NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
WANACHAMA
wa mkutano mkuu maalum wa chama cha ACT-Wazalendo, mkoa wa Chake chake kichama,
wametakiwa kuwachagua viongozi wenye uwezo na nia thabiti, ya kukivuusha chama katika
uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Ushauri huo,Januari 14, 2024 umetolewa na Mjumbe wa Kamati kuu taifa ya chama hicho, Isihaka Mchinjita,
wakati akiufungua mkutano huo, uliofanyika ukumbi cha Chuo cha Samail Gombani
Chake chake Pemba.
Alisema, wajumbe
wa mkutano huo mkuu maalum, ndio wenyejukumu la kuwapata viongozi watakaoshirikiana
na wale ngazi ya taifa, katika kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Alieleza kuwa,
ikiwa watafanya makosa kwa kumchagua kiongozi kwa sifa za juu juu pekee, wanaweza
kukipa wakati mgumu chama, wakati kinapoingia kwenye chaguzi mbali mbali.
Alifahamisha,
ili chama kiwe na nguvu, mwelekeo, dira inayotekelezeka, lazima kuwepo kwa
viongozi imara kuanzia tawi, jimbo, mkoa na kisha taifa.
‘’Wajumbe wa
mkutano huu mkuu maalum wa ACT-Wazalendo hapa mkoa Chake chake, nyinyi
mnaangaliwa na wanachama wote wa mkoa, mkifanya makosa mtajuta,’’alieleza.
Akizungumzia
suala la makundi, wakati wa kuelekea uchaguzi wa chama, alisema ni jambo lisiloepukika,
lakini linatakiwa kuzima mara moja, baada ya matokeo kupatikana.
Alieleza kuwa,
mara mshindi anapotangaazwa, huwa ni kwa ajili ya wanachama wote, na hapo
hutakiwa kuungana pamoja, ili kukipatia chama ushindi.
‘’Makundi
katika uchaguzi na chama chochote huwa hayaepukiki, lakini kinachotakiwa kuepukwa
ni kuendeleza makundi hata nje ya uchaguzi,’’alifafanua.
Katika hatua
nyingine, Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya ACT-Wazalendo taifa, Isihaka Mchinjita,
aliwataka viongozi watakaochagauliwa, mara baada ya matokeo kutoka, kusahau
makundi yao.
‘’Niwaombe
sana, viongozi ambao leo (jana) mtachaguliwa, msijemkaendeleza makundi, bali
muyavunje na sasa iwe ni kazi yenu kushirikiana na wanachama, na viongozi wa
juu kukijenga chama.
Aliongeza kuwa,
kila chama cha siasa huwa na majukumu mawili makuu, ikiwemo kuongoza serikali
ama kuikosoa, kuiuliza na kuipongeza wakati inapofanya vizuri chama kinachoongoza.
Mapema Mwenyekiti
wa cha chicho mkoa kichama Chake chake Yussuf Salim Khamis, alisema wanachama
wanayohaki ya kumchagua kiongozi wamtakae, ambae ana maono ya kukijenga chama.
Aliongeza kuwa,
wakati wa kupanga safu ya uongozi kupitia mikutano mikuu ndio sasa, hivyo si
busara mwanachama kujilaumu, kwa kumpa kura kiongozi asiyemtaka.
Hata hivyo,
alisema kazi kubwa imefanywa na viongozi waliopita, licha ya kukabiliwa na
changamoto ya rasilimali fedha kwa kutokua na chanzo cha mapato.
Mapema Katibu
wa ACT-Wazalendo mkoa huo, Saleh Nassor Juma, alisema kwa sasa wanaendelea na
changuzi ngazi ya mkoa baada ya kuhitimishwa kwa chaguzi ngazi ya wilaya.
Mjumbe wa
Kamati ya uongozi wa ACT-Wazalendo mkoa wa Chake chake Khamis Abeid Haji, alisema
katika uchaguzi huo, watakaochaguliwa ni pamoja na Mwenyekiti, Katibu mkoa.
Wengine watakaochaguliwa
ni Katibu wa mipango mkoa, Katibu wa habari na uenezi, mshika fedha nafasi iliyogombewa
na wanachama wawili wawili, samba mba na wajumbe wanne wa kamati ya uongozi
mkoa, wenye uwiyano sawa kati ya wanawake na wanaume.
Alisema kuwa,
wajumbe wingine watakaochaguliwa kwa nafasi za ukatibu na mwenyekiti ni ngome
za wazee, wanawake na vijana.
‘’Nafasi
nyingine ni mshika fedha wa ngome mkoa, katibu wa mipango, katibu wa habari na
uenezi wa ngome pamoja na wajumbe wanne wakiwemo wanawake na wanaume wenye idadi
sawa,’’alifafanua.
Hata hivyo,
amesema ushindani kwa baadhi ya nafasi umekuwa mkubwa, kwa kule wanachama wao
kuhamasika kuomba nafasi mbali mbali.
Viongozi hao
watakaochaguliwa kwa nafasi mbali mbali, watakiongoza chama hicho, kwa kipindi
cha miaka mitano ijayo.
Mwisho
Comments
Post a Comment