NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
KAIMU Mkuu kitengo cha uhusiano Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar (ZURA) Shara Chande Omar amesema mamlaka itaendelea kuandaa utaratibu pindi tu inapotokea mabadiliko ya bei elekezi kwa matumizi za huduma ya maji, nishati ili Kuwaondoshea usumbufu wananchi.
Ameyasema hayo akitoa ufafanuzi wa bei mpya ya umeme katika kikao na wandishi wa habari mbali mbali huko kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi za ZURA Kibirinzi chake chake Pemba
Amesema lengo la kikao hicho na wadau wa habari ni kuwafikishia wananchi tarifa hiyo ya mabadiliko ya bei ya umeme ambayo imeanza kutumika kwa sasa.
"
Wandishi wa habari ndio Wenye jukumu la kuwafikishia wananchi tarifa sahihi pindi tu itapotokea mabadiliko ili kuepuka malalamiko na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya umeme. "alisema kaimu huyo.
Aidha amesema kuwa mamlaka imeanda utaratibu wa kuwasajili mafundi wa umeme kwa kuwapatia vibali ili kuepuka usumbufu na matatizo ambayo kwa sasa yameonekana kua ndio chanzo cha uharibifu wakati wa matengenezo.
"tumejipanga kuwafanyia interview wale wote ambao ni mafundi wa njee wa umeme ili kuona yupi anafaa katika kufanya shughuli hizo changamoto kubwa kwasasa imeonekana ni ufungaji wa umeme kienyeji bila ya kua na mchoro ambao unaonesha muundo mzima wa umeme katika nyumban hii husaidia inapotokezea tatizo kujua wapi ilipo anzia wandishi toweni elimu kwa wanachi. alifafanua kaimu huyo.
Akiwasilisha mada na majuku ya mamlaka na uzibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar (ZURA) Afisa uhusiano Makame Suleiman Massoud amesema kua , ZURA ndio yenye mamlaka ya kutoa bei ya mafuta, nishati na maji na kudhibiti huduma hiyo kiufundi zaidi.
Naye Abdallah Hamas Salum mkaguzi umeme kutoka mamlaka ya udhibiti huduma ya maji na nishati zanzibar ZURA akifafanua bei na mfumo mzima wa huduma ya umeme kwa wandishi hao ili kuweza kupeleka Elimu hiyo kwa wananchi ili kupunguza majanga ya umeme ambayo yanajitokeza.
MWISHO.
Comments
Post a Comment