Na
Muandishi Wetu
Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto bi Abeida Rashid Abdallah amewataka
Wazazi na Walezi Wanawake kuwachunguza watoto wao sehemu za siri katika miili yao
ili kuhakikishwa kwamba mtoto hao wako salama na hawajafanyiwa vitendo vya udhalilishaji
vya aina ya ngono.
Kauli hiyo ameitowa
katika mafunzo ya kuwajengea uweza kikundi cha Banaty yaliyofanyika Michenzani
Mall Unguja mara baada ya mtaalam wa Afya Dkt Ummulkulthum Omar kuwasilishaji
mada ya afya ya mfumo wa uzazi pamoja na kueleza kwamba katika utekelezaji wa
majukumu yake anakutana na kesi za watoto wachanga wa miezi minane wameingiliwa kinyume na
maumbile na kuharibiwa.
Bi Abeida amesema kwa
vile Wazazi na Walezi Wanawake hawana vibakio ni vyema kuwa karibu na watoto hasa
watoto wa kiume waliyofikia umri wa balegh kwa kuwauliza masuali bila ya kuona
haya pamoja na kuwaangalia sehemu zao za siri kama ziko salama na hazijafanyiwa
udhalilishaji wa aina ya ngono.
“Tuwe karibu nao hasa watoto
wa kiume sisi wanawake hatuna vibakio kwahiyo lazima tuwe karibu na watoto wetu
tuwahoji Je hakuna mtu aliyeguza sehemu za siri? Na tusiishie kuwauliza tu. Pia
kuwaangalia hasa huko sehemu ya siri tujue kama kuko salama, tusisuniria azoeshe
mchezo mchafu ”. Alisema Abeida.
Alieleza kwamba ripoti ya
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeonesha matukio ya
udhalilishaji 199 yameripotiwa kwa mwezi wa Oktoba, 2023 kati ya idadi hiyo
asilimia 78.9 ni watoto na wanawake ni asimia 16.2 hivyo ni vyema Wazazi na
Walezi Wanawake kila mara wawe karibu na watoto wao.
Aidha katibu Mkuu huyo alitoa
wito kwa washiriki wa mafunzo hayo na wanawake wote waliyopata mafunzo ya
ujasiriamali kutumia ipasavyo elimu hiyo kwani Serikali ya Mapinduzi inatoa
fursa ya mikopo kwaajili ya kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujiongezea kipato na kujikwamua na
umasikinini. Alisema kwani umasikini pia unachangia matendo ya udhalilishaji
kutokea kwa watoto.
Naye Mtaalum wa Afya bi
Dkt Ummulkulthum Omar kutoka Hospital ya Rufaa ya Mnazimmoja Zanzibar katika
mada ya mfumo wa uzazi aliyowasilisha alieleza matatizo mbali mbali yanayowatokea wanawake katika
mfumo wa uzazi ikiwemo kutoshika mimba, kutokwa na uchafu usiokuwa wa kawaida
katika sehemu za siri, n.k. hivyo amewataka wanawake kukimbilia hospitali
endapo wataona dalili yeyote ambayo sio ya kawaida kutokana na elimu
aliyofundisha ili kuwahia kutimbiwa.
Aidha katika uwasilishaji
wa mada hiyo aliezea kwamba anakutana na kesi ya watoto wa umri tofauti ambao wameingiliwa
kinyume na maumbile ikiwemo watoto wa miezi minane, hali ambayo inasikitisha hasa
ukiangalia matendo hayo yanafanywa na mtu wa karibu.
Mapema Mratibu wa mafunzo
hayo ambaye ni Mkurugeni wa Raha online TV bi Raya Hamadi Mchele amesema lengo
la kunadaa mafunzo hayo ni kuwapa elimu kundi la Banaty ikiwemo elimu ya afya, kujitambua
na elimu ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha.
Kikundi cha Banaty kimeanzishwa
kwa lengo la kusaidiana katika shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo harusi
na msiba. Hivyo kikundi hicho kinamuda wa miaka minane na mfuko wao wafedha una
pesa zaidi ya shilingi za Tanzania milioni ishirini.
Mwisho
Comments
Post a Comment