NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR@@@@
MKURUGENZI Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee ndugu Hassan Ibrahim Suleiman amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Ustawi wa jamii unakuwa na wananchi wanaishi katika mazingira mazuri na salama.
Akifungua mafunzo juu
Sera ya hifadhi ya Jamii, yaliyofanyika katika ukumbi wa Sebleni,Unguja amesema
ni vyema Idara hiyo kujenga mashirikiana na wadau mbalimbali kwani mtoto anahitaji
kukua katika makuzi mema yatakayomjenga kuwa Raia bora kwa Taifa lake.
“Idara ya Ustawi wa Jamii
na Wazee inabeba jukumu zito hivyo, wanawajibu wa kushirikiana na kusaidia na
wadau wengine katika kukuza ustawi wa jamii ili jamii waishi katika mazingira
mazuri, hivyo nakuombeni mtowe mawazo yenu juu ya Sera hii, kwani maoni yenu
yatasaidia kupata Sera bora” Alisema Hassan.
Alieleza kwamba jamii
inahitaji mambo mengi hasa ukizingatia kundi la kinamama wanaotelekezwa na
watoto wao, wanakuwa katika hali ngumu ya kukosa uangalizi wao na watoto ambao ndio
tegemeo kubwa la Taifa la kesho.
Naye Afisa kutoka Hifadhi ya Jamii ndugu Rukia Ame Haji wakati akiwasilisha maada juu ya Sera ya Hifadhi ya Jamii, amesema Sera hiyo imeundwa mwaka 2014 hivyo imeonekana kuwepo changamoto kadhaa baadhi ya taasisi hazikutajwa kwenye Sera juu ya majukumu yao, pamoja na kuingizwa sheria ya kulinda Sera katika utekelezaji wake.
Amefahamisha kwamba hivi
sasa wako katika hatua ya kukusanya maoni kwa wadau ili wapate mawazo mbali
mbali na hatimae kuifanyia marekebisho ili Srikali ya Mapinduzi ipate Sera mpya
ambayo itakidhi mahitaji ya jamii katika kustawisha maisha yao.
Wakitoa michango baadhi
ya wadau kutoka taasisi mbalimbali za binafsi wamesema katika masuala ya
Teknolojia sera iangalie uwezekano wa kuwekwa kifaa maalumu kwa watoto kuweza
kuzungumza hasa katika kesi za udhalilishaji kwani watoto wengi waliopatwa na
tatizo la udhalilishaji wanashindwa kujieleza vyema na hivyo kupotea kwa
ushahidi.
Hata hivyo wamesema bado
maboresho ya Sera yanahitajika
kutokanana na kuwa bado hawajafikia kiwango katika ustawi wa Jamii.
Mwisho.
Comments
Post a Comment