Skip to main content

SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR BADO NI KIZUNGUZUNGU


NA SITI ALI, ZANZIBAR@@@@

“Sheria ni msingi wa haki amani na maendeleo kwa kila nchi “Hayo si maneno yangu bali yalikuwa ni  maneno ya Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizindua toleo jipya la juzuu za sheria mwezi  Aprili ,2025 jijini Dar es salaam.

Anasema, bila ya sheria kuwa wazi uhakika wa ulinzi wa haki za raia unatoweka au unakuwa hauna uhakika na kusababisha uvunyifu wa amani.   

Wandishi wa Habari Zanzibar wamekuwa wakidai sheria nzuri na rafiki ya habari bila ya mafanikio yoyote.Kutokana na kutumia sheria ya zamaani na iliyopitwa na wakati  iliyotungwa tokea miaka ya 1988 ambayo kwa sasa ni kikwazo kwa wandishi wa habari.

Akizungumzia kuhusu sheria hiyo, mwandishi nguli wa habari visiwani Zanzibar, Salma Lusangi anasema ni muhimu kwa sasa sheria hiyo ibadilishwe ili iendane na wakati na kukidhi matakwa ya wakati husika.

“Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifanya uchechemuzi wa sheria mbili kuu yaani sheria ya Wakala wa Habari Magazeti na Vitabu ya mwaka (1988) na sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar (1997) ambazo waathirika wakubwa ni wandishi wa habari na jamii kwa ujumla” anasema Salma na kuongeza kuwa. 

“Sheria za Habari zilipotungwa kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii ila sasa tuna mitandao ya kijamii hivyo ni lazima twende na wakati, sheria iifanyiwe marekebisho ili iwe rafiki na ilete tija”.




Salim Said ni mhariri na Mjumbe wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania TEF anasema anaamini kwamba  nia ya kupatikana sheria mpya ya habari haipo kwa Serikali ya Zanzibar, kwani haitaki kuifanyia kazi suala la marekebisho ya sheria za habari na badala yake imekuwa ikifanya udanganyifu kwa kutoa ahadi za uongo.

“Tokea suala hili lizungumzwe na sisi wadau wa habari, tumekuwa tukipewa ahadi tofauti, mfano tupo njiani, tupo mbioni hizo hazina mwanzo wala mwisho, hata Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alipoingia madarakani tulikutana nae, alituahidi hivyo na mpaka sasa hakuna kilichofanyika” anasema Salim.

Salim hakuishia hapo anaona kuwa Waziri wa Wizara hiyo  Tabia Maulid Mwita imekuwa tabia yake , kila anapoulizwa kwa takribani mara tatu 3 ameahidi mswada huo utasomwa katika Baraza la Wakilishi ahadi ambayo hadi sasa haijatimia.

“Katika miaka 20 hii tunayopigania uhuru wa habari, tunashuhudia Baraza la Wawakilishi Zanzibar limepokea na kuzirekebisha au kutunga sheria zaidi ya 10 lakini wanaifumbia macho sheria ya habari”.

Anawasihi viongozi kuiga mifano ya nchi jirani na wanapaswa kujiuliza kwanini nchi kama Uganda, Rwanda na Tanzania bara wamefanya marekebisho ya sheria na kuweka mazingira mazuri ya waandishi wa habari kupaza sauti zao na kutoa maoni ya wananchi.

Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025, wandishi wa habari wanabanwa kufanya kazi zao kwa uwazi na wanapojaribu kuhoji kuhusiana na kitu fulani wanaitwa wachochezi.



Mwanaharakati na mtetezi wa maswala ya habari Zanzibar Juma Khamis Juma, anasema sheria ya habari ni muhimu katika kuimarisha uhuru wa kujieleza na kutoa maoni katika nchi yoyote duniani.

 “Zanzibar ni sehemu ya nchi hizo, ingawa sheria iliyopo ni ya muda mrefu ambayo imetungwa tokea mwaka 1988, miaka mitatu ijayo itatimiza miaka 40, hivyo bila shaka kuna haja ya kuwa na sheria mpya ya habari”.

Juma anaogeza kuwa, sheria ya sasa ya habari ina changamoto ambazo wadau wanaamini zinawakwaza katika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwemo mamlaka makubwa aliyopewa askari polisi kuingia katika chombo cha habari bila ya idhini au kwa idhini ya mahkama.

“Sheria pekee haiwezi kusaidia kuboresha mazingira ya kazi, lakini uwepo wa sheria na utashi wa kuitekeleza ndio utaleta mabadiliko yenyewe”.
 
