Skip to main content

FAMILIA HAZIWAPI KIPAOMBELE WATOTO WA KIKE KUSHIRIKI UONGOZI

 



NA ASIA MWALIM, ZANZIBAR@@@@


SIKU hizi imekua tofauti na zamani, wanawake kuwa viongozi si jambo geni kujitokeza kugombea nafasi hizo na kushinda, licha ya kukumbana na vikwazo vingi kila pembe.
 
Nchi nyingi, hivi sasa zimeendelea kutokana na wanawake kupewa nafasi za uongozi na kufanikiwa kuleta mabadiliko ya kiutendaji.
 
Nchi hizo ni kama Ethiopia, Liberia ,Tanzania na nyenginezo, ambazo uchumi wake umepanda na kupata mabadiliko makubwa katika sekta tofauti.

Ellen Johnson-Sirleaf ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Pia Malikia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. 

Katika miaka michache iliopita,  Tanzania, imepata mafanikio mengi, ikiwa pamoja na utulivu wa kisiasa na maendeleo katika sekta mbali mbali kufuatia uongozi wa nchi kushikwa na Rais wa kwanza mwanamke, Dk. Samia Suluhu Hassan.
 
Mama Samia hivi sasa anahesabika kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na wanawake wa hapa nyumbani na nchi nyengine.

Mifano mwengine ya wanawake wanaofanya vizuri kweye nafasi za uongozi ni balozi Amina Salum Ali ambae ni Mwenyekiti wa bodi ya Takwimu Zanzibar, Anna Makinda Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni amepata kiti cha urais umoja wa mabunge duniani.
 
Makala haya yataelezea mchango unaohitajika katika familia na jamii kuwaandaa na kumuwezesha kijana wa kike kuingia katika nafasi za uongozi.

Kawaida familia nyingi humlea mtoto wa kike kwenye utamaduni na mifumo isiyowaweka tayari kuingia katika uongozi na humuwekea mazingira ya mtumishi wa kazi za ndani kitu kinachojenga taswira mbaya katika makuzi ya watoto.

Licha ya vikwazo na changamoto mbali mbali wanazopitia watoto na vijana wakike, bado uwezo wao wa kuongoza ni mkubwa na hili linadhirika mara tu anapopewa nafasi.
 
Tukumbuke kuwa Idadi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 imefikia, 699,845, wanawake 368,066 na wanaume 331,779, ni wazi kuwa vijana wakike ni wengi kuliko wakiume.

Aidha idadi ya vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 24, imefikia 384,647 wanawake ni 202,067 huku wanaume ni 182, 580.

“SAFARI ya mwanamke kuongoza, huanza kuonekana mapema (utotoni) kuanzia ngazi ya familia hasa pale anapoanza kujiami, kutoa maamuzi ndani ya familia yake” alisema sabra.

Sabra Abdallah Said, Katibu wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Dimani, alisema wanawake wana mchango mkubwa katika jamii na familia zao licha ya changamoto za kifamilia kuwarudisha nyuma.

Kawaida familia nyingi humlea mtoto wa kike kwenye utamaduni na mifumo isiyowaweka tayari kuingia katika Uongozi badala yake humfanya kama mtumishi wa kazi za ndani na mtoto wa kiume kama muangalizi wa familia, kitu ambacho kinaleta taswira mbaya katika makuzi ya watoto.
 
“Nina hakika familia zingekua zinatoa malezi sawa kwa watoto wote,  wanawake tungekuwa na maendeleo zaidi ya wanaume, badala yake zinatulea katika mfumo wa kutukandamiza” alisema.
 
Alisema ni vyema wazazi kuwapatia kazi za ndani watoto wote bila ya kujali jinsia zao na sio kuwapa watoto wa kike tu, jambo ambalo linawakosesha kufanya mambo mengine ya maendeleo na uongozi.
 
“Familia ina mtizama mtoto wa kike, kufanya kazi zote za ndani, mfano kupika, kufua, kuosha vyombo, kujaza maji, akimaliza anataka kufanya mambo yake binafsi, je atapata wapi nguvu ya kuitumikia jamii” alisema.
 
