NA
MWASHAMBA JUMA, THBUB@@@@
NAIBU Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bw. Juma
Msafiri Karibona amepongeza juhudi za watumishi wa tume hiyo kujengeana uwezo
na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Karibona aliyasema
hayo alipofungua mafunzo ya Mifumo ya Utendaji kazi kwa tume hiyo ya kujengeana
uwezo baina ya watumishi wa tume hiyo yaliyofanyika ofisini kwao Mombasa,
Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Novemba 19, 2025.
Aidha, alisifu hatua
ya watumishi hao kujijengea uthubutu na kujiongezea uelewa mpana hasa katika
kufuatilia na kuyafanyia kazi matumizi ya mifumo katika utendaji kazi wao za
kila siku ili kuendana sambamba na mabadiliko ya teknolojia.
Akiuzungumzia mfumo
wa Utumishi wa utendaji wa “ESS” moduli ya “PEPMIS” Naibu Karibona aliwahimiza
watumishi hao kuendelea kuufanyia kazi mfumo huo kwa wakati ili kuendana
sambamba na majukumu yao ya kila siku huku akiwatanabahisha watumishi hao
kutokuutumkia kikamilifu ni kwenda kinyume na kanuni za utumishi katika mfumo
huo.
Akizungumza katika
mafunzo hayo Mkufunzi Bw. Abdalla Salum Muhamed ambaye pia ni Afisa TEHAMA wa
tume hiyo, Ofisi ya Zanzibar aliwapitisha watumishi wenziwe katika maeneo manne
ya mifumo wanayoitumia THBUB ukiwemo Mfumo wa Ofisi Mtandao “e-Office”, Mfumo
wa kushughulikia Malalamiko (CMIS), Mfumo wa Utendaji wa kiutumishi, (ESS),
Mfumo wa kuombea vibali vya kusafiria nje ya nchi kwa Watumishi wa Umma
(e-Vibali) na Mfumo wa kufanyia mikutano (e- Mikutano).
Kwa upande wao
watumishi hao walikishukuru kitengo cha ICT cha THBUB eneo la TEHAMA kwa
kuwaandalia mafunzo hayo nakueleza kuwa yamewajengea uwezo kwa kuwaongezea
uelewa mpana kwenye maeneo mengi ambayo baadhi yao yalikua na ukakasi kwa
baadhi ya watumishi hao hasa katika matumizi ya mifumo na tekniolojia ili
kuendana sambamba na wakati uliopo.
Mafunzo hayo ya Mifumo ya Utendaji kazi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, yalitayarishwa na eneo la TEHAMA na yalifungwa rasmi na Afisa utumishi wa tume hiyo, Bw. Fadhili Yussuf Khamis kwa kuwanasihi watumishi hao kuyatumia vyema mafunzo hao kwa ufanisi wa kazi zao za kila siku.
Comments
Post a Comment