Na Mwandishi wetu, Lindi@@@@
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Ikulu (kazi maalum) Kapten George Huruma Mkuchika amevutiwa na huduma zinazotolewa na Benki ya watu wa Zanzibar tawi la Mtwara ambapo ameipongeza benki hiyo.
Akizungumza alipotembelea banda la maonyesho ya nanenane kanda ya kusini yanayofanyika katika viwanja vya ngongo mkoani Lindi amesema kuwa ni benki yenye gharama nafuu.
Amesema kuwa unafuu huo umekuwa ukiwasaidia wakulima kupata malipo yao ya korosho na ufuta kwa wakati.
Akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, Ikulu (kazi maalum) Kapten George Huruma Mkuchika, kwenye Maonyesho ya Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya ngongo kwenye Mkoa wa Lindi Mwakilishi wa Benki hiyo katika maonyesho hayo Nassoro Mohamed Zaid amesema kuwa huduma hizo zitawezesha wakulima kuhudumiwa popote walipo.
Amesema kuwa uwepo wao katika maonyesho hayo ni kuhamasisha wakulima na wafugaji kuweza kutumia benki hiyo ambayo imeweza kukua kwa kasi na kusogeza huduma bora kwao.
"Wito wangu kwa wakulima watumie Benki hii kwa manufaa yao ambapo ukiweka na ukitoa hakuna makato lakini pia pesa ukitunza unaikuta kama ilivyo hatua ambayo itaongeza hamasa zaidi kwa wakulima na wafugaji kujiwekea akina kupitia benki hii" amesema Nassoro
MWISHO
Comments
Post a Comment