Skip to main content

WATU WENYE ULEMAVU WATAKA NAFASI MAJIMBONI SIO VITI MAALUM PEKEE

 

NA ASIA MWALIM, ZANZIBAR @@@@

 
NCHI nyingi hupanga mipango yake ya Kimaendeleo na kiuchumi kwa kuzingatia mambo mengi.Hii ni pamja na idadi ya watu wake na zaidi mahitaji yao, ikiwa pamoja na kuzingatia maumbile.
 
Katika hayo mazingatio limo kundi la watu wenye mahitaji maalum katika maisha yao ya kila siku na miongoni mwao ni wale wenye ulemavu.
 
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha takriban asilimia 15 ya watu duniani ambao ni zaidi ya bilioni moja ni wenye ulemavu, wengi wakiwa wanawake.
 
Kati ya hawa zaidi ya watu milioni 80 katika Bara la Afrika ni wenye aina moja au nyengine ya ulemavu.
 
Hata hivyo, kundi hili bado halijapewa umuhimu unaostahiki katika baadhi ya maeneo, hali inayowanyima haki zao za kikatiba na kidemokrasia.
 
Miongoni mwa malalamiko yanayosikika hapa kwetu ni ya vyama vya siasa kushindwa kuwasimamisha watu wenye ulemavu majimboni na badala yake kutegemea nafasi za viti maalumu pekee.
 
Wapo wanaouliza kama Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi, wanawaingiza wanawake wenye  ulemavu katika uteuzi wao kipi kinachofanya hali kama hiii kushindikana katika vyama vya siasa kuwaweka hawa kuwa wag ombea katika uchaguzi?  
 
Matokeo ya sensa yanaonesha kiwango cha watu wenye ulemavu Tanzania kimeongezeka kutoka watu 93 katika mwaka 2012 hadi 112 mwaka 2022 kwa kila watu 1,000.
 
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imeshuhudia serikali ikiteua wanawake zaidi, wakiwemo wenye ulemavu katika nafasi za juu za uongozi.
 
Katika mahojiano maalum wanawake wenye ulemavu walielezea wanavyotamani kuipata haki ya kuchaguliwa kwenye majimbo kwa njia nyepesi, kama ilivyo kwa watu wengine.
 
Vyama vya siasa havijatoa umuhimu wa kusimaisha watu wenye ulemavu majimboni na hili limelezewa na wanwake wenye ulemavu kama ni ubaguzi.
 
Jamila Borafya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisema kundi hilo lina uwezo wa kuongoza nafasi za uwakilishi au ubunge majimboni na sio tu kupitia nafasi za viti maalumu.
 
"Tunataka nafasi za majimboni na sio za viti maalumu pekee kwani tunao uwezo na uzoefu wa kutosha" alisema.
 
 Alisema ni vizuri wanawake wenye ulemavu wanapojitokeza kugombea wakapewa nafasi sawa na wagombea wengine na hata kuwapa kupaumbele.
 
Alsema mtindo wa sasa wa kutoa zaidi nafasi kwa wanaume sio sahihi na unahitaji marekebisho.
 
Viashiria ya kijamii, uchumi na mazingira viliojitokeza katika sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, vinaonyesha katika ngazi ya mkoa Zanzibar watu wenye ulemavu kuanzia   miaka 7 na kuendelea ni 114 kwa kila 1000.
 
Ripoti inaonesha idadi ya watu wenye ulemavu imeongezeka kwa watu 39 kwa kila 1,000 kati ya sensa ya mwaka 2012 na ya 2022.
 
Adil Mohammed Ally, Mratibu Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB), alisema watu wenye ulemavu wana himili kuongoza nafasi za majimbo, lakini ipo haja kwa vyama vya siasa kuzingatia hilo ile watu hao wapate haki yao ya kikatiba.
 
Alitaka Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuweka sheria madhubuti na msisitizo kwa vyama vya siasa kutoa kipaumbele kwa watu wa kundi hili watapotaka kugombea majimboni.
 
Hata hivyo, aliwataka watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi majimboni mwaka 2025 kwani jamii imebadilika na yamefanyika marekebisho ya mifumo ya kupiga kura kwa watu wenye ulemavu.
 
