NA MARYAM NASSOR, PEMBA @@@@
WATUHUMIWA wa kesi ya kuua kwa makusudi, inayowakabili vijana wanne akiwemo Yassir Mussa Omar ‘Makababu’ na wenzake , wote wakazi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, wameendelea kusota rumande, baada ya upande wa mashtaka, kushindwa kukamilisha maelezo ya kesi na mashahidi kwa wakati.
Mara baada
ya watuhumiwa hao kuwasili mahakamani hapo wakitokea rumande, Mwendesha Mashtaka
kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka
Pemba, Mohamed Abdallah Juma, alidai kutokamilisha kwa baadhi ya mambo muhimu.
Alimueleza, Jaji wa Mahakama kuu Ibrahim Mzee
Ibrahim kuwa, kesi hiyo ipo mahkamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ingawa bado
maelezo ya shauri hilo hayajakamilika.
“Mheshimiwa
Jaji leo (jana), kesi hii ipo kwa ajili ya kutajwa, lakini bado hatujakamilisha maelezo ya kesi na mashahidi , hivyo tunaomba utupangie
tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa tena,”alidai.
Baada ya
maelezo hayo, Jaji wa mahakama kuu Zanzibar kanda ya Pemba, Ibrahim Mzee
Ibrahim, alimuuliza wakili wa upande wa utetezi, Saleh Said Mohamed kuwa ana
pingamizi yoyote, juu ya ombi hilo.
Wakili huyo alidai kuwa, hana pingamizi yoyote
juu ya ombi hilo, ila aliuomba upande wa mashtaka kujihimu kukamilisha maelezo ya mashahidi, ili
watuhumiwa hao wajuwe hatma yao.
“Mimi sina
pingamizi na ombi la upande wa mashtaka, ila nawaomba wajihimu kukamilisha
maelezo hayo, ili watuhumiwa hawa wajuwe hatma ya kesi inayowakabili,’’alidai.
Jaji wa
mahakama hiyo, aliwauliza upande wa mashtaka kuwa, lini watakuwa wameshakamilisha
maelezo ya kesi na mashahidi na kujibu kuwa wanahitaji wiki mbili.
Jaji huyo
alisema kuwa, upande wa mashtaka wanatakiwa kukamilisha hayo yote ifikapo Febuari
5, mwaka huu na mahakama iwaite jopo la wazee wa mahakama, ili kushirikiana nao
kwa kesi hiyo.
Kwa mara ya
kwanza shauri hilo, lilisomwa mahakamani hapo Novemba 14 mwaka 2023, na kughairishwa
kwa kutokana na kutokuwepo kwa Jaji wa mahakama kuu.
Awali ilidaiwa
mahakamani hapo, na Mwendesha Mashtaka kutoka O fisi ya Mkurugenzi wa mashtaka
kuwa, watuhumiwa hao Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwar Mussa Omar miaka 30,
na Ali Mussa Omar ‘Mkapa’ miaka 29, kwa pamoja wanadaiwa kumuua kwa makusudi,
kijana Said Seif Kombo.
Ilidaiwa
kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16 mwaka 2023,
baina ya majira ya saa 7:00 mchana na saa 11:00 jioni, katiak eneo la
Machomanne wilaya ya Chake chake, mkoa wa kusini Pemba.
Kufanya
hivyo ni kosa, kinyume na vifungu vya 179 na 180 vya sheria namba 6 ya mwaka
2018 sheria ya Zanzibar, iliyopitishwa na baraza la wawakilishi.
Kesi hiyo rasmi,
imeghairishwa Febuari, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena mahakamani hapo na
watuhumiwa wamerejeshwa rumande.
MWISHO
Comments
Post a Comment