Skip to main content

UTAMADUNI WA KUTOBOA, KUWEKA KIPINI CHA PUA, WAIBEBA MICHEWENI, WANAUME WAKIRI KUVUTIWA

 

  



NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

 ‘’TUMESHAWAHI kusimamisha shughuli ya harusi kwa dakika 10, mke asichukuliwe, baada ya kugundua hatujamtia pambo la kipini cha pua,’’anasema Rehema Faki Shehe (60) wa Kwale Micheweni Pemba.

Ilishazoelekea kuwa, kuwa mapambo ni aina ya mafuta, podari, pete, mkufu, udi, wanja na hina, ingawa kwa wanawake wilaya ya Micheweni, kipaumbele ni utoboaji wa pua kwa ajili ya utiaji wa kipini.

Utamaduni wa utoboaji (utomoaji) wa pua tena ya upande wa kushoto, wenyewe wanawake wa Micheweni waliurithi zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Kwa mfano, Rehema Faki Shehe (60) alimkuta bibi yake wakati akiwa huo akiwa na miaka 50, akiwa ametobolewa tundu la upande wa kushoto ya pua, akiwa na kipini.

KINA MAAGA GANI KIPINI CHA PUA?

Sharifu Massoud Hamad (60) wa Kwale Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, anasema moja ni tofauti kati ya mwanamke na mwanamme.

Anaona hata unapokuta wamevaa mavazi yenye kufanana, lakini dalili kubwa ya tofauti hiyo, ni kumuangalia kwenye mlango wa tundu ya pua ya upande wa kushoto, atakuwa na sehemu ya kuwekea kipini.

‘’Ukifika miaka kati ya mitano hadi minane, lazima kwa mtoto wa wilaya ya Micheweni apelekwe kwa mtoboaji na afanye hivyo, ili ajitayarishe kwa baade kuweka kipini,’’anasema.

Saada Said Kombo (68) anasema, kwa umri wake huo hakukuwa na dada yake wala mdogo wake wa kike ambae hakutobolewa pua, kwa ajili ya kuwekewa kipini.

Anasema kila familia imekuwa na mtoboaji wake maalum, tena huwa bila ya malipo, kwa kila mmoja.

NANI ANAVA AKIPINI?

Kumbe uvaaji wa kipini ni kwa ajili ya mwanamke ambae tayari ameshaolewa pekee na sio mwengine, ambae bado hajafunga ndoa.

Hii wanasema, utamaduni unasindikiza kwa namna ya kumtofautisha kati ya mwari ‘kigori’ na mtu aliyekwishaolewa au mjane.

Aisha Hamad Shamata (65) anasema, tena ilishamtokezea mara mbili katika maisha yake, bibi harusi kumzuia kwa dakika 10, baada ya kusahau kumtia kipini.

Anasema, hakuna hata pambo moja ambalo ni muhimu na la lazima kwa harusi wa kike wa Micheweni, kama sio kipini cha pua.

Fatma Hamad Ali (40) anasema, hata yeye alipoolewa alilazimika wiki tatu kabla ya harusi yake, kutobolewa pua, kwa vile hakulelewa eneo hilo na alikosa huduma hiyo awali.

‘’Kwa mfano mimi sikulelewa Micheweni, ingawa ndio kwetu lakini nililazimika kutobolewa, ili kuiheshimisha ndoa na familia yangu,’’anasema.



Kweli anasema, mwanamke alimpenda mno baada ya kumkuta akiwa na kipini cha pua, na hayo anasema aliyabaini siku waliokwenda kuwasalimu wazazi, wiki mbili baada ya harusi yao.

Aisha Hashim Said (25) anasema wao ni utamaduni waliourithi na imekuwa vigumu hasa ikiwa utalelewa Micheweni, kuuacha.

Halima Ibrahim Khamis (30) na mwenzake Hadia Ramadhan Himid (22) wanasema, ingawa siku ya kutobolewa hupata maumivu, lakini haiwi kikwazo kwa wingine kutobolewa.

‘’Maumivu yake kama sindano ya kawaida, lakini ninachoamini kama unataka uzuri, lazima kwanza uzurike,’’anasema Halima Ibrahim Khamis.

Maryam Issa Khamis anasema yeye alikataa kutobolewa pua akiwa na miaka 20, na aliolewa hadi sasa ana watoto watano, akiwa kwenye ndoa bila ya kipini.

‘’Kama hutaki kutobolewa, wenzako wingine wanakucheka wingine wanakuunga mkono na unaolewa bila ya shida,’’anasema.

