NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SHAMRA shamra za kuelekea miaka 60 ya
Mapinduzi ya Zanzibar, yaliofanyika mwaka 1964, zinatarajiwa kuendelea tena
asubuhi hii, katika wilaya za Chake chake na Wete, kwa ufunguzi wa miradi
miwili.
Shamra shamra hizo, zitaanzia kwa wilaya ya Chake chake,
ambapo Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, anatarajiwa
kufungua soko la samaki na mboga eneo la Machomane wilayani humo.
Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 2:00
asubuhi, kwa kuwasili wananchi na wageni wingine mashuhuri, kabla ya Katibu Mkuu
wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za ‘SMZ’ Issa
Mahafudhi, kumpokea mgeni rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari,
na Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Mattar Zahor Massoud, alisema tayari kila kitu
kilichopangwa kwa ajili ya hafla hiyo, kimekaa sawa.
Alisema, tayari mgeni rasmi wa ufunguzi wa soko hilo,
alishapatikana mapema, na kilichobakia ni kwa wananchi na wafanyabiashara
kushiriki katika hafla hiyo.
‘’Ni kweli asubuhi hii ya Disemba 27, mwaka huu Naibu
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma, anatarajiwa kulifungua soko
jipya la na kisasa la Samaki na mboga, ndani ya shamra shamra za kuelekea miaka
60 ya Mapinduzi Zanzibar,’’alisema.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Salama
Mbarouk Khatib, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, mradi ambao unatarajiwa
kufunguliwa jioni ya leo, ni ule wa ghala la chakula na vifaa vya ujenzi, lililopo
Kinyasini wilaya ya Wete.
Alieleza kuwa, kuelekea shughuli hiyo, tayari mambo kadhaa
yameshakaa sawa, ikiwa ni pamoja utenzi, wimbo maalum wa mapinduzi na ngoma
nyingine za utamaduni.
Aidha alieleza kuwa, Katib Mkuu wizara ya Biashara na
Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ndie mwenyeji wa shughuli hiyo kwa upande mmoja, kwa
ndio wizara husika.
Wakuu hao wa mikoa wakielezea umuhimu wa kufanyika kwa
mapinduzi hayo, walisema yalikuwa na lengo zuri la kumkomboa mzalendo wa nchi hii,
ambae alikuwa hana thamani.
Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema
hakukuwa na mwananchi aliyekuwa akifikiria namna ya kulima na kupata tija, au
kufanyakazi na kupata malipo mazuri.
‘’Leo tukiwa ndani ya miaka 60 ya Mapinduzi, kila mmoja
ni shahidi kuwa, sasa tumekomboka na kila mmoja anafanyashughuli zake kwa
mujibu wa uwezo wake, haya ndio maana na mapinduzi daima,’’alisema.
Hata hivyo amewakumbusha wananchi hao, kuendelea
kushiriki katika hafla za uwekaji mawe ya msingi na ufunguzi wa miradi mbali
mbali, kwani serikali, inafanya kwa ajili yao.
Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib,
alisema maana ya mapinduzi, ni kuendeleza mbele ujenzi wa miradi mbali inayowahusu
wananchi na yenye tija katika maisha yao.
‘’Kila mmoja ni shahidi kupitia serikali ya awamu ya
nane, imeshafanya miradi kadhaa hasa ndani ya mkoa huu, tena ndani ya muda
mfupi ukiwemo kituo cha Vijana, bara bara ya uwekezaji, skuli ya msingi kisiwa
cha Kojani pamo na skuli ya Ole,’’alifafanua.
Miradi ambayo itafunguliwa kesho ni pamoja na ofisi ya
elimu Wete, uwekaji jiwe la msingi skuli ya msingi Mwambe pamoja na mradi wa
vijana uliopo Weni wilaya ya Wete.
Mwisho
Comments
Post a Comment