NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, katika uzinduzi
wa tamasha la 31 la utamaduni wa mzanzibari, linalotarajiwa kufanyika leo hii,
uwanja wa michezo Gombani Chake chake Pemba.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika, kuanzia
majira ya saa 8:00 jioni ya leo, na shamara shamara na maandalizi ya tamasha
hilo zitaanzaa mapema, uwanjani hapo.
Akizungumza na mwandishi wa habari, Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Dk.
Omar Salum Mohamed alisema, maandalizi yote yameshakamilika, kwa ajili ya uzinduzi
wa tamasha hilo.
Alisema kuwa, lengo kuu la kuanzishwa tamasha
hilo, ni kuhakikisha wazanzibari wanaendelea kukumbushwa, kuelimishwa na
kushajiishwa, kuzingatia mila silka, desturi, maadili na mambo mengine yote
yanayohusu utamaduni wao.
"Katika tamasha hili hapa kisiwani Pemba mchana wa leo, tunatarajia
sana, kuwa mgeni rasmi awe Rais wetu wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, maana
yeye ndio, mpenda utamaduni wa mwanzo ndani ya taifa hili,’’alisema.
Alisema kuwa, katika tamasha hilo, litawakumbusha na litawarithisha
vijana, kuendelea kuhifadhi utamaduni wao wa kizanzibari, ili vizazi viendelee
kurithi.
Alieleza kuwa, tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo
kwa mwaka huu ni 31, na matarajio yao, ni kushiriki zaidi ya vikundi 20 vya
burudani na ngoma za asili na kuwepo kwa wajasiriamali wa bidhaa za kiutamaduni,
wasiopungua 50.
Aliongeza kwa upande wa Pemba katika tamasha hilo,
kwa kuanzia litazindulìwa leo hii, na litadumu wastani wa siku nne, na
litaendelea kisiwani Unguja hadi Septemba
25.
Alibainisha kuwa, baada uzinduzi huo uwanja wa michezo
Gombani, kesho Septemba 20, wataelekea Wete, ukumbi wa Baraza la Wawakilishi,
kwa kupambwa na vikundi mbalimbli vya maulidi ya home, dufu, mnanda na maagizo
yenye mnasaba na utamaduni.
Alisema kuwa, Septemba 21,
watahamia wilaya ya Mkoani, ambapo tamasha hilo la 31 la utamaduni wa mzanzibari,
litahusisha manahoza 15, wakiwania ushindi wa kwanza, kwa resi za ngalawa.
Kamishna huyo alisema, siku inayofuata baada ya Rais wa Zanzibar kulizindua,
litakuwa Pujini, kwa kupambwa na resi za baskeli, zitakazoanzia Kiwani hadi
Pujini.
‘’Niwaombe wananchi kwa hili, wasikubali kuhadithiwa, maana baada ya
kuwapokea washindi wa biskeli, uwanja wa mpira wa Pujini, sasa utanogeshwa kwa
mchezo wa Ng’ombe,’’alifafanua.
Aidha Kamisha huyo alifahamisha kuwa, mbali na
matukio hayo, kuendelea wajasiriamali watakuwa katika kiwanja hicho cha Gombani
kwa siku zote, wakiendelea na burudani na sarakasi, kama kawaida, kuanzia saa
2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.
Akizungumzia kuhusu tamasha hilo, alisema kwa upande wa Unguja,
litahamia kuzia Septemba 23 hadi 25, ambapo nako shughuli kadhaa, zitafanyika.
Hivyo,
amewaomba wasanii, waandishi wa habari, wanafunzi, viongozi wa chama na
serikali na wananchi wa Pemba, kuwasili mapema leo uwanja wa Gombani.
Mapema Kaimu Ofisa Mdhamini wizara ya Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo Pemba Sharifa Hamad Shapandu, amezishukuru kamati za
maandalizi ya tamasha hilo, kwa kufanikisha shughulizi walizopangiwa.
Alisema kamati hizo, zimekuwa zikifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na
wa pamoja, jambo lililofanikisha uzinduzi huo na shamra shamra zake.
"Zipo kamati zaidi ya tano, zilizozinduliwa kwa ajili ya kufanikisha
hafla ya tamasha hilo, ambapo mchana wa leo, kiongozi wetu Dk. Hussein Ali
Mwinyi anatarajiwa kulizindua,’’alifafanua.
Hata hivyo amewataka wakuu wa Idara zilizomo ndani ya wizara hiyo, kuwakumbusha
watendaji wote wa wizara, kuhudhuria kwa wingi kwenye tamasha hilo.
Kwa upande wake, Mkuu
wa Divisheni ya Utamaduni Pemba Hamad Ali Haji, alisema tamasha hilo litakuwa
la aina yake kwa mwaka huu, kwa kuvishirikisha zaidi ya vikundi 10 vya ngoma
asili, kutoka Unguja na Pemba.
Alisema, tangu
kuanzishwa kwa tamasha hilo, kwa mwaka huu, ambalo ni 31, kwa wanachi
watakaojitokeza watanufaika na mambo makubwa, ikiwemo resi za ngalawa, Punda,
msewe wa zamani na sasa, taarab asilia na mbio za baiskeli.
‘’Kwa mwaka huu
wizara yetu ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, chini Waziri Riziki Pembe
Juma Khamis na Katibu Mkuu Matar Zahor Massoud, tamasha hili, litakuwa la kuvutia
na si la kukosa,’’alisisitiza.
Tamasha hilo lililoasisiwa mwaka 1995 na Rais mstaafu wa Zanzibar awamu
ya tano Dk. Salim Amour Juma na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, imekuwa
likitekeleza agizo hilo la kuendesha tamasha hilo kila mwaka.
Ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema ‘UTAMADUNI WETU NDIO URITHI KWA
VIZAZI VYETU’
MWISHO.



Comments
Post a Comment