Alitoa mfano wa katiba ya Zanzibar ya 1984, ambayo inaeleza katika kifungu 21(2) kila Mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki ukamilifu katika kufikia uamuzi wa mambo yanayomuhusu yeye na taifa.
 
Vile vile katika marekebisho ya 2010 katiba imeeleza katika kifungu nambari 67 (1) kuwa kutakuwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanawake kwa asilimia 40 ya wajumbe wa kuchaguliwa katika majimbo.
 
Aisha Ali Abdallah, kutoka ZANAB wilaya ya Chake chake, Pemba, alisema ushiriki wao katika kugombea nafasi za uongozi ni mzuri, lakini vyama vya siasa haviwapi nafasi.
 
"Nilishiriki kugombea uwakilishi katika uchaguzi wa mwaka 2020, lakini sikuipata hiyo nafasi" alisema.
Alisema hadi sasa Pemba hakuna kiongozi mwenye ulemavu ambaye wanaweza kumpa changamoto za kutatua matatizo yao kwa wakati.
 
VIONGOZI WENYE ULEMAVU
Mwantatu Mbarouk Khamis, Mwakilishi wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM) alisistiza haja ya wana siasa kuwaunga mkono watu wenye ulemavu kwa kuwapa nafasi majimboni ili waweze kushiriki katika vyombo vya maamuzi.
 
Hadi kukamilika uchaguzi 2020, Katika Baraza la Wawakilishi kuna viongozi watatu tu waliopata nafasi hizo kupitia viti maalumu kwa tiketi za CCM.






 
"Mwanamke mwenyewe ulemavu anao uchungu wa kusaidia jamii yake kupata maendeleo na hakuna sababu ya kuweka matabaka, Sote ni viumbe hatujakamilika, kila mtu ni mlemevu mtarajiwa", aliongeza.
 
VIONGOZI WA MAJIMBONI
Mbunge wa Kiembesamaki, Mohammed Maulid, alisema jamii inapaswa kuwapa nafasi wanawake na watu wenye ulemavu kwani ni baraka na kuwakwamisha ni kutowatendea haki.
 
Diwani wa Fukuchani, Fatma Ngwali Khamis, alisema licha ya hali yake na kukumbana na changamoto alishinda kupitia kura za wananchi   kutokana na uwezo wake wa kuongoza na kuwataka watu wenye ulemavu kujitokeza zaidi majimboni licha ya magumu wanayopitia.
 
Alisema wapo wanaodhani ukimuweka mtu mwenye ulemavu jimboni ni kama kupoteza nafasi, dhana iliyobebwa na jamii kubwa hasa wanasiasa.
 
WANAHARAKATI
 
Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-ZNZ, Dk.Mzuri Issa, alisema licha ya jitihada zinazofanyika zipo changamoto wanazopata wanawake na watu wenye ulemavu kufikia malengo yao.
 
Miongoni mwa changamoto ni baadhi ya viongozi wa dini, jamii na vyama vya siasa hawajaweka umuhimu kwa wanawake na watu wenye ulemavu kupewa nafasi za uongozi.
 
Alisema wakati mwengine watu wenye ulemavu wanabezwa na kufanyiwa dhihaki kwa kuangaliwa hali zao na kipato chao na kuitaka jamii kubadilika.
 
Alishauri sera na sheria za vyama vya siasa kusisitiza usawa kwenye nafasi za uongozi na maamuzi na kuvitaka vyombo vinavyohusika kusimamia haki.
Vyombo hivi nipamoja na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kuweka mustakabali mzuri kwa makundi yote.
 
Ukhty Amina Salum, alisema sio sahihi kutumia dini kama kigezo cha kumzuia mwanamke kuongoza, kwani dini inatambua uwezo wa mwanamke kuongoza.
 
Bi Asha Abdi, Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Zanzibar, alisema kuna umuhimu wadau na wanaharakati kulifanyia kazi sula la watu wenye ulemavu, hasa wanaogombea uongozi.
 
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR (ZEC)
Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar, (ZEC)Thabit Idarous Faina, alisema kazi ya tume ni kupokea maombi ya wagombea waliopitia mchakato katika vyama vyao.
 
