Skip to main content

USAFI LIFANYWE JUKUMU LA WOTE, MASHEHA WATOA RAI

 


NA ZUHURA JABIR, ZNAIBAR

“Usafi ni nusu ya afya."

Haya sio msemo wa utani, bali ni ukweli unaogusa maisha ya kila siku ya wananchi.

Mazingira safi yanamaanisha afya bora, heshima ya makazi na maendeleo ya jamii, lakini pale ambapo mifumo ya usimamizi haieleweki, wananchi hubeba mzigo ambao haukupaswa.

Majadiliano yaliyowakutanisha masheha, wahamasishaji wa jamii na wataalamu wa Baraza la Manispaa Mjini, yameonesha wazi kuwa changamoto za usafi wa mazingira bado zinahitaji mshikamano.

Methali isemayo, "Kidole kimoja hakivunji chawa," inaakisi hali halisi ya mapambano dhidi ya uchafu wa mazingira.

MGONGANO WA MAMLAKA KATIKA UKUSANYAJI WA TAKA

Moja ya hoja zilizojitokeza kwa uzito mkubwa ni mgongano wa mamlaka katika ukusanyaji wa taka ndani ya shehia ya Mchangani.

Kwa mujibu wa sheha Nassir Mohammed Ali, wananchi wanakabiliwa na hali ya kuchanganyikiwa, kutokana na taasisi mbili, Baraza la Manispaa Mjini na Mamlaka ya Mji Mkongwe, kufanya kazi katika eneo moja huku kila moja ikikusanya malipo yake.

 

Wananchi wanajiuliza kwa haki kabisa, wamlipie nani, wakati taasisi moja inadai malipo ya kiwango fulani kwa mwezi, taasisi nyingine nayo inawafuata wananchi haohao kwa madai mengine.

‘’Mwisho wa siku, mzigo unabaki kwa mwananchi, ambao ni wanyonge na wenye kipato cha chini,’’anasema.

 

Anasema hali hiyo, imeongeza malalamiko na kupunguza imani ya wananchi, katika mfumo wa utoaji wa huduma.

Kilichosisitizwa zaidi ni umuhimu wa taasisi hizo kukaa pamoja, kuweka mipaka ya kiutendaji na kuzungumza kwa sauti moja, ili kuondoa mkanganyiko unaowakabili wananchi.

 

Sheria ya Serikali za Mitaa pamoja na misingi ya utawala bora, inasisitiza ushirikishwaji wa wananchi na viongozi wa maeneo husika, katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao.

Ushirikishwaji hujenga uwazi, huondoa migogoro na kuongeza uwajibikaji.



Maamuzi yasiyoshirikisha wadau mara nyingi huishia kuzalisha migogoro na mifarakano ndani ya jamii.

Mshiriki wa kikao hichon Ali Khami Mtumweni anasema licha ya vijana kupita nyumba kwa nyumba kukusanya taka, bado wananchi hawajui wanafanya kazi chini ya taasisi ipi.

Anaeleza kuwa, wakati mwingine vijana hao husema wameitwa na Manispaa, wakati mwingine wameitwa na Mji Mkongwe, anaona hilo sio sahihi.

VIZIMBA VYA KISASA VYA TAKA NI HATUA NZURI

Suala la ujenzi wa vizimba vya kisasa vya kuhifadhi taka lilizungumzwa kwa kina, kwenye majadiliano hayo.

Masheha walikubaliana kuwa, maeneo mengi ya Mji Mkongwe, hayana nafasi ya kutosha kutokana na msongamano mkubwa wa nyumba.

Wanasema washiriki wa majadiliano hayo kuwa, kwa upande mwingine, maeneo ya Mwembeladu na sehemu nyingine za pembezoni, bado yana nafasi zinazoweza kutumika.

Hii inaonesha kuwa suluhisho moja haliwezi kutumika kila mahali. Kila eneo linahitaji mpango unaozingatia hali yake ya kijiografia.

 

MAPENDEKEZO YA MAGARI MADOGO YA UKUSANYAJI TAKA

Miongoni mwa mapendekezo yaliyopokelewa vizuri ni matumizi ya magari madogo yanayopita usiku au alfajiri kukusanya taka moja kwa moja kutoka kwa wananchi.

Magari hayo yanaweza kutumia vipaza sauti kuwatangazia wananchi kutoa taka kwa wakati maalumu.

 

Mfumo huu unapunguza muda ambao taka hukaa mbele ya nyumba na kupunguza uwezekano wa kusambaza harufu mbaya pamoja na magonjwa. Ni mfano wa ubunifu unaoweza kusaidia hasa maeneo yenye msongamano mkubwa.

 

MITARO YA MAJI MACHAFU BADO NI CHANGAMOTO

Mbali na taka ngumu, changamoto nyingine kubwa ni mifereji ya maji machafu.

Baadhi ya mifereji husafishwa na mingine huachwa kwa muda mrefu hadi kufunikwa na magugu pamoja na uchafu unaosukumwa wakati wa mvua.

 

Kutokana na hali hiyo, maji hushindwa kupita vizuri na kuongeza hatari ya mafuriko pamoja na kuzaliana kwa wadudu wanaosababisha magonjwa.  Mazingira haya yanahitaji usimamizi endelevu badala ya kusubiri hadi pale kunapotokea dharura.

 

UHAMASISHAJI WA JAMII UMEANZA KULETA MABADILIKO

Fatma Khamis Ali, mhamasishaji wa jamii kupitia mradi unaotekelezwa na TAMWA, ZAFELA, JUWAUZA na PEGAO, alieleza namna wananchi walivyoanza kushiriki kutatua changamoto zinazowazunguka.  Kupitia kamati za wananchi, baadhi ya kero zimeanza kupatiwa ufumbuzi bila kusubiri maamuzi kutoka ngazi za juu pekee.

