NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WANUFAIKA wa sadaka ya
nyama ya Ng’ombe, zaidi ya 189 wa shehia za Wambaa na Chumbageni wilaya ya
Mkoani Pemba, wamepongeza hatua ya jumuiya ya udhu-hiya ya shehia hizo, kwa
kukamilisha bila ya kasoro, zoezi la ugawaji wa sadaka hiyo.
Walisema, wamefakiniwa kupata nyama hivyo kwa ajili
hya kukamilisha mlo wa sikukuu, tena kwa wakati, jambo ambalo walijiona sawa na
wingine, wenye uwezo wa kifedha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, kwa
mashatri ya kutochapishwa majini yao, mara baada ya kupokea sadaka hiyo,
walisema walipatiwa wastani kilo 1.5, ambayo wingi wao walipata na sikukuu ya
pili.
Walisema, uwepo wa Jumuiya hiyo, kwa miaka mitatu
mfululizo sasa, imekuwa ikiwahakikisha kupata kitoweleo, jambo ambalo kama sio
sadaka hiyo, wapo wanaokula dagaa kavu ama samaki siku hiyo.
Walisema, hatu hiyo imekuwa ikiwarahisishia maisha
walau kwa siku mbili za sikukuu, jambo ambalo hujiona ni sawa na wingine wenye
uwezo.
Mnufaika mwingine mwenye watoto watano, mkaazi wa
kijiji cha Chumbageni, alisema alishasikia kuwa kuna uchinjaji wa Ng’ombe tisa
mwaka huu, ingawa hakuwa na uhakika kwamba engefikiwa na sadaka hiyo.
‘’Nilishajipanga ikifika saa 6:00 kama sijaona
sadaka hiyo, basi nijitayarishe kwa harage, lakini baadae niligongewa mlango na
kukabidhiwa nyama,’’alisema.
Mapema Mwenyekiti wa kamati hiyo Khamis Khatib
Khamis, alisema kwa mwaka huu, waliongeza Ng’ombe, kutoka sita wa mwaka jana
hadi tisa.
Alisema, kitendo hicho kilipelekea wanufaika 189 wa
moja wa moja kupata nyuma, yenye ujazo wa kilo 1.5 kwa kila mmoja, kwa
utaratibu ulioekelezwa na Allah.
Alieleza kuwa, mfumo wa upatikanaji wa Ng’ombe hao,
ni kila waislamu saba, humiliki Ng’ombe mmoja, na kisha kila mmoja hupendekeza
majina matatu, kwa wale wenye hali ngumu ya maisha.
‘’Kisha ndani ya nyama hiyo, fungu moja ni kwa ajili
ya kitoweleo, na fungu jingine mwanachama mwenyewe, huwapatia ndugu, jamaa na
majirani wake,’’alifafanua.
‘’Kadiri wanachama walivyokuwa wingi, ndivyo ambavyo
wale wasiokuwa na uwezo nao wanaongezeka kupata sadaka hii, ambayo inamanufaa
makubwa, mbele ya Muumba wetu,’’alifafanua.
Mshika fedha wa Jumuiya hiyo Ali Ussi, alisema
mchango wa shilingi 160,000 huwawezesha wanachama saba, kukusanya shilingi
milioni 1,120,000, ambazo zinatosha kupata Ng’ombe mmoja, kwa ajili ya
uchinjaji unaokubalika.
‘’Ndio maana kwa msimu huu, kwa wanachama wetu 63,
wastani wa shilingi milioni 10, zilichangwa na kununuliwa Ng’ombe hao tisa,
waliowafikiwa wanufaika 189 wale wa moja kwa moja,’’alifafanua.
Wanachama wa Jumuiya hiyo Subira Haji Makame na Time
Makame Ussi, waliwataka wanawakwe wenzao, kujiingiza kwenye jumuiaya hiyo, kwa
kupata manufaa ya milele.
‘’Wanawake wanakuwa na akiba kila wakati, na ndio
maana hakuna harusi ambayo hawaichangii, sasa akiba nzuri zaidi mbele ya
Muumba, ni kwenye maeneo kama haya,’’walishauri.
Kwa mwaka huu, kati ya Ng’ombe hao tisa
waliochinjwa, wanaufaika wote kwa ujumla ni 252, wakiwemo 63 wanachama na 189
waliofikiwa, huku ikikadiriwa waliokula sadaka hiyo kwa mwaka huu ni zaidi watu
1,000.
Mwisho




Comments
Post a Comment