WANAUME WA MICHEWENI WANASEMAJE?

 Wanasema, kama wanawake waliowaoa hawakuwakuta na utamaduni huo, huwa na maswali yanayokosa majibu vichwani mwao.

Kwa mfano Faki Khamis Kai (64) anasema, moja ya pambo ambalo haliishi hamu, ni uwepo kwa pua yenye kipini kwa mke wake.

Kwao suala la udi, hina, piko, podari na asumini yapo kama mapambo ya ujumla, ingawa utamaduni wa utoboaji wa pua na kuweka kipini huwa ndio kipaumbele.

‘’Hata sisi kwenye vikao vyetu, huwa tunataniana na kuelezena kuwa, ikiwa mwanamke hana kipini cha pua hana tofauti na mwanamme,’’anasema.

Khamis Juma Khamis (73) anasema kipini cha pua ndio mpango mzima kwa mke, na mapambo mingine kama udi, hina na piko ni vitu vya kuondoka.

‘’Hata kama mwanamke anaumwa, au wewe mwanamme unaumwa, bado mke anakuwa anakupendezesha kwa kule kuwa na mng’ara pua kwa kipini,’’anasema.

Kwao hawajali na wala hawashughuliki aina ya kipini, kiwe cha dhahabu, almasi, silva hata cha kutengeneza kwa mali ghafi zinazotoka Micheweni, kwao huvutia.



Issa Hamad Shehe (25) anasema hata vijana wa leo utamaduni wa utoboaji pua, wanaupenda kwa wake zao, maana ndio pambo lisilo na gharama.

‘’Udi mpaka uwe na shilingi 1,000 kila baada ya muda, piko na hina zinawakati huchakaa kama ilivyo kwa udi, lakini kipini mpaka mtu anafariki,’’anasema.

Kombo Haji Simba (35), anasema ni aibu kubwa kwao kuoa mke ambae mmetakana na familia yake, kukosekana kwa pambo la kipini cha pua.



HISTORIA YA UTOBOAJI WA PUA

Kwa zaidi ya karne tatu (miaka 300), hapo zamani wanawake wa jamii ya Kihindi na wale wa mwambao wa pwani hasa Tanga, walinza kutoboa sehemu katika pua.

Pia kwa wakati huo, halikuwa jambo la ajabu kuweka jino la dhahabu na hata kutoboa masikio yote mawili.

Ingawa historia inaonesha, unapotoboa pua, lazima kisha uweke kipini cha dhahabu, baada ya maumivu kupona na sio kweka jambo jingine lolote.

Kutoboa pua kumekuwepo kwa miaka mingi, katika ustaarabu tofauti ambao, umetumia kurejelea vitu tofauti.

Ukubwa wa mapambo ya kujitia puani yalikuwa na maana ya utajiri wa kifamilia kwa makabila katika Afrika na Mashariki ya Kati.

Na mithili ya pete za pua zinadaiwa kutolewa kwa marafiki wa kike wapya na waume zao, kama hatua ya usalama.

Vivyo hivyo, ustaarabu wa Amerika ya Kati na Kusini umetumia kutoboa kwa septamu na mapambo yao kama alama za hadhi.

Katika jamii ya kisasa ya Magharibi, kutoboa pua kunahusishwa na tamaduni anuwai kama punk, tamaduni mbadala, na tamaduni ya bohemia.



Kutoboa pua hakuhitaji tu tahadhari na uvumilivu wa maumivu, lakini muhimu zaidi kuliko inavyosikika.

Kutoboa ncha ya pua ya wima ni kutoboa pua ya kipekee na nadra, ambayo hutembea wima, kama jina linavyopendekeza, kutoka juu tu ya ncha ya pua hadi chini tu ya ncha ya pua.

Kwa sababu ya muundo wa pua yako, baa iliyopindika kwa kweli ni mapambo pekee yanayokubalika kwa aina hii ya kutoboa. 

 

ATHARI ZA UTOBAJI PUA USIOZINGATIA UTAALAMU

Maumivu ya pua, yanaweza kusumbua na kuumiza, na wakati mwingine yanaweza kusababishwa na homa, yenye kuambatana na mvutano wa misuli kwenye taya.

 

Daktari Issa Khamis Ali anasema lakini hata kwa mtobolewaji anaweza kukumbwa na shinda kwenye sehemu ya shingo, muoteo wa meno, muwasho usio wa kawaida, kwenye pua ndani na nje.

               Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...