 

Katika Shehia ya Kikwajuni, suala la usafi wa mazingira lilifuatiliwa kwa kushirikiana na Manispaa.  Katika Shehia ya Kwahani, tatizo la maji yaliyokuwa yanatiririka kutoka kwenye nyumba mpya lilifuatiliwa na kupatiwa suluhisho kupitia ushirikiano kati ya wananchi, sheha na Shirika la Nyumba.

 

Aidha, kampeni dhidi ya utoro wa wanafunzi zimeonesha mafanikio kwa kupunguza idadi ya watoto wanaokosa kuhudhuria masomo.  Hii ni ishara kuwa pale wananchi wanapopewa nafasi ya kushiriki, maendeleo yanakuwa ya kudumu.

 

WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU WANAONGEZA USHIRIKI WAO KATIKA UONGOZI

Mradi huo pia umeongeza mwamko kwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi.

Wanawake wengi wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa badala ya kusubiri uteuzi wa viti maalumu.

 

Hatua hii inaendana na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambazo zinatambua haki ya usawa, ushiriki wa wananchi na kutobaguliwa katika masuala ya uongozi na maendeleo. 

Aidha, inaendana pia na malengo ya usawa wa kijinsia yaliyoainishwa katika Dira ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.

 

MTARO WA KWAALINATU BADO UNAHITAJI NGUVU ZA PAMOJA

Sheha wa Kwaalinatu, Salum Shabaan Mzee, alieleza kuwa pamoja na jitihada za wananchi kusafisha mtaro mara kwa mara, bado changamoto hiyo ni kubwa.  Alibainisha kuwa ukosefu wa vifaa vya kazi unafanya juhudi za wananchi kuwa ngumu zaidi.

Hii inaonesha kuwa ushiriki wa wananchi pekee hautoshi bila kuwepo msaada wa taasisi zinazohusika.

 

MAAJAA YALIYO KARIBU NA MAKAZI NI KERO YA MUDA MREFU

Mhamasishaji Ismail Khamis Akhui alieleza kuwa katika maeneo ya Kwahani, Jang'ombe na Kikwajuni wananchi bado wanaishi karibu sana na maeneo ya kutupa taka.

Hali hiyo inaleta wasiwasi wa kiafya hasa kwa watoto pamoja na familia zinazozunguka maeneo hayo.  Wananchi wanahitaji kuona maboresho yanayoonekana kwa macho badala ya kuendelea kuishi karibu na taka kwa miaka mingi.

 

MPANGO WA MANISPAA KUHUSU VIZIMBA VYA KISASA

Afisa Mazingira wa Baraza la Manispaa Mjini, Ikrima Jumanne Khamis, alifafanua kuwa mwaka 2018 Manispaa ilipata ufadhili kutoka Benki ya Dunia uliowezesha kujengwa vituo 73 vya taka.

Baadhi ya vituo hivyo viliondolewa kutokana na kupisha miradi ya maendeleo au kukosa sifa za kuendelea kuwepo karibu na makazi ya watu.

 

Kwa sasa, kupitia mradi wa BIG-Z, unaotekelezwa kwa kushirikiana na kampuni husika, Manispaa inaendelea kujenga vizimba vya kisasa vitakavyoficha taka na kupunguza uchafu unaoonekana wazi.  Lengo ni kuboresha usimamizi wa taka huku ikipunguza athari kwa afya ya jamii.

Hata hivyo, Manispaa imeeleza kuwa bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa magari ya kutosha kwa ajili ya kukusanya taka moja kwa moja kutoka kwenye nyumba za wananchi.

 

SHERIA ZINASEMA NINI?

Masuala ya usimamizi wa taka na afya ya mazingira yanatambuliwa katika Sheria ya Afya ya Jamii ya Zanzibar, Na. 11 ya mwaka 2023, ambayo inaweka wajibu wa kulinda afya ya jamii kwa kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.

Pia, Sheria ya Serikali za Mitaa ya Zanzibar, Na. 7 ya mwaka 2014, inazipa mamlaka serikali za mitaa kusimamia usafi wa mazingira, ukusanyaji wa taka na utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia uwazi na ushirikishwaji.

Kwa upande wa mazingira, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Zanzibar, Na. 3 ya mwaka 2015, inasisitiza wajibu wa taasisi na wananchi kushirikiana kulinda mazingira na kuzuia uchafuzi unaoweza kuhatarisha afya za watu.

Sheria hizi zinatoa msingi wa kuhakikisha kila taasisi inawajibika ndani ya mipaka yake na wananchi wanapata huduma bora bila kubebeshwa migongano ya kiutawala.

 

MWISHO

Kauli za masheha, wahamasishaji wa jamii na wataalamu zimeonesha jambo moja muhimu: changamoto nyingi hazikosekani kwa sababu ya ukosefu wa nia, bali mara nyingi husababishwa na ukosefu wa uratibu.  Wananchi wanahitaji huduma iliyo wazi, inayotabirika na isiyowalazimisha kulipa mara mbili kwa huduma moja.

 

Pale taasisi zinaposhirikiana, viongozi wanaposhirikisha wananchi na jamii inapopewa nafasi ya kushiriki katika maamuzi, hata changamoto kubwa hupata ufumbuzi.  Kama isemavyo methali ya Kiswahili, "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu." Huu ndio msingi wa kujenga miji safi, afya bora na jamii yenye maendeleo endelevu. Usafi wa mazingira si jukumu la taasisi pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja wetu.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...