NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MWAKILISHI wa Jimbo la Chambani wilaya ya
Mkoani Pemba, Bahati Khamis Kombo, amewasisitiza vijana kuchangamkia kilimo cha
matango bahari, kwani bei yake iko juu kuliko kilimo cha karafuu.
Alisema, kama Katibu mkuu wa wizara ya Uvuvi na Uchumi wa
Buluu, alivyosema kuhusu soko na bei, ni fursa kwa vijana wa jimbo la Chambani
kuekeza kwenye kilimo hicho.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya
kuwekwa kwa jiwe la msingI la kituo cha kutotoleshea vifaranga vya matango
bahari eneo la Dodo Pujini hivi karibuni, alisema sasa vijana washindwe wao.
Alisema, kama kilo matangao (majongoo) bahari ni shilingi
100,000 ni wakati vijana kwenda kujikomboa kupitia sekta ya bahari.
Alieleza kuwa, awali upatikanaji vifaranga ilikuwa ni changamoto
kwa wakulima hao kuagizisia kisiwani Unguja, ingawa kwa sasa kituo cha
uzalishaji kipo kisiwani Pemba.
‘’Changamoto kubwa ya kilimo cha matango bahari ilikuwa
ni upatikanaji wa vifaranga, lakini sasa kituo cha kisasa kipo na tumearifiwa
kina uwezo mkubwa wa kutoa 5000 kwa mwezi,’’alieleza.
Katika hatua nyingine Mwakilishi huyo wa Jimbo la
Chambani Bahati Khamis Kombo, alisema maono ya Dk. Mwinyi ni kutaka
kuhakikisha, anakikomboa kisiwa cha Pemba, kwa vitendo.
‘’Kila mmoja ni shahidi kwenye sekta za maji, hospotali,
elimu na sasa ameongeza kasi kawenye uchumi wa buluu kwa kugawa boti na mashine
yote ni kutaka kuongeza kipato kwa wananchi,’’alifafanua.
Hata hivyo ameikumbusha wizara husika, kuhakikisha
wanaongeza idadi ya mashamba yay a ufugaji wa matango bahari, kutoka 50 yaliopo
Pemba na kuongeza walau kufikia 200.
Wakulima wa kilimo hicho kutoka Gando, Asia Mwalimu Omar
na mwenzake Mtumwa Budi Pandu, walisema kilimo hicho licha ya kukabiliwa na changamoto
wakati wa kuanza, lakini kina tija mno.
‘’Pale mwanzo wa kupokea vifaranga panahitajika umakini
wa hali ya juu, lakini ikimalizika miezi mitatu, hawana shidna tena wewe subiri
upate fedha zao tu,’’walisema.
Nae Himdi Mjaka Himid wa Pujini, alisema uwepo wa kituo
hicho kitasaidia kupanua wigo wa kujiajiri kwa vijana na wanawake, ambao ndio
waliojiekeza baharini.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wizara ya Uchumi wa Bulu una
Uvuvi Zanzibar Aboud Suleiman Jumbe, aliwataka wananchi wa Zanzibar,
kuchangamkia kilimo hicho haraka, kwani kwa sasa thamani nzima ya soko kwa
bidhaa hiyo duniani inafikia Dola za Marekani Bilioni 10.
Alieleza kuwa, kwa nchi za Afrika, 80 kila 100
zilizopakana na ukanda wa pwani zinajishughulisha, kilimo, uuzaji usafirishaji
wa matanga bahari na theluthi moja ya zao hilo ni kutoka nchi za Afrika kwenda
kwenye masoko ya nchi za China, Japan, Hong kong, Taiwan na Korea.
inatoka magharibi
wa ukanda wa hari ya hindi inapopatikana Zanzibar,’’alifafanua.
Alieleza kuwa, mara baada ya Zanzibar kujenga kituo cha
kwanza cha kuzalishia matango bahari mwaka 2017, na kuanza ufugaji, uzalishaji
na usafirishaji nje ya nchi, mwaka 2019 ulikuwa ni tani 30.
Alifahamisha kuwa, kisha usafirishaji huo, ulisita kwa
ujio wa janga la Covid 19, mwaka 2020 hadi 2021 na kufikia tani 5.58, ingawa mwaka
2022 usafishaji huo uliongezeka na kufikia tani 15, zenye thamani ya shilingi
milioni 492.4.
Mwisho
Comments
Post a Comment