NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@
WIZARA ya Afya Pemba
imesema, itaendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma na upatikanaji
wa huduma za afya kwa watu wenye ulemavu, kama sheria zinavyo elekeza.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Afisa mdhamini wa wizara hiyo
Pemba Khamis Bilali Ali alisema,
ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora kama ilivyo kwa wengine, wizara itahakikisha hospitali zinawekwa njia za kupitia watu wenye ulemavu
(Ramp) ili kupita kwa urahisi pale wanapofika kufuata huduma.
Alisema jambo jengine linalotekelezwa ni kutoa maelekezo kwa watoa huduma za afya kuhakikisha wanatoa kipaombele kwa watu wenye ulemavu wanapofika hospitalini,
kama kanuni zinavyo eleza ili kuhakikisha watu hao wanapata haki yao ya msingi ya afya bila ya usumbufu.
“Tumeweka (Ramp) pia kuna kanuni zinazo wataka watoa huduma kutoa kipaombele kwa wenye ulemavu na wizara inasimamia kwakaribu suala hili na linafanyika”,
alieleza.
Alisema ingawa kuna changamoto ya wakalimani wa lugha ya alama kwa ajili ya wenye ulemavu wa uziwi hospitalini, wizara huwashauri watu hao kutumia wakalimani wa lugha ya alama waliomo katika jumuiya zao
au watu wao wakaribu, ili kurahisisha mawasiliano na upatikanaji huduma bora.
Aliongeza kua katika kulizingatia hilo watoa huduma huweka umakini mkubwa wa kimawasiliano bainabaina yao na wagonjwa wenye uziwi,
ambao wanaweza kujieleza wenyewe ili kuhakikisha
wanapata huduma stahiki.
“Miundombinu ya utoaji huduma inaridhisha kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali,
lakini bado changamoto ipo kwa wenye ulemavu wa uziwi,
wakalimani hatuna bali tuna shauri wafike hospitali na wakalimani wao au
watu wao wa karibu”, alieleza.
Alifafanua wizara imeona upungufu mkubwa katika eneo hili
la wakalimani wa lugha ya alama hospitalini,
na imeona ipo haja ya kuweka wakalimani hao ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wenye ulemavu wauziwi,
hivyo wanaendelea kuishauri serikali kuu umuhimu wa jambo hili.
Alisema wizara ya afya itaendelea kuweka miundombinu rafiki ya utoaji huduma bora kwa watu wenyeulemavu,
kwani ni haki ya msingi ya kila mmoja kama sheria zinavyo eleza.
Aidha aliwataka watu wenye ulemavu kuendelea kutumia vituo vya afya na hospitali ili kutatua changamoto zao za kiafya na kwamba serikali inawazingatia ipasavyo ili kuhakikisha wananufaika na huduma zote za msingi .
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wamesema kwakiasi kikubwa serikali kupitia wizara ya afya imefanikiwa katika utoaji huduma kwao, na upungufu zaidi unakuwepo kwa wenye ulemavu wa uziwi, hivyo wameiomba serikali kuwazingatia watu hao ili wapate huduma bora kama ilivyo kwa wengine.
Sheria ya
Zanzibar ya watu wenye ulemavu (2022) kifungu cha 28,
kinaeleza kua watu wenye ulemavu wanastahiki kupata haki zote za msingi ikiwemo ya afya.


Comments
Post a Comment