NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
MWANASHERIA wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Idara Maalum ‘SMZ’ Aziza Suleiman Mohamed amesema, jamii imekuwa ikifahamu
udhalilishaji, unaopelekea madhara ya kimwili, bali unajumuishwa madhara
ya kingono, kihisia, kutelekezwa pamoja na kumnyima mtu usalama wake.
Ameyasema hayo jana
August 3, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa shehia ya Uwandani wilaya
ya Chake chake, juu ya elimu iliyoandaliwa na Mwemvuli wa Asasi za Kiraia Pemba
PACSO na kufanyika skuli ya Uwandani.
Alisema kuwa upo udhalilishaji mbalimbali unaojumuishwa madhara
ya kingono, kihisia, kutelekezwa pamoja na kumnyima mtu usalama wake.
Alisema matokeo ya udhalilishaji ni makubwa
kiasi ambacho, kunaweza kusababisha majaraha, kifo kuenea kwa maradhi tabia
hatarishi na matokeo mabaya kwa wanaofanyiwa.
Alifafanua kuwa wahanga wakubwa wanaothirika na vitendo hivyo ni wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, hivyo ipo sheria ya Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011, imeelza kuwa ni wajibu wa kila mtu kuwahifadhi, kiwalinda ili kuondokana na udhalilishaji.
"Vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikitukosesha raha jamii yetu, hivyo ni vyema tukashirikiana kwa pamoja, kupambana ili tupate kizazi kilichobora na salama,"alifafanua.
Aidha lieleza kuwa, endapo mtu atafanyiwa udhalilishaji,
anatakiwa apate matibabu bila kubaguliwa na amewataka wananchi hao kuwafichua
wahalifu wanaofanya vitendo hivyo.
Nae Msaidiz wa sheria kutoka Jumuiya ya
wasaidizi wa sheria wilaya ya Chakechake ‘CHAPO’ Asha Faki Juma alisema kuwa,
ipo Sheria ya mwaka 2018 ya msaada wakisheria, inayotoa mfumo wa upatikanaji wa
haki, kwa wale ambao hawana uwezo wa kujisimamia kesi zao.
Alisema kuwam wasaidizi sheria, wamekuwa wakitoa elimu, ushauri na msaada kwa jamii bila ya malipo, iwe ni kuhusu migogo ya ardhi, udhalilishaji talaka na ndoa.
"Tupo wasaidizi wa sheria katika shehia zote za Unguja na Pemba, kwa lengo la kuwasaidia wananchi, ambao hawawezi kujisimamia kesi zao na hawana uwezo, wa kulipa mawakili wa kujitegemea,’’alifafanua.
Mapema Mkurugrnzi wa ‘PACSO’ Alhajji: Mohamed Najim alisema kuwa,
wamekuwa wakishirikiana na waratibu, katika shughuli mbalimbali, ili
kuwawezesha wananchi, uelewa na masuala ya jamii.
Alisema, umoja wa jumuiya zisizo za kiserikali za Pemba
‘PACSO’ ni mtandao uliosajiliwa rasmi mwaka 1995 na umekuwa na mchango mkubwa
katika kuimarisha maendeleleo endelevu, ya jamii kisiwani humo.
‘’Lazima kwa hili, niendelee kuwapongeza wafadhili wetu wa UNDP, maana
wamekuwa wakituwezesha kuzizunguruka shehia za Pemba, ili kuwafundisha wananchi,
haki na wajibu wao kisheria,’’alifafanua.
Kwa upande wake sheha wa Uwandani
Ali Mussa Bakari, ameishukuru PACSO, kwa
uhamasishaji na utoaji wa elimu na aliwaomba kuwa na muendelezo wa shughuli
kama hiyo.
Nae mwananchi wa Uwandani Khamis Rashid alisema kuwa, kupitia elimu hiyo watakuwa balozi mzurim kuhusiana na vitendo hivyo kwa kutoa ushirikiano na kutovifumbia macho.
PACSO kwa sasa iko ukingoni kumalizia mradi wa Uwezeshaji wa Kisheri na Upatikanaji
wa Haki, ambao ulianzia mwaka 2022, na ukitarajiwa kumalizika Disemba mwaka
huu, ambao ukifadhiliwa UNDP.
MWISHO.
Comments
Post a Comment