Skip to main content

Posts

ACT-WAZALENDO CHAKE CHAKE CHAPATA VIONGOZI WAPYA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Chake chake kichama, wamekamilisha uchaguzi wao mkuu, baada ya kuwapata viongozi wapya, watakaokiongoza chama hicho, kwa miaka mitano ijayo.   Katika uchaguzi mkuu huo, umemrejesha tena kwenye nafasi ya Katibu, aliyewahi kuwa Mwakilishi wa majimbo ya Vitongoji na Wawi wakati huo, Saleh Nassor Juma, baada ya nafasi yake kukosa mpinzani. Ambapo katika uchaguzi huo, uliofanyika Gombani Chake chake Pemba, alijizolea kura 65, kati ya kura 73 zilizopigwa, huku kura mbili zikiharibika na kura sita zikimkataa. Aidha Msimamizi wa uchaguzi huo Rashid Ali Abdalla, alimtangaaza Yussuf Salim Khamis, kuwa ndie Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, baada ya kupata kura 39 na kumshinda mpinzake Mohamed Juma Khatib aliyepata kura 34. Katika uchaguzi huo, ulimchagua Khadija Ali Abeid kuwa Mshifa fedha wa Mkoa wa Chake chake kwa kura 36, baada ya kumuangusha mgombea mwenzake, Khadija Anuwar...

WANANCHI PEMBA WASEMA JAMBO FEDHA ZA UVIKO19 KWENYE AFYA

     NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ WANANCHI kisiwani Pemba, wamesema fedha za ahuweni ya UVIKO 19, zilizoelekezwa kwenye miradi ya wizara ya Afya kisiwani humo, zimetumika vyema, na sasa wanaendelea kunufaika nazo. Walisema, serikali iliweka wazi mgao wa fedha hizo na matumizi yake, ambapo kwa upande wa Wizara ya Afya na hasa kisiwani Pemba, zilizitumia kwa ujenzi wa hospitali za kisasa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya kumalizika na kuanza kazi kwa hospitali hizo, walisema majengo hayo yamekuwa ya kiwango cha juu, ujenzi wake. Walieleza kuwa, sasa wameshaachana na majengo ya zamani, ambayo hayakuwa na nafasi, kwa ajili yao na madaktari wanapotoa huduma kwa wagonjwa. Maryam Himid Mjaka wa Micheweni, alisema sasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kukaa kumsubiri daktari, ikilinganishwa na hospitali yao ya zamani. Kazija Haji Mshamata wa Konde, alisema sasa wamekuwa na hamu ya kwenda kutafuta huduma kwenye hospitali ya Micheweni ama Kinyasini, kutokana na...

MJUE MWANAMKE ANAYEZIPENDEZESHA FUKWE KWA USAFI

  NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@ Maisha ya binaadamu huwa   salama na ya afya njema kama mazingira yanayomzunguka yapo safi na salama na yanapokuwa yameharibika huwa hatarishi kwake, wanyama, wadudu na mimea. Hali hii ndio inayopelekea kusikia kila kukicha   wizara ya afya   kwa kupitia wataalamu wake mbali mbali inasisitiz umuhimu wa kuweka mazingira safi ndani na nje ya nyumba zetu, mitaani, vijijini na katika maeneo ya biashara kama masoko au ya kuuza na kununua chakula. Mwanamke amekuwa akionesha uongozi mzuri kwenye jamii zetu kwa kuanzia kwenye familia na kutokana na jamii yetu, katika miaka ya karibuni kutotilia maanani sana usafi wa mazingira kumepelekea kujitokeza watu kuongoza jamii kufanya marekebisho yanayohitajika. Miongoni mwa wana jamii waliojitokeza   kuwa mstari wa mbele kuongoza juhudi za kutunza mazingira ni mwana mama anyeiingoza Kikundi cha Ulinzi wa Mazingira, Siwema   Mshenga   Issa, kutoka Sheiha ya Bubwini Makoba. Yeye ...

ACT-WAZALENDO CHAKE CHAKE: 'CHAGUWENI VIONGOZI WATAKAOKIVUUSHA CHAMA 2025'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa mkutano mkuu maalum wa chama cha ACT-Wazalendo, mkoa wa Chake chake kichama, wametakiwa kuwachagua viongozi wenye uwezo na nia thabiti, ya kukivuusha chama katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025. Ushauri huo,Januari 14, 2024 umetolewa na Mjumbe wa Kamati kuu taifa ya chama hicho, Isihaka Mchinjita, wakati akiufungua mkutano huo, uliofanyika ukumbi cha Chuo cha Samail Gombani Chake chake Pemba. Alisema, wajumbe wa mkutano huo mkuu maalum, ndio wenyejukumu la kuwapata viongozi watakaoshirikiana na wale ngazi ya taifa, katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Alieleza kuwa, ikiwa watafanya makosa kwa kumchagua kiongozi kwa sifa za juu juu pekee, wanaweza kukipa wakati mgumu chama, wakati kinapoingia kwenye chaguzi mbali mbali. Alifahamisha, ili chama kiwe na nguvu, mwelekeo, dira inayotekelezeka, lazima kuwepo kwa viongozi imara kuanzia tawi, jimbo, mkoa na kisha taifa. ‘’Wajumbe wa mkutano huu mkuu maalum wa ACT-Wazalendo hapa mkoa C...

