Skip to main content

ZSSF YATAKA MAFAILI YA WATUMISHI WANAOSTAHIKI KUPATA MAFAO YASICHELEWESHWE

 



IMEANDIKWA NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@

MAAFISA Utumishi kwenye taasisi za Serikali na binafsi wametakiwa kutokuchelewesha mafaili ya watumishi wanaohitaji stahiki zao za mafao ZSSF, ili kuondosha usumbufu unaojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi hiyo.

Akizungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba, Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) Pemba, Msabah Massoud Msabah alisema, kuna haja ya kuwa na Ofisa maalumu ambae atashughulikia mafaili hayo na sio kubadilishwa.

Alisema kuwa, kumekuwa na ucheleweshwaji mkubwa wa mafaili ya watumishi ambao wanastahiki kupatiwa mafao yao kwa namna moja ama nyengine, jambo ambalo linaweza kuchukua muda mrefu kupatikana kwa haki, na wakati mwengene wanaweza kuikosesha kabisa, kwani kuna muda maalumu uliopangwa kwa ajili ya kuwasilisha vielelezo.

“Tushirikiane pamoja katika hili kuhakikisha wanapatikana watendaji maalumu, ambao hata kwenye mafunzo watakuwa wanakuja hao hao kwa ajili ya kuwajenga zaidi kiufanisi katika kazi zetu, hii itaondosha usumbufu,” alisema Mkurugenzi huyo.



Alisema kuwa, lengo la mkutano huo ni kuimarisha utendaji kazi wa maofisa hao, kwani ZSSF ndio kwenye maisha ya baadae ya watumishi.

Akielezea Dhana ya Hifadhi ya Jamii, Mkuu wa Kitengo cha Sheria ZSSF, Ramadhan Juma Suleiman alisema, ni utoaji wa hifadhi ya jamii kupitia mifumo ya bima ya jamii au mifumo ya lazima ya akiba na Pensheni, ambapo wafanyakazi na waajiri wao hutoa michango ya lazima kwa mfuko wa hifadhi ya jamii, kwa mujibu wa sheria ambayo hutumika kutoa mafao kwa wanachama wanapokabiliwa na hatari za kijamii.

Alieleza kuwa inaaminika kidunia kwamba, kila mmoja anatabiriwa changamoto, na ndio maana ZSSF inahakikisha mwanachama wao anapata kinga kwa kupatiwa mafao yake, kwa ajili ya kuendeleza kipato chake hata akiwa amepatwa na majanga.

“Tumeweka utaratibu huu maalumu, ili kumsaidia mtumishi kupata kipato cha kujiendeleza kimaisha, ikiwa amepatwa na ugonjwa, ajali, upotevu wa ajira, uzee na uzazi, hivyo maofisa mnatakiwa kulijua hili na kuwaelimisha watumishi, ili wasikose haki zao hizi,” alisema.



Kwa upande wake muwasilishaji mada ya Mafao ya upotevu wa ajira, Rashid Shoka Salim alieleza kuwa, ni kiwango maalumu cha fedha kinachotolewa kwa mwanachama aliepoteza ajira kutokana na sababu zilizoainishwa kwenye Sheria na kanuni za mafao hayo.

Alisema ili mwanachama aweze kupata fao hilo, ni lazima awe ameachishwa kazi kuanzia Oktoba mwaka 2022, awe amechagia kwa kipindi kisichopungua miezi 18, awe amekosa kazi kwa kipindi cha miezi sita, awe mtanzania na pia awe ameachishwa kazi na muajiri wa mwisho.

“Lakini hawezi kupata fao hili mtumishi ambae ameacha kazi mwenyewe,  au alieachishwa kazi kwa kosa la nidhamu, rushwa, wizi, ubadhirifu au ameacha kazi kwa shughuli za kisiasa,” alisema Shoka.



Nae Muwasilishaji wa Fao la kuumia kazini, Meneja Mafao ya Muda Mfupi ZSSF Zainab Rajab Baraka, alitaja changamoto zinazowakabili ni, kuchelewa kuwasilisha taarifa za ajali kwa wakati, wanachama kuripoti kwa madaktari kwa ajili ya kupatiwa siku za mapumziko na utambuzi wa maradhi yatokanayo na kazi kwa wafanyakazi.

“Mfanyakazi anaestahiki kulipwa mafao ya kuumia kazini ni, yule ambae ni mwanachama wa ZSSF, michango yake ya asilimia moja inawasilishwa kwetu, amepatwa na majeraha, maradhi au kifo kutokana na kazi bila kukusudia, na ameshindwa kufanya kazi kuanzia siku tatu,” alifahamisha.



Mshiriki wa mkutano huo kutoka hoteli ya Mantarif, Suleiman Kombo Ali alisema, elimu waliyoipata ni faida kwao kwani yamewajengea uwezo mkubwa wa kuelewa haki zao kwenye Mfuko huo, kwa sababu sekta binafi ajira sio za kudumu, hivyo wengi hupoteza haki zao.

“Awali ilikuwa hatujui kuhusu fao la upotevu wa ajira, hivyo kupitia elimu hii tutawafundisha wengine, ili waelewe na kupata haki zao za msingi, tunaewapongeza ZSSF kwa kutuelewesha, tumefurahi sana,” alisema mwakilishi wa hoteli ya Fundolagon Kessi Shehe.

                                           MWISHO.

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...