Lakini ili kuondosha upendeleo usio wa lazima ni vizuri kwa vyama vya siasa kuliangalia hili kjwa undani ili kuondoa tataizo liliojitokeza.
 
Alisema tatizo la usimamizi wa wagombea ni kwa vyama kutowasilisha majina ya agombea mapema ili kuhakikisha asilimia 40 ya wanawake wagombea inafikiwa.
 
Alisema katika kueleka uchagyzi wa 2025, ZEC itaendelea kushirkiana na vyama vya siasa ili kupambana na rushwa na kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele ili waweze kushiriki kwa asilimia kubwa zaidi.


 
Kwa hali ilivuo sasa suala la vikwazo ambavyo wanawake na watu wenye ulemavu wanapambana navyo wanapoamua kugombea nafasi za uongozi ni tatizo inalohitaji kufanyiwa kazi ya ziada.
 
IDARA YA WATU WENYE ULEMAVU
Katibu Mtendaji wa Baraza La Taifa la Watu wenye ulemavu Zanzibar, Ussy Khamis Debe, alisema ni vyema Tume ya uchaguzi na mabaraza ya vyama vya siasa kuweka mazingira rafiki ya watu hao kupata nafasi hizo.
 
Aliitaka jamii na vyama vya siasa kuacha kuwatenga na kutokana na dhana potofu zinazotumika kuwazuwia wanawake na watu wenye ulemavu wasigombee uongozi.
 
JUMUIYA YA WANAWAKE WENYE ULEMAVU ZANZIBAR (JUWAUZA)
 
Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar, Bakar Omar Hamad, alieleza kuwa watu wenye ulemavu na hasa wanawake wanapitia wakati mgumu wanapotamani kuwa viongozi.

Katika mwaka 2020 kupitia vyama vya siasa takriban watu wenye ulemavu 30 walijitokeza kugombea nafasi tofauti majimboni na mwanamke mmoja mwenye ulemavu alishinda nafasi ya udiwani kati ya majimbo yote 50 ya Unguja na Pemba.
 
 
Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu, Salma Haji Saadat, alisema vyama vya siasa vinao wajibu wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapewa kipaumbele katika nafasi za uongozi.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Abeda Rashid alisema licha ya changamoto zinazowagusa wanawake, lakini wamenufaika na fursa fursa hizo katika miaka ya karibuni.
 
Abeda alisema kuna nafasi muhimu katika taasisi za serikali zinazoshikiliwa na wanawake.
 
Miongoni mwao ni ya yeye amabye ni mwenye ulemavu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii.
 
Aliwapongeza wadau maendeleo na taasisi mbali mbali ikiwemo WILDAF, TAMWA, JUWAUZA, kwa kuwa mstari wa mbele kuwashirikisha wanawake kwenye mafunzo ya kuwezesha kushika nafasi za uongozi.
 
MATAMKO MBALIMBALI YALIOLENGA USAWA
Dira ya maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050 imekusudia kuongezek kwa fursa kwa makundi ya watu wasiojiweza wakiwemo watu wenye ulemavu, wanawake watoto na wazee.
 
Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) mkataba wake wa kikanda uliotiwa saini mwaka 2008 na nchi wanachama wake ikiwemo Tanzania, wenye vifungu 43 unaelekeza nchi hizo kuzingatia suala la haki na usawa kati ya wanaume na wanawake katika suala la uongozi.
 
Kwa muhtasari ipo haja ya kulifanyia tathmini suala hili ili kuhakikisha watu wenye ulemavu na hasa akina mama wanatendewa haki na jamii yetu.
 
Kwa muda mrefu na hadi sasa umepatikana uthibitisho wa kutosa wa kuonyesha uwezo wa watu wneye ulemavu, wanaume na wanawake, kushika hatamu na kuwa viongozi wa kupigiwa mfano.
 
Moja ya njia ya kuliondoa tatizo hili ni kuongeza idadi yao kupitia majimbo kwani hii itasaidia kupaza sauti zao kwenye vyombo vya maamuzi, hasa wakati wa kutungwa sera mbali mbali.
 
Mwisho



 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...