Alisema changamoto ya mfumo wa malezi ndani ya familia zinawakwamisha vijana wa kike, kwa sababu ya kazi nyingi wanazopewa hivyo kukosa fursa ya kufundishwa ushujaa mapema kama ilivyo kijana wa kiume.



 
Kuanzia utotoni, mtoto wa kiume anapewa jina la jeshi, na mtoto wa kike anapewa jina la biharusi, suala ambalo si sawa, katika jamii kumuona mwanamke hawezi kuwa kiongozi mzuri, badala yake inamjenga katika mazingira ya kuolewa na kuitunza familia tu.

Aliomba jamii kubadilika kutoa malezi sawa ili watoto wa kike kutumia fursa wanazozipata katika  masuala ya uongozi na kuwajenga uzoefu mapema ili kugombea nafasi mbali mbali na sio kusubiri uteuzi.
 
Jitihada alizochukua kufikia nafasi ya Jimbo, alisema licha ya mashirikiano madogo kutoka kwa familia yake,  lakini juhudi zake za kujitoa katika kutumikia chama hazikumuacha nyuma kwani anajitoa  kuanzia ngazi ya tawi, na kupata ushawishi kwa vijana wezake kugombea nafasi hiyo.
 
Alisema, hana hofu ya kuwa kiongozi wa nafasi yoyote, kutokana na ujasiri alioupata kutoka kwa viongozi wanawake anaokutana nao na kujifinza vitu mbali mbali.

"Nimejifunza mengi hasa kupitia Mwakilishi wangu wa Dimani, Mwanaasha Khamis Juma, ambae ni mwanamke jasiri, anajiamini na anafanya kazi vizuri kwenye siasa hata anapokua Baraza la wawakilishi" alisema.

Kama hao hawatoshi basi wanajifunza kupitia viongozi wanawake kutoka nchi nyengine, mfano ni Jaji wa Afrika Mashariki, Juli Monic na Rais wa 24 wa Liberia Ellen Johnson Serlief.

Ruth Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka mwaka 1996 hadi 1997.

Jamii na familia ziwape kipaumbele wanawake kuingia kwenye uongozi kwani idadi ya wanawake na vijana ni kubwa zaidi, kuna umuhimu wa nafasi hizo zipelekwe zaidi kwa wanawake.

Mfano Takwimu za Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022, wanawake ni wengi zaidi kwa asilimia 51.6 dhidi ya wanaume ambao ni asilimia 48.4. Huku Zanzibar ina idadi ya watu 1889, 773 kati yao wanawake 974,281 na wanaume ni 915,492.

Zainab Saleh Salum, (ZASASA), Mbungewa  Jimbo la Tanzania nafasi ya vijana, alisema anatarajia kufika nafasi kubwa za uongozi na kuchukuwa nafasi mbali mbali ikiwemo uwakilishi, ubunge na nyenginezo.
 
Changamoto ni mila na desturi zenye mtazamo potofu zinamchukulia mwanamke kama mtu dhaifu asiyestahiki kuongoza badala yake kukaa nyumbani kutunza familia na mara nyengine mawazo yake kutothaminiwa, hivyo kuathiri maendeleo ya kina mama.



 
Malezi yasiyomjenga mtoto wa kike kujiamini, na kumpa nafasi kushiriki katika maamuzi ya familia, na kujenga hofu kutokana na vitisho vinavyofanywa na jamii kwa wanawake wanojitokeza kuwania nafasi za uongozi.
 
Samaki mkunje angali mbichi, huu ni msemo unaothibitisha kuwa wanawake wanapaswa kupewa elimu ya uongozi wakiwa na umri mdogo ili kuwajenga uwezo katika suala la uongozi.
 
“Uhamasishaji na mafunzo ya uongozi utasaidia wanawake kuwa majasiri na kujitokeza kwawingi, kuwania nafasi za matawi, wadi, jimbo, mkoa hadi taifa, itakuwa fursa nzuri kwao na jamii kiujumla,” alisema.
 
