NA HAJI NASSOR, PEMBA::
MTUHUMIWA
wa ubakaji Mohamed Ali Hassan miaka 19, aliyekataa kusomewa hukumu yake Novemba
21, mwaka huu kwa madai ya kuuguliwa na mzazi wake, juzi tena Novemba 24, mahakama
imeshindwa kumsomea, baada ya kuanguka ghafla mahakamani hapo.
Mtuhumiwa huyo, alifika
mahakamani hapo akiwa mzima, hadi ilipofika wakati wake aliitwa na kupanda juu
ya kizimba cha mahakama ya makosa maaluma ya udhalilishaji ya mkoa wa kusini
Pemba, ili kusubiri kusomewa hukumu yake.
Wakati Hakimu Muumini Ali
Juma wa mahakama hiyo, akijitayarisha kuweka mambo sawa na mtuhumiwa huyo akiwa
tulia kuangali kinachoendelea, ndipo ghafla alipoanguka.
Mtuhumiwa huyo alianza
kuelezea kuwa hali yake imeshabadilika ghafla, huku akilalamikia maumivu jambo
ambalo liliishughulisha mahakama.
‘’Mheshimiwa Hakimu, kwa
hakika hali ya afya yangu imeshaharibika na sijiskilii, huku akishikilia baadhi
ya viungo vyake, akielezea kupata maumivu makali,’’alilalamikia.
Kisha mtuhumiwa huyo,
aliangua hadi chini mahakamani hapo, na sasa ikawa kazi kwa baadhi ya waliokuja
kusikiliza kesi na watendaji wa mahakama, kumsaidia kumpeleka hospitali ya
Chake chake kwa matibabu.
Hivyo Mahakama hiyo kwa juzi
Novemba 24 mwaka huu, kwa mara ya pili, imeshindwa kumsomea hukumu mtuhumiwa
huyo, ambae Novemba 21, pia alikataa kusomewa kwa madai ya kuumiliwa na mzazi
wake na yeye mwenyewe.
Hivyo Hakimu Muumini Ali
Juma, alimtaka mtuhumiwa huyo ambae yuko nje kwa dhamana, kwenda kuhangaikia
matibabu na amemtaka arudi tena mahakamani hapo siku tatu zijazo mwaka huu, kwa ajili ya kusomewa
hukumu yake.
‘’Pamoja na mitihani na
dharura unazozipata hapa mahakamani na nje ya mahakama, bado mahakama
inakumbuka kuwa imefikia hatua ya hukumu, sasa kwanza katibiwe lakini Novemba
30 uje ili tuendelee,’’alisema Hakimu Muumini.
Awali Mwendesha mashataka wa
serikali Ali Amour Makame, alimueleza hakimu wa mahakama hiyo kuwa, shauri hilo
lipo kwa ajili ya hukumu.
Alidai kuwa, baada ya upande
wao kufunga ushahidi na mtuhumiwa kujitetea, nae kufunga ushahidi, juzi Novemba
24, mwaka huu, ilikuwa ni siku yake ya kusomewa hukumu.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, kijana huyo bila ya halali na bila ya ridhaa ya wazazi wa mtoto wa
kike, alimbaka mtoto huyo mwenye miaka 16, akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa.
Alidai kuwa, siku hiyo mtuhumiwa alimuingilia mtoto huyo katika mwaka 2019, majira ya mchana, jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
(kumradhi: Picha iliyotumima sio halisi)
Mwisho
Comments
Post a Comment