NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
WANANCHI
wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema kwa muda mrefu sasa,
hawana shida tena ya huduma ya maji safi na salama, kufuatia urekebishaji
mkubwa uliofanywa na Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA, tawi la Pemba.
Walisema kwa
sasa wanapata nafasi ya kujipangia muda wao wa shughuli za kilimo, biashara,
wajasiriamali na wanaokwenda ofisini, baada ya kuwepo kwa huduma hiyo ya
uhakika.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema haijawahi kutokea, kwa mud
mrefu kuwa na huduma hiyo kwa uhakika, ingawa sasa miaka karibu mitatu hawana
wasi wasi.
Walisema,
kuwa shughuli zao za kujitafutia huduma za chakula na safari nyingine sasa,
zimekuwa zikipangika vyema, kwani hapo awali walikuwa wakisuumbuka kutokana na
huduma hiyo.
Mmoja kati
ya wananchi hao Asma Said Abdalla wa Chanjamjawiri, alisema kwa upande wake
sasa, amepata utulivu wa kujipangia shughuli zake, kutokana na uwepo wa uhakika
wa huduma yam aji safi na salama.
Nae Zulekha
Nassor Hilali, alieleza kuwa hata kwa waliojipanga kuyatumia maji hayo kwa
ajili ya kuendelea kilimo, wamekuwa na uhakika kwa sasa.
Kwa upande
wao wananchi wa kijiji cha Misooni, Mbarouk Idrissa Omar, Asha Suleiman Hamad
na Amina Suleiman Juma, walisema hata kijijini kwao, kwa sasa huduma hiyo
inafika.
Walieleza kuwa,
baada ya kutoa kilio cha muda mrefu, hatimae ZAWA walirekebisha kisima chao
kilichopo Matuleni na sasa huduma yam aji sio shida tena shehia mwao.
‘Kwa sasa
tunafua na kutumia kwa shughuli nyingine maji hayo muda tuutakao, maana kama
umeme upon a hakuna hitilafu kwenye kisima chetu, maji yanatoka saa 24,’’walisema.
Hata hivyo,
waliishauri ZAWA kuangalia uwezekano wa kuwajengea minara ya tanki ya
kuhifadhia maji hayo, ili umeme unapokatika au ikitokezea hitilafu mfano wa
mashine kuharibika wawe na uhakika.
Sheha wa
shehia ya Shungi Hamad Ramadhan Soud, alikiri kuwepo kwa huduma yam aji safi na
salama saa 24, ambayo ilitokana na mikakati thabiti ya ZAWA, ya kukifanyia matengenezo
kisima chao.
Alieleza kuwa,
ni kweli wananchi walikuwa wakilalamikia kuzorota kwa huduma hiyo, ikiwemo
kupatikana nyakati za usiku, au kutoka wiki mara moja, ingawa kwa sasa hali
imebadilika.
‘’Ni kweli
ndani ya shehia ya Shungi, hakuna kijiji ambacho kinamiundombinu ya huduma ya maji
safi na salama na kisha kukosekana kwa huduma hii,’’alieleza.
Wakati huo
huo sheha huyo, aliwataka wananchi kuwendelea kuwa walinzi wa miundombinu ya maji
safi na salama, ili iendelee kuwanufaisha wao na vizazi vijavyo.
‘’Wananchi
waelewe kuwa, wapo baadhi ya wananchi wingine kwenye shehia mbali mbali
wanaililia huduma hiyo, sasa kama Shungi ipo wahakikishe wanaitunza ili iwe
endelevu,’’alieleza.
Mkuu wa Mtandao
wa maji Pemba kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA tawi la Pemba Juma Omar Khamis,
alisema siri ya wananchi wa shehia hiyo na vijiji vyake kupata huduma kwa saa 24,
ni kuwepo visima viwili kwa ajili yao.
Alisema wananchi
hao wanapata lita 70,000 kwa saa moja, ambapo ni sawa la lita 1,680,000 kwa siku
ambazo zinazalishwa kwenye visiwa viwili, huku kimoja kikizalisha lita 36,000
na chingine lita 17,000 kwa saa moja.
Hata hivyo
alisema wanampango wa kuwajengea tanki maalum la kuhifadhi maji, ili
inapotokezea hitilafu ya kuzimwa kwa umeme au kuharibika mashine huduma iendelee.
Shehia ya Shungi
iliyopo wilaya ya Chake chake Jimbo la Chonga, inao wananchi 3,884 ambapo
inaundwa na vijiji vya Missoni, Shungi, Kiziwani, Chanjamjawiri, inayomiundombinu
ya elimu, afya na barabara.
Mwisho
Comments
Post a Comment