Skip to main content

Posts

MAFUNZO YA UTUNZAJI WA MISITU YA MIKOKO YAANZA RASMI COMMUNITY FORESTS PEMBA

  BY MUNIRA KAONEKA, ZANZIBAR@@@@ Katika jitihada za kuimarisha uhifadhi wa mikoko na matumizi endelevu ya rasilimali za asili, Jumuiya ya Community Forests Pemba (CFP) imefungua mafunzo maalum kwa Watoa Mafunzo ya Jamii (ToTs) kuhusu uhifadhi wa mikoko na usimamizi wa rasilimali za jamii. Mafunzo haya, yalifanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Februari katika ofisi za CFP Unguja, na yalilenga kuwawezesha washiriki kuwa viongozi wa uhifadhi wa mazingira katika jamii zao. Mafunzo haya yameandaliwa ili kuongeza uelewa wa washiriki kuhusu umuhimu wa mikoko, mbinu za kuhifadhi misitu, na namna ya kushiriki katika usimamizi wa rasilimali za asili kwa njia endelevu. Kupitia mafunzo haya, ToTs watapata ujuzi wa vitendo na mbinu za kufundisha ambazo zitawawezesha kuwa mabalozi wa mabadiliko katika maeneo yao. Akifungua rasmi mafunzo haya, Mkurugenzi Mtendaji wa CFP alisisitiza kuwa uhifadhi wa mikoko ni jukumu la jamii nzima. “Uhifadhi wa mikoko na urejeshwaji wake ni kazi ya pamoja, na ni...

BAKARI KHAMIS: DEFYING DISABILITY TO LEAD CLIMATE ADAPTATION IN PEMBA

BY, KHELEF NASSOR, ZANZIBAR@@@@ In Kambini Mchangamdogo, a small village on Pemba Island, lives Bakari Khamis Bakari, a man whose resilience and determination overcome great challenges. A devoted father of seven, Bakari has refused to let his physical disability—an impairment in one of his legs—limit his aspirations. Instead, he has become a driving force of inspiration, proving that people with disabilities can be at the forefront of climate adaptation efforts. Bakari’s journey into agroforestry began when he was mobilized and trained by Community Forests Pemba through the Zanzibar Women Leadership in Adaptation (ZanzADAPT) project. The Zanzibar Women Leadership in Adaptation (ZanzADAPT) project, under which Bakari was trained, aims to foster women’s leadership in climate resilience efforts. By equipping women and marginalized groups with knowledge, skills, and resources, the project promotes inclusive solutions to climate change challenges. Despite initial skepticism from the communi...

MBUNGE YAHYA AKABIDHI VIFAA TIBA VYA MAMILIONI HOSPITALI KIVUNGE

NA MWANDISHI WETU, UGUJA@@@@  Zaidi ya shilingi miloni 700  zimetumika katika ununuzi wa vifaa tiba vilivyokabidhiwa huko hospitali ya Kivunge mkoa wa Kaskazini Unguja.   Akikabidhi vifaa hivyo mbunge wa Jimbo la Kijini Yahya Ali khamis alisema vifaa tiba hivyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa huduma za wagonjwa. Ameleza kumekuwa na utekelezaji mkubwa wa miradi lakini kipao  mbele Cha kwanza ni kuelekeza nguvu katika miradi ya hospitali. "Sisi tunajali sana wananchi wetu na ndio maana tukatanguliza vifaa vya afya ambayo ndio msingi wa awali katika maisha yetu wanaadam"alisema Alieleza tayari miradi mingi ya kimkakati katika Jimbo Hilo unaendelea kufanyika kama vialea miradi ya Maji,umeme,na hata Bara Bara Mbunge huyo aliwataka wananchi kuthamini nguvu za viongozi wao kutoka na jitihada wazi zichukua kwa kitafura wafadhili wa maendeleo. Nao wananchi waliohudhuria ghafla hiyo ya makadhiano ya vifaa tiba hospitalini hapo walimpongeza mbunge huyo kwa kutoa msaada huo....

WANAWAKE WANAOWEKA VITU SEHEMU ZA SIRI KUUA MFUMO WA UZAZI

NA ZUHURA JUMA, KU@@@@ WANAWAKE wametakiwa kuacha tabia ya kuweka vitu kwenye sehemu za siri, kwani wanaweza kuathiri mfumo mzima wa viungo vya uzazi. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa chama cha Waandishi Tanzania (TAMWA) Mkanjuni Chake Chake Pemba, Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar alisema, kuna baadhi ya wanawake huweka vitu katika sehemu zao za siri, jambo ambalo ni hatari kwa afya ya uzazi. Alisema kuwa, ni vyema wakawa wanafika hospitalini na vituo vya afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mara kwa mara ili ikiwa wamepata matatizo waweze kupatiwa matibabu na sio kuweka vitu ambavyo vinaweza kuwapatia madhara zaidi. "Kuna baadhi yao huweka vitu kama wanajitibu baada ya kupata magonjwa ya kujamiiana na kuna wengine wanaweka vitu hivyo kwa urembo, haya yote hayafai kwa sababu wanaweza kuathirika katika mfumo wa kizazi," alisema Katibu huyo. Aidha, akielezea kuhusu maambukizi ya magonjwa ya kujamiiana alisema, pia yanasababisha kuathiri kiza...

