Skip to main content

HUKUMU ALIYEDAIWA KUMBAKA MTOTO WA KAMBO CHAKE CHAKE LEO

  


NA HAJI NASSOR, PEMBA::

SHEMSA Hakim Khamis wa Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, ameiambia mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini Pemba kuwa, mume wake hajambaka mtoto wao wa kumlea, bali ni uongo alioutengeneza mtoto huyo.

 

Alidai kuwa, mtoto huyo amekuwa muongo mzoefu na mzushi, maana siku ambayo, alidai amebakwa na mumewake, alikuwa safarini kikazi kisiwani Unguja.

 

Shemsa ambae ni shahidi nambari nne kwenye shauri linalomkabili mumewake (mtuhumiwa Said Abdalla Issa), alidai kuwa mumewa alikuwa kisiwani Unguja kikazi siku hiyo aliyodaiwa kubaka.

 

Alidai kuwa, mtoto huyo ambae ni wa kulea, amekuwa muongo na alishawahi kumsingizia jirani wao mwanamme, kuwa alishawahi kumvulia nguo na kumuonesha sehemu zake za siri, ingawa walipofuatilia, haikuwa sahihi.

 

Mke huyo wa mtuhumiwa, alidai kuwa mtoto huyo pia alishawahi kukamatwa na barua ya mahaba, ndani ya mkoba wake wa mabuku ya skuli, akiashiria kuwa mtoto huyo alishaanza kubadilika kitabia zamani.

‘’Mume wangu hahusiki na kesi hii, maana hata siku ambayo alipelekwa hospitali kwa uchunguzi mtoto huyo, alishaoonekana kuingiliwa, ingwa sio mume wangu,’’alidai shahidi huyo.

 

Aidha shahidi huyo akiongozwa na wa utetezi Abied Mussa Omar, alidai kuwa alishakanywa na mama yake mzazi anaeishi nae kuwa, ni vyema mtoto huyo amrejeshe kwao eneo la Kiwani, kabla hajazusha balaa jengine.

 

Shemsa, aliendelea kuiaminisha mahakama kuwa, chanzo cha mtoto huyo kumtaja baba yake huyo wa kambu (mtuhumiwa), kuwa alimbaka, ni baada ya kumuadabisha kwa bakora.

 

‘’Ni kweli siku moja, baada ya kuwaita wenzake na kukila chakula chaote cha ndani, baba yake wa kambu (mtuhumiwa), alimchapa bakora, na kisha mtoto huyo kuahidi kumlipizia babayake huyo kwa kipigo hicho,’’alidai shahidi huyo.

 

Aidha shahidi huyo alidai kuwa, kuanzia hapo, ndio baada ya siku chache, alifikiwa na Polisi kutoka wilaya ya Chake chake, wakimuelezea kuwa, mume wake anakabiliwa na kesi ya ubakaji.

 

Baada ya kumaliza kutoa suahidi wake, Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alimpa nafasi wakili wa serikali, Ali Amor Makame, kumuuliza maswali shahidi huyo wa upande wa utetezi.

 

‘’Unakumbuka kuwa, awali ulikwenda kituo cha Polisi kumlalamikia mume wako (mtuhumiwa), kwa kosa la kumbaka mtoto wenu wa kulea,’’alihoji Wakili huyo.

 

‘’Utakubaliana na mimi kuwa, baadae wewe tulikuletea wito wa mahakama, kuja kutoa ushahidi, juu ya malalamiko yako na ulishindwa kuja, na leo uko umegeuka unamtetea mume wako,’’aliuliza Wakili wa serikali.

 

Hata hivyo, wakili huyo alimuuliza shahidi huyo, ikiwa anakumbuka vyema kuwa, mtoto wake huyo, alimpeleka hospitali kwa ajili ya uchunguuzi, mara baada ya mumewake kumbaka.

 

Hata hivyo shahidi huyo wa upande wa utetezi, ambae ni shahidi nambari nne, aliyakana maswali yote, aliyoulizwa na wakili wa serikali.

 

Baada ya maelezo hayo, wakili wa upande wa utetezi Abied Mussa Omar, alimueleza Hakimu Muumini Ali Juma kuwa, ameshafunga ushahidi wake, na kuiachia mahakama iendelee na taratibu nyingine.

 

Hivyo, hakimu huyo aliliahirisha shauri hilo hadi Novemba 28, mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa hukumu ya mtuhumiwa huyo, ambae yuko nje kwa dhamana.

  

 Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Said Abdalla Issa mkaazi wa Kengeja na Chanjamjawiri wilaya ya Chake chake, alidaiwa kumbaka mtoto wake wa kulea, tokea mwaka 2019.

 

Kufanya hivyo ni kinyume, na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.

 

                Mwisho     

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch