Na muandishi wetu
@@@@
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amewashauri wajasiriamali nchini,
kuendelea kutumia ubunifu wao wa kupika vyakula mbalimbali kwa ajili ya
biashara zao za mama ntilie ili waweze kujikwamua na umasikini.
Kauli hiyo ameitowa wakati akizungumza
na wajasiriamali katika uwanja wa urafiki, Jimbo la Shaurimoyo, Unguja katika
mashindano ya mapishi ikiwa ni shamrashamra za miaka 60 ya Mapainduzi ya Zanzibar.
Mhe Riziki katika yeyete ile inahitaji ubunifu hivyo ni vyema mama ntilie wawe
wabunifu katika mapichi mbali mbali katiba biashara ya chakula kwani hatua hiyo
itasaidia kuongeza kipato na kujikwamua an umasikini.
Waziri Pembe amewataka wajasiriamali
hao kuitumia fursa ya mikopo iliyopo ikiwa ni juhudi ya Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt
Hussein Ali Mwinyi ya kuwawekea mazingira wezeshi wajasiriamali kwa nia ya kufikia malengo waliyojiwekea.
Aidha amesema Oryx Gas na Azania
Group, wameamua kwa makusudi kuwasaid wajasiriamali ili
kuhakikisha wajasiriamali wote nchini wanafanikiwa na wanakuwa mfano wa
kuigwa katika kutoa huduma bora za vyakula popote nchini.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la
Shaurimoyo ambae pia ni Waziri wa nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera,
Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe.Hamza Hassan Juma, amesifu juhudi
zinazofanywa na wajasiriamali wa Jimbo la Shaurimoyo kwa kuonesha ubunifu
mkubwa wa vyakula mbalimbali ambao
utawasaidia kutambulika kitaifa na kimataifa.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Oryx Gas Bi Anjela Bitungwa amesema
wameamua kuwapelekea nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda mazingira pamoja na afya kwa
wajasiriamali wa jimbo la Shaurimoyo ili kuwaepusha na madhara ya kutumia kuni
na mkaa na kuahidi kuendelea kuratibu
kwa kutoa mitungi ya gesi 200,
yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 25.
Naye msimamizi wa biashara ya
Azania Group Bw Joel Laiser, amesifu hatua ya maendeleo iliyofikiwa hivi sasa
chini ya Rais Dkt Mwinyi katika kuelekea
miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, huku akieleza kuwa Azania
Group itaendelea kushirikiana na viongozi wa Zanzibar kwa kuwawezesha
wajasiriamali kwa kuwapatia nyenzo zote zinazozalishwa katika kampuni hiyo ili
kuwasaidia wajasiriamali hao.
Washindi watatu wamepatikana na kupatiwa
zawadi, ambapo mshindi wa kwanza katika
mashindano ya mapishi ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amezawadiwa shilingi
laki tano, Mchele, Unga wa Sembe, Unga wa Ngano kilo 50 kilo moja, Sukari na Mafuta lita 20.
Comments
Post a Comment