Skip to main content

Posts

KAZI 529 ZA WAANDISHI WA HABARI ZASHINDANISHWA KUWANIA TUNZO ZANZIBAR

  NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR JUMLA ya kazi 529 za waandishi wa habari zimewasilishwa TAMWA kwa ajili ya kuwania tuzo za umahiri za uandishi wa habari za takwimu za wanawake na uongozi. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar, (TAMWA – ZNZ), Dkt. Mzuri Issa,amesema miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na vipindi vya redio, televisheni, makala za magazeti na kutoka katika mitandao ya kijamii zilizoandikwa na kurushwa katika vyombo vya habari kuanzia mwezi Januari hadi Disemba 31, 2023. Dk Mzuri amesema lengo la tuzo hizo ni kuhimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao na vyombo vya habari kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa masuala ya wanawake katika uongozi na kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi. “Kazi hizo zinaonesha ni jinsi gani waandishi wamekuza mwamko wa kuandika habari za uongozi kwa wanawake ambapo zinashajihisha wanawake na vijana wakike kujiamini zaidi na kuwa na matuma...

AFISI YA MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR: 'WANANCHI ANDIKENI, WASILISHENI MAMALAMIKO YANEU KWETU'

  Na Faki Mjaka-AMM-ZANZIBAR@@@@ Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar Hamisa Mmanga Makame amewaomba wananchi wenye Malalamiko na kadhia mbali mbali kuandika malalamiko hayo na kuyawasilisha katika Afisi ya Mwanasheria Mkuu ili kusaidiwa kupata ufumbuzi.   Amesema katika Afisi yao lipo Faili maalum kwa ajili ya malalamiko ya Mwananchi yeyote ili pale anapoyawasilisha, Afisi iweze kuyafanyia kazi malamiko hayo.   Wakili Hamisa amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Mangapawani Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati Afisi ya Mwanasheria Mkuu ilipoenda kutoa elimu ya masuala mbali mbali ya kisheria kwa wananchi hao ikiwa ni shamra shamra ya wiki ya sheria Zanzibar.   Amefahamisha kuwa, pale Mwananchi atakapoandika malalamiko yake dhidi ya Taasisi yoyote ya kiserikali, Afisi ya Mwanasheria Mkuu huchukua jukumu la kuwaita walalamikiwa kwa lengo la kutafuta suluhu dhidi ya malalamiko hayo.   “Mwananchi anapoandika malalamiko yake, sisi tu...

WANANCHI SHUNGI: 'MAJI YA ZAWA ''BUL BUL'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema kwa muda mrefu sasa, hawana shida tena ya huduma ya maji safi na salama, kufuatia urekebishaji mkubwa uliofanywa na Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA, tawi la Pemba. Walisema kwa sasa wanapata nafasi ya kujipangia muda wao wa shughuli za kilimo, biashara, wajasiriamali na wanaokwenda ofisini, baada ya kuwepo kwa huduma hiyo ya uhakika. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema haijawahi kutokea, kwa mud mrefu kuwa na huduma hiyo kwa uhakika, ingawa sasa miaka karibu mitatu hawana wasi wasi. Walisema, kuwa shughuli zao za kujitafutia huduma za chakula na safari nyingine sasa, zimekuwa zikipangika vyema, kwani hapo awali walikuwa wakisuumbuka kutokana na huduma hiyo. Mmoja kati ya wananchi hao Asma Said Abdalla wa Chanjamjawiri, alisema kwa upande wake sasa, amepata utulivu wa kujipangia shughuli zake, kutokana na uwepo wa uhakika wa huduma yam aji safi na sal...

