NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
KESI ya tuhma ya mauwaji kwa maksudi,
inayowakabili vijana wanne, akiwemo Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ na wenzake, wote wakaazi
wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba, inatarajiwa kunguruma tena leo Mahakama
kuu Zanzibar kisiwani Pemba.
Watuhumiwa wingine wanaotarajiwa
kuwasilia mahkamani hapo wakitokea rumande ni Yassir Mohamed Juma miaka 23,
Anuwari Mussa Omar miaka 30 na Yassir Mussa Omar ‘Makababu’ miaka 29,
ambao wanatuhumiwa kumuua kwa maksudi kijana Said Seif Kombo.
Awali kesi hiyo kwa mara ya
mwisho ilinguruma mahkamani hapo, ingawa kwa siku hiyo ya Novemba 30, mwaka jana, haikuendelea
kusikilizwa wala kutolewa ushahidi, baada ya Jaji wa mahkama kuu Pemba,
kutokuwepo mahkamani hapo.
Ambapo kwa siku hiyo kesi hiyo,
ilisikilizwa na Hakim wa mahkama ya mkoa Chake chake, ambae kisheria hana
mamlaka ya kusikiliza kesi za mahakama kuu, vyenginevyo kuwe na utaratibu
maalum.
Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Chake
chake aliyepokea watuhumiwa Ziredi Abdull-kadir Msanifu, alilighairisha hauri
hilo, hadi asubuhi hii, kuendeshwa na Jaji wa mahkama kuu.
‘’Mahkama hii kisheria haina
uwezo wa kusikiliza shauri lenu, kwani ni kesi za mahkama kuu, na Jaji wenu hayupo,
itabidi murudi rumande hadi Januari 23 mwaka 2024 (leo),’’alisema
Hakimu huyo.
Kwa mara ya kwanza kesi hiyo, ilisomwa
mahakama kuu, Novemba 14, ambapo siku hiyo ikaghairishwa tena hadi Novemba 30,
kabla ya kutakiwa kurudi tena mahakama kuu, leo Januari 23, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka
kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja,
wanadaiwa kufanya mauwaji hayo ya maksudi.
Ilidai kuwa, wote kwa pamoja,
walitenda kosa hilo Oktoba 16 mwaka 2023, baina ya majira ya saa 7:00 mchana na
saa 11:00 jioni, katika eneo la Machaomane wilaya ya Chake chake.
Ilidaiwa kuwa, kufanya hivyo ni
kosa kinyume na vifungu vya 189 na 190 vya sheria nambari 6 ya mwaka 2018
sheria ya Zanzibar, iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi.
Hata hivyo watuhumiwa hao,
waliieleza mahakama hiyo kuu kuwa, wanaewakili katika kesi yao hiyo, ingawa kwa
siku ya kwanza, hakuweza kufika mahakamani, kutokana na sababu mbali mbali.
Mwisho
Comments
Post a Comment