Hudhaima Tajo, Mwanafunzi chuo cha Chwaka, alisema kutokana na Mafunzo aliyopata hahofii kuongoza nafasi yoyote, wala kuogopa wanaume ambao wanaonekana ni vikwazo kwa baadhi ya nafasi za uongozi, badala yake amejipanga kugombania nafasi hata ya urais.
 
WANA JAMII
 
Khadija Salum Ali, mzazi wawatoto 4, alisema hakuna sababu za msingi ambazo zinamkataza mwanamke asigombee nafasi mbali mbali za uongozi ila kilichokuwepo ni mfumo dume ambao umetengenezwa na jamii.
 
Alisema changamoto hiyo husababisha wanawake wengi kutokuwa tayari kujitokeza kugombea nafasi hizo hata kama uwezo wanao, ikiwa atakosa mashirikiano mazuri kwa familia yake.
 
Alisema baadhi ya wanaume wanaawacha wake zao pale mwanamke anapotangaza nia ya kugombea nafasi yauongozi katika maswala ya kisiasa.
 
Rashid Muhidini Rashid, alisema umefika wakati wa kuwatafutia vijana wa kike fursa zaidi, hasa zinazohusu uongozi ili kupata wasaidizi wa Rais Samia na kuongoza nafasi nyengine kwa maslahi ya taifa. 
 
Vigumu wanawake kushughulikia masula ya kuingia katika Uongozi wakati hajajua watoto wake watabaki katika mazingira gani katika masuala ya chakula na usalama wao kutokana na hali ndogo ya kiuchumi.
 
WANAHARAKATI 
 
Maryam Ame Chumu, mwana harakati na Mratibu wa kuinua wanawake na uongozi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upande wa Zanzibar, TAMWA, alisema muda mrefu wanawake wamekua na nafasi ndogo katika nafasi za uongozi na ngazi za maamuzi na ndio maana waliamua kuwajengea uwezo na kuwashajiisha watumie fursa ziliopo kugombea uongozi.
 
Alisema TAMWA iliamua kufanya baada ya kuona Tanzania ina vijana wa kike wenye uwezo wa kuongoza , lakini  wanakabiliwa na vikwazo vingi katika safari ya kufikia huko na hili limeonkana wazi katika uchaguzi mkuu.
 
Mkufunzi na Mshauri elekezi, Imelda Urio, alieleza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wa kike kushiriki katika uongozi kwamba  mafunzo yalilenga kuwajengea uwezowa wa kufikia azma za vijana wa kike za kushika nafasi za uongozi kwenye taasisi mbali mbali huku wakiwa wamejizatiti kupambana na changamoto zinazoweza kuwakatisha tama.
 
Alisema tathmini inaonesha  idadi ya wanawake nchini inaendelea kuongezeka za uongozi kutokana na elimu inayotolewa katika jamii na utayari wa mtoto wa kike mwenyewe kujitokeza mbele na kuongoza.
 
Alibainisha kuwa baadhi ya wazazi wanawajengea mapema watoto wao wa kike uzoefu na kuwaunga mkono kwa njia tofauti.

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana wakike kwa lengo la kuisaidia jamii,
Mkurugenzi Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar TAMWA, Dr Mzuri Issa alisema, wameamua kuwakutanisha vijana wakike wenye vipaji tofauti na uthubutu ili kusaidia wanawake na jamii kiujumla.

Alisema dunia imeamini kuwa wanawake wana uwezo katika nafasi za uongozi kama anavyoweza kulea familia, vijana wa kike wakikaa pamoja na kupeana mawazo na kufanya maamuzi ya kusaidia jamii kufika sehemu nzuri.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka vijana wakike kuitumia vizuri nafasi hiyo, kwa kuendeleza vipaji na kuiga mfano kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan.