SERIKALI YA WANAFUNZI ‘IPA’ PEMBA YAPATA VIONGOZI WAPYA

  NA MARYAM NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa serikali ya wanafunzi Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar, (IPA) tawi la Pemba, wamewataka viongozi wa chuo hicho, kutatua changamoto zinazowakabili kwa wakati. Ombi hilo, limetolewa na Naibu waziri mkuu wa Serikali ya wanafunzi chuoni, Rashid Khamis Yussuf, mara baada ya kuapishwa na kupata cheo hicho huko mjini Chake chake. Alisema, chuo hicho kinakabiliwa na changamoto lukuki, ambazo zinashindwa kupatiwa ufumbuzi kwa wakati sahihi, jambo ambalo linakwamisha maendeleo kwa wanafunzi. Alisema kuwa, kuna kipindi walikuwa na shida ya huduma maji katika chuo hicho, na ilidumu kwa muda mrefu na muhasibu alishindwa kuchukuwa fedha, ili kulitatua tatizo hilo. “Kuna wakati tulikuwa na shida ya maji katika Chuo chetu, na tatizo hilo lilidumu kwa muda, bila ya kupatiwa ufumbuzi na muhasibu yupo, ingawa alishindwa kulishughulikia,”alisema. Mwanafunzi Deo Mabula Alfred, alisema changamoto inayowakera ni kutokupewa vitambulisho, kile cha mit...

WAZIRI LEILA AWAPA KONGOLE WANAFUNZI NG'OMBENI 'A' MKOANI KWA UFAULU

NA SALIM HAMAD, PEMBA @@@@   Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Leila Mohamed  Mussa amewapongeza wanafunzi wa Skuli ya Msingi  Ngo’mbeni  'A'  Wilaya ya Mkoani waliofulu vizuri  michepuo ya Darasa la saba waliofanya mitihani yao mwaka 2023. Waziri Leila aliyasema  hayo huko Mkoani Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akizungumza na Walimu,Wazazi na Wanafunzi  katika sherehe ya kuwapongeza wanafunzi  wa Skuli  hiyo waliofaulu michipuo na kuwa  Skuli ya kwanza  katika Mkoa wa Kusini Pemba.  jumla ya wanafunzi 157  waliofanya Mitihani ya Darasa la saba katika Skuli ya Ng’ombeni (A) na katoa  michipuo 51 ambapo idadi hiyo imeifanya Skuli hiyo kuwa kwanza  kwa ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema haikuwa kazi rahisi waliofanya wanafunzi hao kwani walipitia mazito wakati wa masomo yao,hivyo hawanabubudi kuzidisha jitihada zaidi katika kuona wanafika mbali na kutimiza ndoto zao. Alise...

TAMWA -ZNZ: 'SHERIA MPYA YA HABARI, MWANGA WA KUWATOA WOGA WAANDISHI WA HABARI'

NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR@@@@ Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar Dk Mzuri Issa amesema kuwepo kwa Sheria mpya ya habari inayokwenda sambamba na maendeleo ya Sayansi na teknolojia itatowa fursa kwa waandishi wahabari kufanya kazi zao kwa ufanisi. Akitowa taarifa kwa vyombo vya habari amesema pamoja na kuwepo maoni mengi yaliyotolewa na waandishi wahabari pamoja na wadau na watetezi wa haki za binadamu kuhusu mabadiliko ya sheria ya zamani iliodumu kwa takribani muongo mmoja bado kunahitajika kuwepo kwa sheria rafiki inayokwenda na wakati wa sasa. Dk Mzuri amewapongeza wadau mbali mbali walioshirikiana na vyombo vya habari ikiwemo Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya msingi ya kupata habari kama inavyosema Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 18, pamoja na Mikataba ya Kikanda inayosimamia uhuru wa vyombo vya habari nchini. “Wakati tunaingia mwaka mpya 2024 waandishi na vyombo vya habari wana matumaini makubwa ya kuzita...

HAROUN: 'KITUO CHA UTATUZI MIGOGORO ZANZIBAR KIVUTIZI KWA WAWEKEZAJI'

  NA FAKI MJAKA, AMM  -ZANZIBAR@@@@   Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleiman amesema kuanzishwa kwa Sheria ya Usuluhishi na Kituo cha Utatuzi wa Migogoro Zanzibar kutaongeza imani ya wawekezaji kuja nchini kuwekeza miradi yao ya kimaendeleo.   Amesema kituo hicho kitakapoanzishwa kitawahudumia wenyeji na wageni na hivyo kupunguza kasi ya watu kuepelekana mahkamani hasa pale migogoro ya kibiashara na uwekezaji inapotokea.   Waziri Haroun aliyasema hayo huko katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege alipofungua Mkutano wa Wadau uliojadili Rasimu za Miswada ya Sheria ya Usuluhishi na Sheria ya kuanzisha Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro Zanzibar uliohudhuriwa na wadau kutoka sekta mbali mbali nchini.   Alisema hali ya Zanzibar kiuchumi inaimarika sana kutokana na juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi za kuwavutia Wawekezaj...