Suala la haki za kibinaadam linalenga pia uwepo wa sheria zinazoangalia mustakbali wa uhuru wa kupata, kutafuta na kupokea taarifa au habari, Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Msaada wa Kisheria Zanzibar (ZALHO) Harusi Miraji Mpatani anasema  suala la  uhuru wa habari ni suala la haki ambayo  imeelezwa katika kifungu cha 18  cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984  ambayo inasema kila raia ana haki ya  kutoa na kupokea taarifa
.
“Tunahitaji sheria ambazo zitaamini kuwa suala la habari ni suala la haki, ambayo inatakiwa kutolewa bila ya makando kando yoyote ambayo unapewa kwa mkono wa kushoto na unanyang’anywa kwa mkono wa kulia” anasema Harusi kwa msisitizo huku akiongeza kuwa kuna athari kubwa kwa jamii kama hakuna sheria nzuri za habari kwani kutapelekea kuenea kwa habari zisizo sahihi.

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-Z wamekuwa katika harakati za mageuzi kwenye suala la uhuru wa habari na kupatikana kwa sheria nzuri zitakazolinda maslahi na usalama wao.



Afisa mradi wa masuala ya utetezi na uchechemuzi kutoka TAMWA-Z Zaina Abdallah Mzee anasema kuwa wanachukuwa jitihada mbalimbali za kuzisemea sheria zote zinazohusu habari ambazo haziko huru na rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari  ambazo ni sheria ya Wakala wa Habari Vitabu na Magazeti ya mwaka 1988, Sheria ya Tume ya Utangazaji, Sheria ya Uchaguzi na nyenginezo ambapo sheria zote hizi zinawagusa waandishi wa habari na vyombo vya habari na badala yake kupendekeza kuwekwa sheria moja tu ambayo ni rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari katika kazi zao.

“Tumekuwa tukipaza sauti zetu kwa muda mrefu sasa kupatikana sheria mpya ya habari Zanzibar kuzisemea sheria ambazo zina mapungufu kwa waandishi wa habari na badala yake kupendekeza sheria moja tu ambayo ni rafiki kwa waandishi wa habari”.

Zaina anaelezea mashirikiano yao baina ya Kamati ya Wataalam wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO na serikali ikiwa ni pamoja na kukutana na kufanya mazungumzo  na viongozi wa  nchi akiwemo Rais na Waziri wa Habari ,Tume ya kurekebisha sheria ,Idara ya habari maelezo na wajumbe wa baraza la wawakilishi ambapo wote hawa wamekiri kuwepo kwa mapungufu katika sheria ya habari iliyopo.

“Mashirikiano ni mazuri baina yetu na serikali kwani tumepata kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali wa nchi na wao wamekiri kuwepo kwa mapungufu katika sheria ya habari iliyopo na kuwahidi kufanyia marekebisho”. 

Abdallah Mfaume ni mjumbe wa Kamati ya Wataalam wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO anasema kuna umuhimu mkubwa wa kuharakishwa kwa sheria mpya ya habari ili iwasaidie waandishi wa habari hasa katika kutekeleza majukumu yao.

“Waandishi wa habari wanahitaji utulivu, usalama na ulinzi ili jamii inufaike kupitia fani hiyo ambayo ndiyo yenye jukumu la kuhabarisha jamii”.

Baraza la Habari Tanzania MCT lilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kunawepo kwa mabadiliko ya Sheria za Habari Tanzania bara wakifanya shughuli zao hapa Zanzibar wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa sheria mpya na rafiki kwa wana habari.

Ziada Kilobo ni Msimamizi wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania upande wa Zanzibar anasema kuwa suala la sheria nzuri za habari ni suala la kupewa kipaombele hasa kwa nyakati hizi ambazo tunaelekea kwenye uchaguzi.
“Kukiwa na sheria nzuri wanahabari wanaweza kuwasaidia wakafanya kazi zao kwa weledi na kuna umuhimu wa kuwa na sheria mpya na zenye kulinda maslahi ya waandishi na hata jamii”

Ziada ameongeza kuwa kwa upande wa serikali ni vyema kuona suala hili kuwa linahusua maisha ya jamii zaidi.
“Serikali ione suala hili kuwa ni muhimu kwa nchi na kwa jamii maana uhuru wa Habari ni suala linalotoa nafasi kwa waandishi kuzisemea changamoto na mafanikio yaliyopo kwenye jamii yao”.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...