NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa
wa kusini Pemba, kimepiga marufuku kwa watia wa nafasi mbali mbali, kuacha
kujipotisha pitisha kwa wajumbe, na kuanza kampeni za chini kwa chini, kwani
wakati wake haujafika.
Akizungumza na mwandishi wa
habari katibu wa CCM mkoani humo, Kajoro Vyohoroka, alisema huu sio wakati kwa
watia nia kujipitisha karibu na makaazi ya wajumbe na kuanza kampeni.
Alisema, CCM inaomfumo mzuri
wa kidemokrasia wa kuwapata wajumbe watatu, ambao ndio watashushwa chini kwa ajili
ya kupigiwa kura, na sio sasa kuanza kufanya jambo lolote.
Alieleza kuwa, ni marufuku
kwa sasa kwa watia nia hao, kufanya jambo lolote linaloashiria kampeni ama
kuingilia utaratibu wa vikao vya chama, na badala yake wawe watulivu majumbani
mwao.
‘’Ni kweli kuwa, hatua ya
kwanza ya kuwapata wagombea wetu kwenye uchaguzi mkuu, umeshakamilika hivyo,
watia wastahamili waanze kishindo cha kuwasilimu wajumbe, huu wakati wake bado,’’alifafanua.
Aidha alisema, atakaekaidi utaratibu
huo na akibainika, sheria na mingozo cha Chama cha Mapinduzi inaweza kutumika
na kujikuta amejindoa mwenyewe.
‘’CCM ndio mwalimu wa
demokrasia kwa vyama vyingine vyote nchini, hivyo hata wanachama wake wanatakiwa
wawe wavumilivu kwa kufuata utaratibu uliopo,’’alieleza.
Katibu huyo wa CCM mkoa wa
kusini Pemba, Kajoro Vyohoroka, alisema anaviamini mno vikao vya juu vya chama
chake, kwamba havitashusha wagombea wasiokuwa na sifa.
‘’Kwa mujibu wa utaratibu,
kila nafasi watashushwa wagombea watatu, ambapo hapo kisha wale wajumbe wa ngazi
ya majimbo, ndio ambao watapigia kura,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, aliwasisitiza
wajumbe na watia nia kujitenga mbali na mazingira ya rushwa, kwani ndani ya CCM
jambo hilo ni dhami kubwa.
‘’Unajua wasisi wetu hayati
Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na marehemu Abeib Aman Karume, wameacha
misingi ambayo hadi leo ni mizuri kwa maslahi ya taifa,’’alifafanua.
Kwa upande wake Katibu wa CCM
wilya ya Wete Rished Omar Khalfan aliwataka watia nia wote kuwa watulivu katika
kipindi hichi, cha kusubiri mamuzi ya ngazi ya juu ya chama.
Taarifa zinaeleza kuwa, wapo
wanachama 270 wakiwemo wanawake 71 na wanaume 199, waliohitokeza kuomba nafasi
za Ubunge na Uwakilishi katika majimbo 18 kisiwani Pemba.
Kati hao 270, walioomba
nafasi ya Ubunge wote walikuwa ni 147, wanawake wakiwa 40 na wanaume 107, huku
kwa nafasi ya Uwakilishi wote waliomba ni 123, wakiwemo wanawake 31 na wanaume 92.
Wilaya ambayo wanawake
walijitokeza kwa wingi ni wilaya za Micheweni na Mkoani zilizokuwa na watia nia
idadi sawa ya 19 kwa nafasi ya Ubunge na Uwakilishi kila wilaya.
Wilaya iliyoshika nafasi ya tatu
kwa wanawake wa CCM kujitokeza kwa wingi ni wilaya za Wete, iliyoibua wanawake 17,
huku wilaya ya Chake chake ikishika nafasi nne, kwa watia nia 16.
Zoezi la uchukuwaji wa fomu kwa
watia nia kwa nafasi wa CCM mbali mbali, lilianza Juni 28 na kumalizika Julai 2
mwaka huu nchi nzima.
MWISHO.
Comments
Post a Comment