MKURUGENZI USTAWI: 'TUTAENDELEZA USHIRIKIANO NA WADAU KWA MASLAHI YA JAMII'

  NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR@@@@ MKURUGENZI Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee ndugu Hassan Ibrahim Suleiman amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Ustawi wa jamii unakuwa na wananchi wanaishi katika mazingira mazuri na salama. Akifungua mafunzo juu Sera ya hifadhi ya Jamii, yaliyofanyika katika ukumbi wa Sebleni,Unguja amesema ni vyema Idara hiyo kujenga mashirikiana na wadau mbalimbali kwani mtoto anahitaji kukua katika makuzi mema yatakayomjenga kuwa Raia bora kwa Taifa lake. “Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee inabeba jukumu zito hivyo, wanawajibu wa kushirikiana na kusaidia na wadau wengine katika kukuza ustawi wa jamii ili jamii waishi katika mazingira mazuri, hivyo nakuombeni mtowe mawazo yenu juu ya Sera hii, kwani maoni yenu yatasaidia kupata Sera bora” Alisema Hassan. Alieleza kwamba jamii inahitaji mambo mengi hasa ukizingatia kundi la kinamama wanaotelekezwa na watoto wao, wanakuwa ...

WANAWAKE MGELEMA SASA WASHUSHA PUUMZI NI BAADA YA...............

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAWAKE wa shehia ya Mgelema wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa barabara yao kwa kiwango cha lami, roho zao zimewatua na hasa inpotekezea kutaka kwenda hospitali kuu, kufuata huduma za mama na mtoto. Walisema, kwa karne zaidi ya moja, hawakuwa na furaha na wakielewa na machungu, inapotokezea wamepewa rufaa ya kwenda hospitali ya wilaya ya Chake chake, kutokana na shida ya barabara yao, ilivyokuwa. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, mara baada ya kufunguliwa kwa barabara yao ya Kipapo-Mgelema, na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, walisema sasa joto limewatua. Mmoja kati ya wanawake hao Maryam Mohamed Issa, alisema ijapokuwa ni mgeni kijijini hapo, lakini ameshatimiza miaka tisa ya mateso, shida na tabu ya kuitumia barabara hiyo. ‘’Binafsi, mara mbili nilipokuwa mjamzito, nilitakiwa niripoti hospitali ya wilaya ya Chake chake, kwa uchunguuzi zaidi, lakini nilishin...

PEMBE AWATAKA MAMA NTILE WAWE WABUNIFU KIBIASHARA

  Na muandishi wetu @@@@ Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewashauri wajasiriamali nchini, kuendelea kutumia ubunifu wao wa kupika vyakula mbalimbali kwa ajili ya biashara zao za mama ntilie ili waweze kujikwamua na umasikini. Kauli hiyo ameitowa wakati akizungumza na wajasiriamali katika uwanja wa urafiki, Jimbo la Shaurimoyo, Unguja katika mashindano ya mapishi ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapainduzi ya Zanzibar. Mhe Riziki katika yeyete ile inahitaji ubunifu hivyo ni vyema mama ntilie wawe wabunifu katika mapichi mbali mbali katiba biashara ya chakula kwani hatua hiyo itasaidia kuongeza kipato na kujikwamua an umasikini. Waziri Pembe amewataka wajasiriamali hao kuitumia fursa ya mikopo iliyopo   ikiwa ni juhudi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la   mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ya kuwawekea mazingira wezeshi wajasiriamali kwa nia ya   kufikia malengo waliyojiwekea. Aidha amesema Oryx Gas na ...

MAJUKUMU MAZITO YA FAMILIA CHANZO CHA WANAWAKE KUTOGOMBEA UONGOZI

  IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA Jamii ya Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingi nyengine, imejenga mazoea ya kuwa mwanawake ni mama wa nyumbani tu na hapaswi kushiriki au kushirikishwa katika mambo ya maendeleo.   Kwa maana nyengine mwanamke amekuwa kama abiria katika basi na hana maamuzi juu ya safari, seuze ya kupewa usukani wa kuongoza hicho chombo.                      Mtazamo huu uliokuwa unatumika kwa muda mrefu umeiathiri jamii na kumuacha mwanamke kuwa nyuma, jambo ambalo sio sahihi kabisa.   Hali hii ipo kinyume na mafunzo na maelekezo ya dini mbali mbali.    Kwa mfano, katika dini ya Kiislamu mwanamke hatakiwi kuachiwa pekee mzigo mzito wa nyumbani na pamekuwepo matokeo ya mwanamke kupewa uongozi hata katika masuala mazito, kama ya kuongoza kikosi kwenye vita.   Zipo hadithi sahihi na simulizi nyingi juu ya namna wana...

INSPEKTA KHALFAN: ATAKA UDHIBITI MAJANGA YA MOTO

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@   MKAGUZI wa shehia ya Pandani wilaya ya Wete Pemba, Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi, amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kujikinga na majanga mbali mbali yanayoweza kutokea ikiwemo ya moto.   Alisema kuwa, ni vyema kufuata utaratibu nzuri, wakati wanapoamua kujenga nyumba katika maeneo yao, kwa kuweka nafasi ya kutosha baina ya nyumba moja na nyingine, ili linapotokea janga la moto lisiweze kuathiri nyumba nyingi.   Aliyasema hayo wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya skuli, kwa watoto wa familia ya mzee Mwalimu Kombo Said wa kijiji cha Madebeni shehia ya Pandani wilaya ya Wete, kufuatia tukio la moto lililounguza nyumba yao Novemba 11 mwaka jana.   Alisema kuwa, familia hiyo ilipata janga la moto ambao uliunguza nyumba yao na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani, hali iliyomfanya kuiahidi familia hiyo kuwanunulia watoto vifaa vyote vya kusomea.   "Nawapongeza w...