Skip to main content

JUMAZA INAUNGA MKONO MARIDHIANO VYAMA VYA SIASA ZANZIBAR

 


NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@
JUMUIYA ya Maimamu Zanzibar   (JUMAZA) imesema inaunga mkono tamko la maridhiano ya chama cha CCM na ACT Wazalendo kwani ni hatua  ya msingi katika kuimarisha amani, umoja na maendeleo ya Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Shekh Ali Abdalla Amour, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jamatkhan Vuga mjini Unguja.

Alisema jumuiya hiyo imepokea kwa faraja na furaha maridhiano yaliyotangazwa hadharani Julai 9, katika viwanja vya Ikulu 
Zanzibar mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Aidha alisema ni vyema kwa  viongozi hao kutofanya khiyana katika utekelezaji wa makubaliano hayo ili kuendelea kujenga amani, umoja  na mshikamano kwa wananchi wa Zanzibar.

Alieleza kuwa jambo hilo limeonesha utayari wa viongozi kuweka mbele maslahi ya Zanzibar na wananchi wake badala ya tofauti za kisiasa.

Alisema mafanikio ya maridhiano  hayo yatategemea uaminifu, dhamira ya kweli na utekelezaji wa makubaliano kwa ikhlasi hivyo viongozi wote wana wajibu wa kutekeleza ahadi walizoweka mbele ya wananchi na mbele ya Mwenyezi Mungu.

Sambamba na hayo aliwapongeza viongozi wastaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Dk. Amani Abeid  Karume na Juma Duni Haji kwa mchango wao katika kusimamia maridhiano katika awamu ya uongozi iliyopita.

" Viongozi wetu wameonyesha ukomavu wa kisiasa uliowezesha kufikiwa kwa makubaliano tunayoyaona sasa" alisema.

Nae, Naibu Amiri JUMAZA Taifa, Shekh Mohammed Haji Omar, alisema nia ya dhati inapokuwepo mambo yanafanikiwa 
kwa asilimia kubwa na anaamini  matumaini yake jambo hilo litakwenda vizuri.

Alifahamisha kuwa kuna na  manufaa makubwa kutokana na historia kwani serikali ya awamu ya nane ina maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii katika sekta mbalimbali.

“Jambo moja lilobaki ni hili la wananchi kuwa pamoja kimaadili,kisiasa na kimaendeleo hivyo tuna imani kubwa mambo yatakuwa mazuri kutokana na serikali ilivyoonesha maendeleo makubwa,” alisema.

Katibu wa Bodi ya Wadhamini JUMAZA, Masoud Hemed Nassor, alisema JUMAZA ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali wakati wowote itakapohitajika  ili kuhakikisha maridhiano hayo yanadumu na kuzaa matunda yenye manufaa kwa Zanzibar na wananchi wake.

Baadhi ya wananchi wa  Zanzibar walisema wanauunga mkono mchakato wa maridhiano hayo kwani suluhu na maelewano ni sehemu ya mafundisho ya dini ya kiislamu na ndio njia bora ya kulinda amani, mshikamano na maendeleo ya taifa.
MWISHO

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...