NA SALIM HAMAD, PEMBA @@@@
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Leila Mohamed Mussa amewapongeza wanafunzi wa Skuli ya Msingi Ngo’mbeni 'A' Wilaya ya Mkoani waliofulu vizuri michepuo ya Darasa la saba waliofanya mitihani yao mwaka 2023.
Waziri Leila aliyasema hayo huko Mkoani Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wakati akizungumza na Walimu,Wazazi na Wanafunzi katika sherehe ya kuwapongeza wanafunzi wa Skuli hiyo waliofaulu michipuo na kuwa Skuli ya kwanza katika Mkoa wa Kusini Pemba.
jumla ya wanafunzi 157 waliofanya Mitihani ya Darasa la saba katika Skuli ya Ng’ombeni (A) na katoa michipuo 51 ambapo idadi hiyo imeifanya Skuli hiyo kuwa kwanza kwa ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema haikuwa kazi rahisi waliofanya wanafunzi hao kwani walipitia mazito wakati wa masomo yao,hivyo hawanabubudi kuzidisha jitihada zaidi katika kuona wanafika mbali na kutimiza ndoto zao.
Alisema suala la kutafuta elimu ni jambo la msingi ambalo Vijana wanapaswa kuendelea kupambana ili kuweza kujijengea msingi mwema wa maisha yao ya hapo baadae.
Alisema kumekuwa na Changamoto kadhaa wanazokumbanazo wanafunzi Mashuleni ikiwa ni pamoja kufanyiwa Vitendo Vya Udhalilishaji na kupelekea baadhi yao kushindwa kutimiza malengo yao huku Wizara na Wadu wengine wakiendelea kupambana katika kupiga vita Vitendo hivyo.
‘’Ni wapongezeni sana wanafunzi mmefanya Vizuri kwa kuongeza kiwango Cha Ufaulu mmekuwa wa kwanza kwenye Mkoa wa Kusini Pemba ,bila shaka kwenye mafanikio kuna magumu mengi mmepitia ninacho waomba muendelee na jitihada zenu naamini mtaweza kufika mbali’’alisema Waziri Leila.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja alisema Mafanikio hayo yaliyopatikana yametokana na Mashirikiano ya pamoja kwa Walimu ,wanafunzi Wazee na Jeshi la Polisi Mkoa huo.
Alisema kabla ya wanafunzi hao kufanya mitihani yao kulikuwa na misako maalumu iliyofanywa na kamati za Skuli hiyo, Wazazi na Jeshi la Polisi katika kuwasaka wanafunzi waliotoroka Mashuleni na kufanikiwa kuwarudisha na katia yao ni miongoni mwa waliofau michipuo.
''Mafanikio haya yametokana na Mashirikiano ya Wadau Mbali Mbali ikiwemo Jeshi la Polisi tumekuwa tukipita kila kijiji katika Wilaya hii ya Mkoani kuwasaka watoro tukafanikiwa kuwarejesha lakini jambo la kufurahisha tumeambiwa miongoni mwa waliofaulu ni wale ambao tayari walishatoroka Mashuleni’’alisema Mjaja.
Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Aamali Pemba,Mohamed Naasor Salum alimshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo Khatib Juma Mjaja kwa juhudi alizozichukua kwa kushirikiana na kamati ya Skuli hiyo na Jeshi la Pilisi kwa kupambana na watoto watoro jambo lililosababisha kupunguza idadi ya ziro kwenye Wilaya ya hiyo.
Akisoma risala katika hafla hiyo Maalim Mstaafu wa Skuli hiyo Bi Mwanajuma Hassan Kaduara alisema pamoja na matokeo hayo mazuri waliyoyapata lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbli katika Skuli hiyo ikiwemo uhaba vikalio pamoja na vyumba Vya kusomea.
Katika hafla hiyo Waziri Leila aliwazawadia wanafunzi hao kwa Vifaa mbali mbali vya Masomo ikiwemo mabuku pamoja na Fedha taslim ili kuwa ni mootisha kwa wanafunzi wengine.
MWISHO.
Comments
Post a Comment