KESI TUHMA YA KUUA KWA MAKSUDI PEMBA: 'PP HATUJAMALIZA MAELEZO YA MASHIDI KWANZA'

  NA MARYAM NASSOR, PEMBA @@@@  WATUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa  makusudi, inayowakabili vijana wanne akiwemo Yassir  Mussa Omar ‘Makababu’ na wenzake , wote wakazi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake,  wameendelea kusota rumande, baada ya upande wa mashtaka, kushindwa kukamilisha maelezo ya kesi na mashahidi kwa wakati. Mara baada ya watuhumiwa hao kuwasili mahakamani hapo wakitokea rumande, Mwendesha Mashtaka kutoka   Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Pemba, Mohamed Abdallah Juma, alidai kutokamilisha kwa baadhi ya mambo muhimu.   Alimueleza, Jaji wa Mahakama kuu Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa, kesi hiyo ipo mahkamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ingawa bado maelezo ya shauri hilo hayajakamilika. “Mheshimiwa Jaji leo (jana), kesi hii ipo kwa ajili ya kutajwa,   lakini bado hatujakamilisha maelezo ya   kesi na mashahidi , hivyo tunaomba utupangie tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa tena,”alidai. Baada ya maelezo hayo, Jaji wa mahak...

'Wanaume ungeni mkono uzazi wa mpango'

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA LICHA ya elimu ya uzazi wa mpango inayotolewa kwenye vituo vya afya lakini bado kuna baadhi ya akinababa huwazuia wake zao, jambo ambalo linaweza kusababisha athari kwa mama mwenye matatizo katika mfumo wake wa uzazi. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi wananchi wa shehia ya Shungi Wilaya ya Chake Chake walisema, madaktari wanajitahidi kutoa elimu kuhusiana na uzazi wa mpango, ingawa kuna baadhi ya wanawake wanaendelea kupata athari kutokana na kutofuata huduma za uzazi wa mpango. Walisema kuwa, uzazi wa mpango ni muhimu kwa wanawake kwani wanapata kupumzika, kuimarika kiafya na kumfanya mtoto akue vizuri, hivyo ipo haja kwa akina baba kuangalia hali ya afya kwanza, ndipo wakatae uzazi wa mpango. ‘’Elimu ipo kwa sababu tunapokwenda vituo vya afya madaktari wanajitahidi kutuelimisha, lakini baadhi ya wanaume wanahisi kama tunataka kufungwa uzazi, jambo ambalo sio sahihi,’’ walisema wananchi hao. Mwananchi Fatma Said Khalfan alisema kuwa, kuna b...

KESI TUHMA ZA KUUA KWA MAKSUDI PEMBA KUNGURUMA ASUBUHI HII MAHKAMA KUU

    NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KESI ya tuhma ya mauwaji kwa maksudi, inayowakabili vijana wanne, akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ na wenzake, wote wakaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, inatarajiwa kunguruma tena leo Mahakama kuu Zanzibar kisiwani Pemba. Watuhumiwa wingine wanaotarajiwa kuwasilia mahkamani hapo wakitokea rumande ni Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 na Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, ambao wanatuhumiwa kumuua kwa maksudi kijana Said Seif Kombo. Awali kesi hiyo kwa mara ya mwisho ilinguruma mahkamani hapo, ingawa kwa siku hiyo ya Novemba 30, mwaka jana, haikuendelea kusikilizwa wala kutolewa ushahidi, baada ya Jaji wa mahkama kuu Pemba, kutokuwepo mahkamani hapo. Ambapo kwa siku hiyo kesi hiyo, ilisikilizwa na Hakim wa mahkama ya mkoa Chake chake, ambae kisheria hana mamlaka ya kusikiliza kesi za mahakama kuu, vyenginevyo kuwe na utaratibu maalum. Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Chake chake aliyepokea watuhumiwa Ziredi A...