NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR@@@@
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar Dk Mzuri Issa amesema kuwepo kwa Sheria mpya ya habari inayokwenda sambamba na maendeleo ya Sayansi na teknolojia itatowa fursa kwa waandishi wahabari kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Akitowa taarifa kwa vyombo vya habari amesema pamoja na
kuwepo maoni mengi yaliyotolewa na waandishi wahabari pamoja na wadau na
watetezi wa haki za binadamu kuhusu mabadiliko ya sheria ya zamani iliodumu kwa
takribani muongo mmoja bado kunahitajika kuwepo kwa sheria rafiki inayokwenda
na wakati wa sasa.
Dk Mzuri amewapongeza wadau mbali mbali walioshirikiana na
vyombo vya habari ikiwemo Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata haki
yao ya msingi ya kupata habari kama inavyosema Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984
kifungu cha 18, pamoja na Mikataba ya Kikanda inayosimamia uhuru wa vyombo vya
habari nchini.
“Wakati tunaingia mwaka mpya 2024 waandishi na vyombo vya
habari wana matumaini makubwa ya kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili
katika utendaji wao wa kazi,” Dk Mzuri.
Akizitaja sheria zinazohitaji kufanyiwa marekebisho amesema
ni pamoja na Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu no 5 ya
mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no 8 ya mwaka 1997 pamoja na
sheria ya Utangazaji no 7 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na sheria no 1
ya mwaka 2010.
“Tuna hamu ya kupata Sheria mpya kwa kupitia kauli na
matamshi ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiongozwa na
Rais na Waziri mwenye dhamana ya habari ambae alieleza wakati wa kutimiza siku
mia moja lakini kwa bahati mbaya hadi leo Sheria hizo hazijarekebishwa,” Dk
Mzuri.
Mapema Afisa Mradi wa Uhuru wa habari kutoka TAMWA,Zanzibar
Zaina Mzee amesema kwa miaka mingi Sheria hii ya habari imekuwa kikwazo kwa
waandishi wahabari na vyombo vya habari kwa ujumla kufanya kazi kwa ufanisi.
Akiwasilisha mada Mshauri Elekezi kutoka Chuo Kikuu cha
Zanzibar (ZU) Said Suleiman Ali katika
mkutano uliwashirikisha wadau wa habari amesema Sheria ya Habari ina mapungufu
mengi amabayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka kwa lengo la kuisaidia
jamii.
“Uhuru wa habari si wa waandishi pekee, ni wa jamii nzima,
kwani ukimnjima uhuru mwandishi kutekeleza majukumu yake ipasavyo na utainyima
jamii fursa ya kupata habari,” Said Suleiman Ali ((Z).
Akiwasilisha Ripoti ya Uchambuzi wa Sheria ya Habari
Zanzibar Juma Abdalla amesema Sheria ya habari inahitaji maboresho makubwa kwa
sababu inaonekana kuwa na vikwazo kadhaa vinavyorejesha nyuma maendeleo na
ufanisi kwa waandishi wa habari.
“Sheria ina mapungufu mengi na waandishi wanailalamikia kwa
muda mrefu hivyo tunaomba irekebishwe kwa faida ya waandishi na kwa jamii,”
Nao wadau wa habari walikutana kujadili masuala ya Sheria
hizo wametowa maoni yao kwa kusema Sheria hiyo imelalamikiwa kwa takribani
miaka kumi na mitano tokea 2010 hadi leo haijafanyiwa marekebisho.
Salim Said Salim
Mwandishi Mwandamizi amesema kwa ulimwengu wa sasa wa Sayansi na
Teknologia ipo haja ya kuwa na Sheria zinazomlinda mwandishi wahabari na kuleta
tija kwa jamii
“Kwa sababu kuna sheria zimeeleza adhabu kubwa kwa mwandhishi
wahabari endapo atafanya kosa, sheria kama hizo zinakwamisha waandishi na
kupelekea kufanya kazi zao kwa woga,” Salim Said.
Shifaa Said kutoka Baraza la Habari Tanzania Zanzibar
amesema waandishi wahabari kushirikiana kwa pamoja kujadili changamoto
zinazojitokeza katika sheria hizo na kuendelea kuzifanyia uchambuzi na
kuishauri Serikali kuzitafutia ufumbuzi
kwa sababu ni za mda mrefu.
Mradi wa kuimarisha masuala ya uhuru wa habari wa miaka
miwili wenye lengo la kuendeleza mapitio ya uhuru wa Sheria za habari (ARFEL),
Unaofadhiliwa na Common Wealth Foundation.
Comments
Post a Comment