ZURA YAWATAKA WAANDISHI KUTOA ELIMU MATUMIZI SAHIHI YA UMEME KWA WANANCHI

NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@  KAIMU Mkuu kitengo cha uhusiano  Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar (ZURA)  Shara Chande Omar amesema mamlaka itaendelea kuandaa utaratibu pindi tu inapotokea mabadiliko ya bei  elekezi kwa matumizi za huduma ya maji,  nishati ili Kuwaondoshea usumbufu wananchi.  Ameyasema hayo  akitoa ufafanuzi wa bei mpya ya umeme katika kikao na  wandishi wa habari mbali mbali huko kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi za ZURA Kibirinzi chake chake Pemba Amesema lengo la kikao hicho na wadau wa habari ni  kuwafikishia wananchi tarifa hiyo ya mabadiliko ya bei ya umeme ambayo imeanza kutumika kwa sasa.  " Wandishi wa habari ndio Wenye jukumu la kuwafikishia wananchi tarifa  sahihi pindi tu itapotokea mabadiliko ili kuepuka malalamiko na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya umeme. "alisema kaimu huyo.  Aidha amesema kuwa mamlaka imeanda utaratibu wa kuwasajili mafundi wa umeme kwa kuwapatia vib...

IDARA YA KATIBA: ‘’KUJITOLEA KWA WASAIDIZI WA SHERIA NI TAKWA LA KISHERIA’'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa Divisheni ya Katiba na Sheria Pemba Bakari Omar Ali, amewasisitiza wasaidizi wa sheria, kukumbuka kuwa ,   bado dhana ya kujitolea kwa aina ya kazi yao hiyo, itabakia pale pale licha ya changamoto walizonazo. Alisema, kwa mujibu wa sheria inayowaongoza, ni kosa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria na kisha kuomba malipo kwa m wananchi husika. Mkuu huyo wa Divisheni, aliyasema hayo leo Febuari 09, 2025  ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ wakati akitoa maoni yake, baada ya kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti kwa wasaidizi wa sheria ,   kisiwani humo. Alisema, ijapokuwa sasa wapo wanaodai malipo kama baraka ya kufanyakazi zao, lakini bado sheria haitambuwi uwepo wa posho kama motisha wa kufanya kazi zao. Alieleza kuwa, msingi mkuu wakati wa lipo omba kazi hiyo na sasa ikiingizwa ndani ya sheria yao, ni kufanyakazi kwa njia ya kutolea, na hasa kwa wananchi wanyonge na makundi maa...

WADAU WALIA NA SHERIA TUME YA UTAANGAZAJI ZANZIBAR

  NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ SASA ni miaka 26 tokea kuasisiwa kwa sheria ya Tume ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997, licha ya kujumuisha na marekebisho yake. Sheria hii, imekuja kusimamia, kuangalia mwenendo wa vyombo vya habari Zanzibar hasa redio, televisheni na vile vya kisasa vyenye kurusha maudhui yao mtandaoni. Sheria hii yenye vifungu 30, vilivyobebwa na sehemu sita kuu, inavyovifungu kwa hakika sio rafiki, kuelekea uhuru kamili wa habari hapa Zanzibar. SHERIA KWA UJUMLA Kama ilivyo sheria nyingine zote, kwenye sehemu ya kwanza imeundwa na vifungu vitatu, maana kile cha nne, kimefutwa na kati ya hivyo kimoja kinatoa jina la sheria na maana ya maneno. Kwa mfano,  mtangaazaji ni mtu ambaye amepewa leseni chini ya sheria hii ya kutoa huduma za utangaazaji katika vyombo vya habari. Kwenye sehemu ya pili ya sheria hii, yenyewe imeundwa na vifungu kuanzia cha tano (5) hadi cha 10, na kubwa zaidi lililopo ni pamoja na uanzishwaji wa Tume ya Utangaazaji Zanziba...

T.O.T WAPEWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA TABIANCHI

  Wanawake  wameombwa kuvitumia vyombo vya habari ipasavyo kwa lengo la kutangaza kazi wanazozifanya katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wanawake viongozi  kupitia mradi wa ZanzAdapt Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ Dkt Mzuri Issa Ali amesema wanawake wanafanya mambo mengi katika jamii ila bado mchango wao haujatambulika kama ilivyo kwa wanaume hivyo kuvitumia vyombo vya habari kutawezesha kutambulika na kujitangaza kwa haraka hasa kupitia mitandao ya kijamii. Amesema historia ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla haioneshi mchango ama juhudi za wanawake kwa sababu wanawake bado hawajawa na ujasiri na uthubutu wa kutumia vyombo vya habari kwa usahihi. “Wanawake wanafanya mambo mengi katika jamii na kujitoa zaidi, sasa wakati umefika kueleza changamoto na mambo yanayowahusu kupitia vyombo vya habari ili kupatiwa ufumbuzi,” Dkt Mzuri. Mkufunzi katika mafunzo hayo Sophia Ngalapi amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya ...

KATIBU MKUU ABEDA ASAINI AGENDA YA MASUALA YA WANAWAKE KUHUSU AMANI, USALAMA

  NA MWANDISHI WETU, UNGUJA KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Abeida Rashid Abdallah amesaini Mpango wa Taifa wa kushughulikia Utekelezaji wa Agenda ya masuala ya Wanawake, kuhusu Amani na Usalama ulioandaliwa mahsusi kwa ajili ya kutekeleza Azimio Na:1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hafla ya utiaji saini imefanyika jana ofisini kwake Kinazini Unguja, amesema Mpango huo ni heshima kwa Tanzania kwani imeonesha wazi kukubali na kutekeleza Azimio hilo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha Wanawake wanakua  katika amani na usalama wakati wote. Amefahamisha kwamba Azimio hilo lilipitishwa tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2000, kwa lengo la kuhimiza umuhimu wa nafasi ya wanawake katika kuzuia na kutatua mizozo, mashauriano ya amani, ujenzi wa amani, ulinzi wa amani, hatua za usaidizi wa kibinadamu na ujenzi baada ya mizozo na kusisitiza umuhimu wa ushiriki sawa katika uendelezaji wa amani na usalama duniani. Ameeleza Wizara ya Maendeleo ya Jam...