Akitolea mfano alipokua kijana, Dk. Mzuri alisema alipata nafasi ya kuajiriwa serikalini lakini hakuona kama nafasi nzuri kwake ya kuitetea jamii hasa wanawake, hivyo aliamua kujiunga na taasisi binafsi kwa lengo la kuisaidia wanawake kwenye nafasi za siasa, uchumi wa masoko na uongozi.

"Mfano sheria iliyotumika ya1985,  zilimkandamiza mtoto wa kike  na kulazimika watoto wa kike wanaopata ujauzito kufungwa Mahakamani kwa miaka 2, kupitia nafasi hiyo walifanikiaa kufanya utetezi kwa sheria zenye madhara na mifumo dume zilizowakandamiza wanawake" alisema.

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR 
Mwenyekiti wa Baraza la vijana Taifa, Yunus Juma Ali, alisema wakati huu wanawake wengi wamekua na muamko wa kufanya shughuli zamaendeleo, ingawa baadhi yao wapo nyuma kutokana na changamoto za kifamilia.
 
Si vyema wanawake kukaa nyuma katika harakati za maendeleo kwa kushiriki katika mabaraza hayo ili kupata ujuzi wa vitu mbali mbali na kufanya shughuli za ujasirimali na kujiajiri.
 
Alisema k katika kuunga mkono jitihada za wanawake kushiriki nafasi za uongozi Baraza limetoa elimu na kuwapa kipaumbele wanawake ambao ndio wengi katika baraza.



 
 
VIONGOZI WA DINI 
 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyuo vya Qur-an Wilaya ya Kati, Ali Haji Ubwa, alisema viongozi wa dini wanayo  nafasi kubwa kuhamasisha viongozi wa siasa kutoa nafasi zaidi kwa wanawake na vijana katika nyadhifa za uongozi ili kuwashirikisha katika kuleta maendeleo yanchi.
 
Mchungaji Yohana Madai Madai wa Kanisa la The Free Pentecostal Church of Tanzania,  alisema wanawake wana ushawishi mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya nchi.
 
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA
 
Katibu Mwenezi na habari chama cha ACT wazalendo, Salum Abdallah Bimani, alisema chama hicho kina toa fursa sawa za uongozi pia hakuna ubaguzi wa nafasi mbali mbali za uongozi.
 
Mwakilishi wa Jimbo la Dimani, Mwanaasha Khamis Juma, alisema nafasi za wanawake ndani ya baraza la Wawakilishi zimeongezeka kwenye majimbo kutoka Wawakilishi saba mwaka 2015 kufikia wanane  mwaka 2020.
 
Aliwataka wanawake kujiandaa vizuri kugombea hizo nafasi katika uchaguzi wa mwaka 2025 na changoto ziliopo wazigeuze fursa ya kuwashawishi kufanya vizuri.
 
Kwa mwaka 2020, wanaume waliojitokeza kugombea uwakilishi Zanzibar 190, walioshinda 42 na wanawake 61 na waliobahatika kushinda ni wanane 8 tu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kutambua umuhimu wa wanawake na kuwaaamini kwenye uongozi, amewapa nafasi mbalimbali ikiwemo nafasi za mawaziri, makatibu na hata Mhandisi mkuu kutumikia nafasi muhimu kwenye ngazi zamaamuzi.

Pia Dira ya mpango wa Maendeleo ya Zanzibar yamwaka 2020 hadi 2050 imeelezea kuboresha mfumo wa kisisa kupitia taasisi mbalimbali katika masuala ya uongozi.

Kwa mijibu wa makubaliano ya Maputo Protocol yaliyofanyika Julai 11, 2003 nchini Msumbiji kipengele namba tisa imeonesha haki ya wanawake kushiriki katika siasa na mchakato wakushiriki katika vyombo vya kutoa maamuzi, makubaliano haya yametoa fursa mbalmbali kwa mwanamke kugombea nafasi za uongozi na nchi kuweka mazingira mazuri ya wanawake kupata fursa hizo.

 
Mwisho


Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo ni vy

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan