Skip to main content

SHEHA FATMA WA KENDWA, AIDHIHIRISHIA DUNIA WANAWAKE WANAPOPATA UONGOZI.....

 


NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@

"UONGOZI sio cheo, ni matendo na matokeo yanayobadilisha maisha ya watu" ni maneno ya wananchi wa shehia ya Kendwa wilaya ya Mkoani.

Wanasema sheha wao ni mwanamke aliyethibitisha kuwa, uongozi wa mwanamke una nguvu ya kubadilisha kabisa muelekeo wa jamii.

Wanakendwa ni kama wanaungana na Mkataba wa umoja wa Mataifa wa kutokomeza aina zote za udhalilishaji (CEDAW) wa 1979 hasa ibara ya 7.

Ibara inayozitaka “Nchi wanachama zihakikishe zinawapa wanawake fursa za kushiriki katika uongozi’’.

Aidha lengo namba 5.5 la maendeleo endelevu ‘SDGs’ ya mwaka 2015 hadi 2030, lililozitaka nchi zote kuhakikisha ushiriki kamili wa wanawake na fursa sawa za uongozi katika ngazi zote, iwe kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Pia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara yake ya 21 (1) inayoeleza kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia Wawakilishi waliochaguliwa kwa hiari.

Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 (ambayo ilihuishwa na kuzinduliwa rasmi kama Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya Mwaka 2023) inahimiza ushiriki wa wanawake katika nafasi mbali mbali za uongozi.

Fursa hii imefika katika shehia ya Kendwa iliopo wilaya ya Mkoa wa kusini Pemba.

Kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Pemba, hupo pia watu wake ni wakarimu, wenye  umoja na mshikamano.

Nyuma ya taswira hiyo, jamii ya wakaazi wa eneo hilo, inasena kwa miaka mingi ilikabiliwa na changamoto nzito za kimaendeleo.

Ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma za afya za karibu, miundombinu duni ya elimu, maji safi na salama, na barabara zisizopitika kwa urahisi.

Shida hizi zilidumu kwa miaka mingi, hadi ilipofika  mwaka 2021, mwaka ambao Fatma Othman Pandu aliteuliwa kuwa sheha wa Shehia hiyo.

“Uteuzi wake haukuwa tu wa kujaza nafasi ya kiutawala, bali ulikuwa mwanzo wa zama mpya za maendeleo jumuishi kwa wanakendwa,” maneno ya Asha Khamis mkaazi wa Kendwa.

Anasema kwa kutumia mchanganyiko wa ujasiri, ushawishi, na ushirikishaji wa jamii, sheha wake, amethibitisha kuwa, uongozi wa mwanamke ni nguzo imara ya mabadiliko ya kijamii.

Mohamed Haji Mohamed, anasema ukitaka kujua kuwa wanawake wanaweza kuongoza, utembelee shehia yao na hilo litadhirika kwa vitendo.

Maryam Haji Omar, anasema wao ndani ya shehia hiyo, damhawana tena shida ya huduma za afya na hasa za mama na mtoto.



‘’Hatusemi kuwa alitoa fedha zake mfukoni, lakini kero zake kwa serikali kuu, tunajivunia uongozi wake, maana hata miundombinu ya elimu imeirika,’’anasema.

YEYE NI NANI HASA?

Jina lake ni Fatma Othman Pandu, mzaliwa wa Kendwa wilaya ya Mkoani kusini Pemba.

Aliepata elimu yake ya msingi, skuli ya Kangani kuanzia mwaka 1980 hadi 1987, alipomaliza darasa la nane,  na kujiunga skuli ya elimu ya sekondari skuli ya Kendwa 1988 hadi alipomaliza kidato cha tatu mwaka 1990.

Kwa vile alikua ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi, mwenyewe anasema baada ya kumaliza masomo yake, alijiingiza katika harakati za kukitumikia chama.

Alikitumikia chama kama mwana chama wa kawaida, hadi mwaka 1994, ambapo aligombea ukatibu wa umoja wa wanawake ‘UWT’ wa tawi la Kendwa, na  kupata nafasi hiyo, kwa idadi kubwa ya kura.

“Nilianza kua kiongozi nipomaliza skuli kwa kushika nafasi kama uongozi wa darasa, Naibu waziri wa mazingira, na nilipomaliza kusoma,  nilipoanza harakati za kukitumikia chama hadi  1994 nikachaguliwa kua Katibu wa UWT jimbo la Kendwa,”anaeleza.



Anahadithia nafasi hio aliitumikia hadi mwaka 2021, ambapo aliteuliwa kuwa sheha wa Kendawa, ingawa kabla ya kushika nafasi hiyo, alikua msaidizi wa sheha.

Katika hili, mtoto wake Fatma aitwae Othman Ali anasema hata kabla ya kua sheha, mama yake alikua ni mwenye kujitolea na kuitumikia jamii kwa moyo mmoja.

Hilo liliwafanya familia na wanakendwa kumuamini, kumkubali na kumshirikisha katika masuala mbalimbali ya  kimaendeleo.

Kwa miaka sita sasa, Fatma ni sheha, na mwanamke wa pili kushika nafasi hiyo katika historia ya shehia yao, baada ya mtangulizi wake Sabiha Mohamed Ali.

Na ni mmoja kati ya masheha 36 wa wilaya ya Mkoani,  yenye masheha wanawake 13 na wanaume 23.

Ilioiwacha nyuma wilaya ya Chake chake yenye masheha wanawake nane na wanaume 24 kati ya masheha 32.

Idadi inayofanya Mkoa wa Kusini Pemba kua na masheha 68, wakiwemo wanaume 47 na wanawake 21, takwimu zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid.

Mwenyewe anasema, haikua rahisi kwake kukubali kama yeye ni kiongozi, baada ya kupewa nafasi hiyo, kutokana na kukosa mafunzo ya kutosha, juu ya uongozi, huku  hofu yake ikiwa atawezaje kuisimamia jamii yote.

“…..ahhh, haikua rahisi kwakukukubali kwamba ningeweza kuongoza na kuiletea jamii yangu maendeleo, sikua naamini juu ya uwezo wangu, ingawa walionizunguka waliniamini”. anaeleza.

Kwa sasa yeye ni hazina na tunu ya wanakendwa, kwani   kwa juhudi zake na mashirikiano na wananchi ameizawadia Kendwa mambo mbali mbali ya kimaendeleo.

AMEIFANYIA NINI KENDWA

Wananchi wa shehia ya Kendwa wanasema, awali walipata tabu kupata huduma za afya, hasa kwa wajawazito na watoto.



Mmoja wa wananchi hao Rehema Ussi Juma anaeleza, walilazimika kwenda Hospitali ya Abdaulla Mzee Mkoani,  kufuata huduma za msingi za mama na mtoto, wakati wa kujifungua,  hii  ilihatarisha maisha ya wengi wakati wa dharura.

Anaeleza kipindi ambacho Fatma amekua sheha, hilo lilikua kipaumbele cha kwanza, kwani alifanya juhudi za kuomba ujenzi wa kutuo kipya cha afya.

Hadi pale viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania ‘TASAF’ walipowapa fursa ya kuchagua mradi wa maendeleo, na kuchagua ujenzi wa kituo cha afya.

“Juhudi za sheha hazikuishia hapo, sisi nayeye tulishirikiana kushika pauro, sururu na jembe kuchimba misingi na kukoroga zege na saruji, hadi kituo cha afya kiloposimama na sasa tunapata huduma nzuri,’’anaeleza.

Na leo hii kinamama wa Kendwa, wanajifungulia katika mazingira salama na yenye staha, jambo linalowapa faraja.

Wanaendelea kusema, miundombinu ya skuli  katika shehia hiyo kwa sasa ni yenye ubora, tofauti na zamani, ambapo ilikuwa finyu na yenye uchakavu mkubwa.

