NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANACHAMA
wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Chake chake kichama, wamekamilisha uchaguzi
wao mkuu, baada ya kuwapata viongozi wapya, watakaokiongoza chama hicho, kwa
miaka mitano ijayo.
Katika uchaguzi mkuu huo, umemrejesha tena kwenye
nafasi ya Katibu, aliyewahi kuwa Mwakilishi wa majimbo ya Vitongoji na Wawi wakati
huo, Saleh Nassor Juma, baada ya nafasi yake kukosa mpinzani.
Ambapo katika
uchaguzi huo, uliofanyika Gombani Chake chake Pemba, alijizolea kura 65, kati
ya kura 73 zilizopigwa, huku kura mbili zikiharibika na kura sita zikimkataa.
Aidha Msimamizi
wa uchaguzi huo Rashid Ali Abdalla, alimtangaaza Yussuf Salim Khamis, kuwa ndie
Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, baada ya kupata
kura 39 na kumshinda mpinzake Mohamed Juma Khatib aliyepata kura 34.
Katika uchaguzi
huo, ulimchagua Khadija Ali Abeid kuwa Mshifa fedha wa Mkoa wa Chake chake kwa
kura 36, baada ya kumuangusha mgombea mwenzake, Khadija Anuwar Mohamed, kumpita
kwa kura moja.
Viongozi wengine
kwa ngazi ya mkoa, waliochaguliwa na wajumbe wa mkutano huo wa mkoa ni Katibu
wa Mipango na Chaguzi, ambapo aliyeibuka mshindi ni Mohamed Ali Salim, aliyepata
kura 55 na kumshinda mpinzani wake, Mbarouk Mohamed Omar aliyeangukia kura 16.
Aidha Msimamizi
huyo wa uchaguzi, alimtangaaza Khamis Abied Mohamed kuwa ndie Katibu wa Habari,
Uenezi wa Mawasiliano ya Umma, baada ya kupata kura 44 na kumshinda mpianzani
wake, Ayoub Yussuf Mgeni aliyepata kura 28.
Kwa upande
wa wajumbe wanne ngazi ya mkoa, ambao lazima wanawake na wanaume idadi sawa,
waliochaguliwa ni Salma Mohamed Ali aliyepata kura 50, Salma Hamad Hassan kura
44, Hamad Khamis Mwalimu kura 48 na Maulid Issa Salim kura 43.
Nafasi ya Mwenyekiti
ngome ya vijana mkoa kupitia chama cha ACT-Wazalendo, aliyechaguliwa ni Yunus
Abrahman Salim, wakati Katibu wake ni Salim Haji Makame, huku ngome ya wanawake
Mwenyekiti akiwa ni Jamila Ali Mohamed na Katibu ni Hazina Ali Saleh.
Wakati huo
huo, Msimamizi huyo wa uchaguzi alimtaangaza Mohamed Abdalla Massoud kuwa ndie
Mwenyekiti ngome ya wazee na Katibu wake ni Faki Saleh Faki, ambao hao watajumisha
katika uongozi wa mkoa wa chama hicho.
Mara baada
ya kumalizika kwa uchaguzi huo, Mwenyekiti wa mkoa Chake chake aliyetetea kiti
chake Yussuf Salim Khamis, aliwataka wanachama wote sasa kuvunja makundi na
kuungana.
Alisema,
sasa macho na masikio wayaelekezwe uchaguzi mkuu wa chama taifa, kisha warudi
kwenye matawi, jimbo na mkoa kwa ajili ya kukijenga chama, ili kurudi kwenye ushindani
kupitia uchaguzi mkuu.
Kwa upande
wake Katibu wa chama Mkoa Saleh Nassor Juma, aliwaahidi wanachama wa
ACT-Wazalendo mkoa wa Chake chake, kufanya juhudi kubwa kuhakikisha, wanaongeza
idadi ya wanachama wapya.
‘’Kwa hili
tushirikiane kwa karibu mno, maana mtaji mkuu wa chama chetu ni kuwa na
wanachama wengi tunaoaminiana, kuwa kitu kimoja na kufanya uamuzi wa pamoja,’’alisema.
Kwa upande
wake Mweyekiti wa ngome ya wanawake Mkoa wa Chake chake Jamila Ali Mohamed,
aliwataka wanawake, kufanya kila juhudi, kuwavuta wanawake wa vyama vyingine,
ndani ya chama chao.
Awali mkutano
huo mkuu maalum, ulifunguliwa na Mjumbe wa Kamati kuu ya ACT-Wazalendo Isihaka
Mchinjita, ambae aliwaeleza kuwa wajumbe wa mkutano huo, ndio wenyejukumu la
kuwapata viongozi watakaoshirikiana na wale ngazi ya taifa, katika kukijenga
chama.
Alieleza kuwa,
ikiwa watafanya makosa kwa kumchagua kiongozi kwa sifa za juu juu pekee, wanaweza
kukipa wakati mgumu chama, wakati kinapoingia kwenye chaguzi mbali mbali.
Mwisho
Comments
Post a Comment