ambao wadau wa haki za uhuru wa habari wanaona ni uminywaji wa
haki za waandishi wa habari, sasa kifungu cha 44 kimekuja kumlinda.
Kifungu
hicho 44 (1) kinaeleza kuwa, ‘mtu yeyote atakayempinga, kumzuia, au
kumkwaza kwa ofisa huyo atakuwa ametenda kosa’
Na
adhabu kwa kosa hilo lipo kifungu cha 73, ambapo ni faini ya shilingi 200,000
au kifungo cha miaka miwili chuo cha mafunzo au adhabu zote mbili kwa pamoja.
WADAU WA HABARI WANASEMA JE?
Mkurugenzi
mtendaji wa Jamii TV Ali Massoud Kombo, anasema kifungu hicho sio rafiki, na
hakitarajii kukiona kwenye sheria mpya ijayo ya habari.
Anasema,
studio na vyumba vya habari ni ofisi nyeti kama zilivyonyengine, hivyo
utaratibu wa kuingia, uwepo kama zilivyo ofisi nyingine.
‘’Mbona
Ikulu, wodi ya wazazi, kambi za Jeshi na hata chuo cha mafunzo kuna utaratibu
wake, na sio ofisa yeyote tu Polisi, tena kwa maoni yake aweze
kuingia,’’anahoji.
Mmiliki
wa mawio tv online Suleiman Rashid Omar, anasema, kifungu hicho hakifai kuwepo,
maana kinahalalisha ukandamizaji wa uhuru wa waandishi wa habari.
Aliyekuwa Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ Kajubi Mukajanga wakati akizungumza
na waandishi wa habari kisiwani Pemba, alisisitiza vyombo vya dola kuwaachia
waandishi watekeleze kazi zao.
‘’Kuwapasha
habari wananchi juu ya matukio ya ndani na nje ni haki kikatiba, sasa kama kuna
sheria au kifungu kinampa uwezo mkubwa Polisi kuingia na kufanya atakavyo sio
sahihi,’’anasema.
Mratibu
wa TAMWA -Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema uhuru wa
waandishi wa habari ni mbolea kwa taifa, kutimiza malengo yake.
‘’Lakini
sheria yetu ya Mgazeti nambari 5 ya mwaka 1988 ya Zanziba na hasa kifungu cha
43, kinaipinga hata Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, iliyotoa haki ya kutoa
maoni,’’anaeleza.
Mjumbe
wa Kamati tendaji wa Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAZA’ Hidaya
Mjaka Ali, anasema sheria bora ni chachu ya kupata waandishi wa habari bora.
Mkurugenzi
wa vijana Pemba Ali Mussa anasema wanawategemea mno waandishi wa habari,
kuwaibulia changamoto za vijana na kuwaonesha njia.
Aliyewahi
kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kuskazini Pemba Juma Saadi Khamis anasema, sio
maeneo kama vyumba vya habari kuwa ofisa, anaweza kuvamia ikiwa hakuna uhalifu.
Aliyekuwa
Mdhamini wa Baraza la Habari Tanzania MCT-Zanzibar Shifaa Said Hassan, anasema
sheria hiyo imeshapitwa na wakati na moja ya vifungu vibaya ni cha 43 na
vifungu vyake vidogo.
‘’Haiwezekani
suala la haki ya kikatiba ya kupata na kutoa habari, apewe uwezo wa kupindukia
Polisi, juu ya kuingia na kupekua kwenye ofisi za waandishi wa
habari,’’anasema.
Mchambuzi
wa sheria za Habari Zanzibar Hawra Shamte anasema, kwenye nchi zinazojali kwa
vitendo utawala bora na utawala wa sheria, suala la kupata na kutoa habari,
haliwekewi masharti mazito.
Mkuu wa taaluma wa Chuo cha uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma Zanzibar
Imane Duwe, anasema dunia ikisherehekea ukuaji wa teknologia kwenye eneo la
habari, lazima waandishi wawe huru.
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari Zanzibar ‘ZPC’ Abdalla Abudull-rahman Mfaume na
mwenzake wa PPC Bakari Mussa Juma, wanasema vifungu ambavyo vinampa wasi wasi
waandishi wa habari, havina nafasi Zanzibar.
Mwanasherua
wa shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar Juma Khamis Juma aliwahi kusema
kuwa, ukuaji wa maendeleo ya taifa lolote duniani, waandishi wa habari mchango
wao upo.
NINI KIFANYIKE?
Mkurugenzi
wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake CHAPO, Nassor Bilali Ali,
anasema lazima kwenye sheria ijayo ya habari, kifungu hicho kifutwe.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wasioona ‘ZANAB ‘Pemba Suleiman Mansour, amesema lazima suala la
vyumba vya habari au wao wenyewe, kupekuliwa lisiwe la kila ofisa wa Polisi.
‘’Sheria
ijayo ya habari, sitamani kurejeshwa kwa kifungu hichi, maana kwa upande
mwengine ni kudhoofisha juhudi za waandishi katika kazi zao,’’anasema.
Afisa
Mdhamini wizara ya Habari Pemba Mfamau Lali Mfamau, anasema ukandamizwaji wa
waandishi wa habari, hudhoofisha maendeleo ya taifa.
Mkuu
wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, anasema sheria bora ya habari, huchangia
kuwa na jamii bora na inayofanya uamuzi sahihi.
Zuhura Juma Said mwandishi wa
habari wa shirika la Magazeti Pemba, anasema sheria hiyo ya Magazeti, Vitabu na
Mawakala wa Habari nambari 5 ya mwaka 1988, imekuwa kikwazo kwao.
Mwandishi
wa habari wa kituo cha tv na redio cha Zenj fm Amina Ahmed, anasema sheria hiyo
hasa kwenye upatikanaji wa kibali, umekuwa shida.
Mkurugenzi
wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzur Issa Ali, anasema ujio wa sheria mpya ya habari
vifungu vinavyompa uwezo mkubwa Waziri, visiwmo.
Mratibu
wa uchechemuzi wa upatikanaji wa sheria ya habari Zanzibar kutoka
TAMWA-Zanzibar Zazina Mzee, anasema wakati umefika Zanzibar kuwa na sheria
rafiki.
‘’Ndio
maana TAMWA -Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wingine, tuko mguu sawa
kuhakikisha sheria mpya ya habari inapatikana,’’anasema.
Hivi
karibuni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita,
anasema Zanzibar iko mbioni upatikanaji wa sheria mpya.
‘’Na
wala maoni yenu hayakutupwa yamezingatiwa na kwa sasa msaada wa sheria hiyo uko
ngazi ya mwanasheria mkuu,’’anasema.
Wakati
akiwaapisha makatibu wakuu miaka mitatu iliyopita, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein
Ali Mwinyi, aliwaagizi kuhakikisha wanazifanyia marekebisho sheria zilizopitwa
na wakati.
Mwisho
Comments
Post a Comment