Skip to main content

Posts

WIZARA YA AFYA KUIMARISHA UTOAJI HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU

NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ WIZARA ya Afya Pemba imesema, itaendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma na upatikanaji wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu, kama sheria zinavyo elekeza. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Afisa mdhamini wa wizara hiyo Pemba Khamis Bilali Ali alisema, ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora kama ilivyo kwa wengine, wizara i ta hakikisha hospitali zinawekwa njia za kupitia watu wenye ulemavu (Ramp) ili kupita kwa urahisi  pale wanapofika kufuata huduma. Alisema jambo jengine linalotekelezwa ni kutoa maelekezo kwa watoa huduma za afya kuhakikisha wanatoa kipaombele kwa watu wenye ulemavu wanapofika hospitalini, kama kanuni zinavyo eleza ili kuhakikisha watu hao wanapata haki yao ya msingi ya afya bila ya usumbufu. “Tumeweka (Ramp) pia kuna kanuni zinazo wataka watoa huduma kutoa kipaombele kwa wenye ulemavu na wizara inasimamia kwakaribu suala hili na linafanyika”, alieleza. Alisema ingawa kuna changamoto ya wakalimani ...

WATU WENYE ULEMAVU NA USHIRIKI WA MICHEZO, BADO KIZUNGUMKUTI, WIZARA YAJITUTUMUA

  NA SAID ALI, PEMBA@@@@ ‘’WATU wenye ulemavu wanastahiki haki zote za msingi za binaadamu, sawa na watu wingine, ikiwemo michezo na burudani,’’inaeleza sheria yao. Sheria hiyo nambari 8 ya mwaka 2022, ikazidi kufafanua kwenye kifungu cha 28 (1) (f), kwamba kundi hilo linastahiki haki zote za msingi, bila ya ubaguzi.   Tena uzuri zaidi kifungu cha 29 (1), kikamtamka kuwa, Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu, katika kuiendea haki hiyo, litahakikisha ufikiaji wa maeneo hayo. Kikafafanua kuwa, lazima pawepo na miundombinu rafiki ya kuyafikia majengo ama maeneo kwa watu wenye ulemevu, wanapoziendea haki zao michezo na burudani. Kifungu cha 30, kikasisitiza kuwa, kila mmoja anawajibu wa kutekeleza, kulinda na kutetea haki za watu wenye ulemavu, kwa kutoa taarifa za uvujifu wa haki hizo. Eneo jingine sera ya maendeleo ya taifa ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004, Ibara yake 3.15 ikazitaka nchi, kuhakikisha wanawekewa utaratibu utakaohakikisha watu wenye ulemavu, wanash...

'THBUB' WAPIGWA MSASA MIFUMO UTENDAJI KAZI

  NA MWASHAMBA JUMA, THBUB@@@@ NAIBU Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Juma Msafiri Karibona amepongeza juhudi za watumishi wa tume hiyo kujengeana uwezo na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Karibona aliyasema hayo alipofungua mafunzo ya Mifumo ya Utendaji kazi kwa tume hiyo ya kujengeana uwezo baina ya watumishi wa tume hiyo yaliyofanyika ofisini kwao Mombasa, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Novemba 19, 2025. Aidha, alisifu hatua ya watumishi hao kujijengea uthubutu na kujiongezea uelewa mpana hasa katika kufuatilia na kuyafanyia kazi matumizi ya mifumo katika utendaji kazi wao za kila siku ili kuendana sambamba na mabadiliko ya teknolojia. Akiuzungumzia mfumo wa Utumishi wa utendaji wa “ESS” moduli ya “PEPMIS” Naibu Karibona aliwahimiza watumishi hao kuendelea kuufanyia kazi mfumo huo kwa wakati ili kuendana sambamba na majukumu yao ya kila siku huku akiwatanabahisha watumishi hao ku...

HUDUMA ZA AFYA KWA WATU WENYE ULEMAVU SIO NGUMU WALA LAINI

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA DUNIA inapaswa ielewe kuwa, watu wenye ulemavu ni sawa na watu   wingine katika jamii. Wana haki ya kunufaika na kupata haki zote za msingi ikiwemo ya afya. Haki ya afya kwa watu wenye ulemavu imetamkwa na kuelezwa kwenye sera na sheria za kimataifa, kikanda na kitaifa. Hapa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za watu wenye ulemavu wa mwaka 2006, ibara ya 25, imesisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kupata huduma za afya bila ubaguzi. Huku Sheria ya Watu wenye Ulemavu ya Zanzibar nambari 8 ya mwaka 2022 nayo kwenye kifungu cha 28, kikisisitiza watu wenye ulemavu wanastahiki kupata haki zote za msingi ikiwemo ya afya. “Watu wenye ulemavu wanastahiki kupata huduma za afya kama matibabu, matengenezo na marekebisho yanayohusiana na ulemavu,” kinafafanua kifungu hicho. Hii inaonyesha, jinsi gani ulimwengu umewazingatia   watu wenye ulemavu katika upatikanaji wa haki zote za msingi ambao ndio haki za kibinaadamu. Kwani watu wenye ulemavu n...

WEMA YAWAANDAA WATOTO WA KIKE KUWA VIONGOZI BORA WA BAADAE

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@    'DUNIA imebadilika...kwani ya jana sio ya leo'   Katika miaka ya sasa, wanaonekana wanawake wengi wanaojihusisha na masuala ya uongozi, katika sekta mbali mbali.   Ikiwa ni katika vikundi vya ushirika, uongozi kwenye jamii, shehia, majimbo na hata kwenye taasisi za umma na binafsi.   Hii ni kutokana na elimu inayotolewa kupitia vyombo vya habari na kwenye jamii, kuhusu ushirikishwaji wa wanawake kwenye masuala ya uongozi.   Na ndio maana hata mfumo wa elimu uliopo sasa, unatambua kwamba watoto wa kike wanapaswa kujengwa mapema kiongozi, ili kila hatua anayopitia aweze kujiamini na kuwa jasiri.   Tangu wakiwa skuli, wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuwa viongozi bora na huwashirikisha wakike na kiume bila ubaguzi, lengo ni kutengeneza taifa lenye viongozi bora wa baadae.   Mwanafunzi Aisha Khamis Ayoub ambae ni Waziri wa Fedha skuli ya sekondari ya Idrissa Abdulwakil Kizimbani Wete ana...

BARAZA LIJALO LA MAWAZIRI WANAHARAKATI WATAMANI 50 KWA 50 IANZIE HAPO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@ NOVEMBA 1, mwaka huu Rais mteule wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, alikula kiapo cha uaminifu cha kushika madaraka ya urais kwa awamu ya pili. Sherehe hizo zilifanyika uwanja wa New Amani Complex, kuanzia majira ya saa 12: 00 asubuhi, huku umati wa wananchi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, wakijitokeza. Sherehe hizo, ni ishara ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, uliopigwa Oktoba 29, mwaka huu na wazanzibari laki 448, 832 kumpa kura za ushindi, ambayo ni sawa na asilimia 74.8. Kisha, Rais huyo wa Zanzibar, alimteua Mwanasheria mkuu wa Zanzibar Mwinyi Talib Haji, hapo ni sawa na kusema, anaanza kupanga safu yake ya awamu ya pili. Pamoja na kumtea Makamu wa Pili wa rais akiwa ndie mtendaji mkuu wa serikali, bila shaka sasa zamu ya baraza la mawaziri linafuata. WANAHARAKATI WANASEMAJE Dk. Mzuri Issa Ali, ambae ni Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar, anampa heko Dk...