NA MWANDISHI WETU, UGUJA@@@@
Zaidi ya shilingi miloni 700 zimetumika katika ununuzi wa vifaa tiba vilivyokabidhiwa huko hospitali ya Kivunge mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akikabidhi vifaa hivyo mbunge wa Jimbo la Kijini Yahya Ali khamis alisema vifaa tiba hivyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa huduma za wagonjwa.
Ameleza kumekuwa na utekelezaji mkubwa wa miradi lakini kipao mbele Cha kwanza ni kuelekeza nguvu katika miradi ya hospitali.
"Sisi tunajali sana wananchi wetu na ndio maana tukatanguliza vifaa vya afya ambayo ndio msingi wa awali katika maisha yetu wanaadam"alisema
Alieleza tayari miradi mingi ya kimkakati katika Jimbo Hilo unaendelea kufanyika kama vialea miradi ya Maji,umeme,na hata Bara Bara
Mbunge huyo aliwataka wananchi kuthamini nguvu za viongozi wao kutoka na jitihada wazi zichukua kwa kitafura wafadhili wa maendeleo.
Nao wananchi waliohudhuria ghafla hiyo ya makadhiano ya vifaa tiba hospitalini hapo walimpongeza mbunge huyo kwa kutoa msaada huo.
Hata hivyo walimtaka mbunge kutochoka katika kitafura wafadhili Ili weweze kusaidia na nyanja nyengine za kimaendeleo.
Comments
Post a Comment