Mwananchi Saleh Mussa Alawi anasema, kwenye hili pia  Sheha Fatma alijitahidi kufuatilia na kuiomba serikali ujenzi na ukarabati wa skuli, ili kuondoa changamoto zilizokuwepo.

“Kwasasa Kendwa, kuna skuli maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa mchepuo wa sayansi na kilimo, yenye miundombinu yote muhimu ya kufundishia, na kujifunzia, watoto wetu wanasomea maabara ya Kompyuta na majengo yenye hadhi,” anaeleza.

Wananchi wanasema sheha wao pia, alianzisha mikutano ya mara kwa mara na wazazi na walezi, ili kusisitiza umuhimu wa elimu, hasa kwa mtoto wa kike, hatua iliyopunguza viwango vya wanafunzi kuacha masomo.



Si hayo tu, Juma Mohamed Said wa Kendwa anasema, katika sekta ya huduma ya maji safi na salama, sheha wao  hakukaa ndio maana, alipoona uwepo wa changamoto hiyo.

Alifanya juhudi za kumfikia Mbungea na Mwakilishi, nao kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Zanzibar ‘ZAWA’ wakajenga visima viwili, vyenye uwezo mkubwa wa kusambaza maji, katika vitongoji vyote vya shehia hiyo na sasa changamoto hiyo imebaki stori tu.

Kendwa ni eneo lenye shughuli nyingi za kiuchumi, ikiwemo biashara na kilimo, na  wakaazi wake husafirisha bidhaa na mazao ya kilimo, kila siku.

Maryam Hassan Salim wa Kendwa anasema miundombinu ya barabara za ndani kwa miaka mingi iliopita ilikuwa katika hali duni.

Anaeleza wakati wa mvua, barabara hizo zilijaa tope na maji, na kufanya usafiri kuwa wa shida kwa wakaazi wake.

Anahadithia, barabara ya mwanzo ya ndani kujengwa Kendwa ilikua sheha Fatma aliomba msaada wa kifusi kilichomwagwa na baadae, serikali kuu sasa imeshaijenga kwa lami.

Sheha huyo, amefanikiwa kushajihisha wananchi kuunda vikundi vya ujasiriamali, vinavyojishughulisha na kazi mbalimbali, ambavyovimefanikiwa kupiga hatua za kimaeneleo.

NJE NA USHEHA

Fatma Othman Pandu ni mke na mama wa watoto sita, anaetimiza majukumu yake ya kuilea familia, bila kuathiri upande wowote.

Ni mkulima na mfugaji anaeamini kwamba “mtaji wa masikini ni nguvu zake” wenye maana kwamba kujituma ni njia pekee ya kupata ukitakacho.

Ni msuluhishi mzuri wa migogoro ya kifamilia, “Napenda sana kua mpatanishi, na jamii yangu inanitumia vizuri kwenye hili.

Anawasihi wanawake wawajibike kutendea kazi nafasi na nyadhifa wanazopata, ili kuondoa dhana za kwamba mwanamke hawezi.

Ali Omar ni muume wa sheha huyo, anasema imani yake ni kwamba, mwanamke anahaki ya kua kiongaozi, na ni mwenye uwezo mkubwa kwenye hili.

Anaihakikishia jamii, kumpa moyo na ushauri wenye kujenga kila siku, ili azidi kua imara na mwenye mafanikio katika nyadhifa hio.

Anaeleza kiu yake ni kuona watoto wake hasa wa kike, hawako nyuma katika uongozi, jambo analoanza kulijenga hivi sasa.

MITANDAO YA KIJAMII

Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii uwakilishi wa wanawake katika uongozi wa ngazi za chini ni mdogo  ikilinganishwa na ngazi za juu za kitaifa.

Takwimu za kimtandao zinaonyesha  ni wastani wa asilimia 2.1 katika ngazi za vijiji.

Huku ikisisitza mitazamo ya Jamii na imani potofu za kijinsia kuhusu uwezo wa wanawake kuongoza katika ngazi za misingi ya jamii ndio sababu ya hali hio.

                                MWISHO

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...