NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@
MSAIDIZI shehia ya
Pandani wilaya ya Wete, Inspekta wa Polisi Khalfan Ali Ussi, amesema, ushirikishwaji
wa jamii katika dhana ya ulinzi shirikishi, kutasaidia vijana kujitambua na
kuishi kwa kuzingatia madili katika jamii.
Aliyasema hayo mara
baada ya kukamilika kwa bonanza la michezo, lilifanyika katika uwanja wa mpira
katika kambi ya ‘FFU’ Finya wilaya Wete.
Alisema vijana ndio
wahanga wakubwa katika jamii kwenye matokeo mbali mbali ya uhalifu, hivyo wanapaswa
kupewa elimu itakayowawezesha kujitambua na kuacha matendo yaliyokinyume na
maadili ya jamii.
Alieleza kuwa,
kundi hilo nalo ni muhimu mno katika jamii ya leo na kesho, hivyo
lazimalitazamwe kwa jicho pan ana kukua wakiwa na maadili mema.
"Mabonanza
kama haya yakiendelea kufanyika yatawasaidia wao, kuhamisha akili yao katika
matendo ya kihalifu na kushiriki katika michezo, ambayo tija yake ni kubwa,’’alifafanua.
Aidha aliwasisitiza
vijana hao kuzingatia masomo yao, kwani umri wao ndio sahihi wa kutengezeza
hatma yao ya kesho, na kufikia malengo waliyojiwekea.
"Musijishirikishe
kwenye matendo maovu wala uvunjaji wa sheria, hususani katika kipindi hichi
tunachoelekea cha uchaguzi mkuu, msikubli kushawishiwa hata kidogo,"alieleza.
Kiongozi wa tasisi
hiyo Edward Frednand Lukwimbi alieleza kuwa tasisi hiyo, inajishughulisha na eneo
la elimu rika, inayowalenga vijana kujitambua na kujiepusha na vitendo viouvu
ikiwemo dawa za kulevya, wizi na udhalilishaji.
"Tumekua na
mchango mkubwa, katika jamii kwa kuwatumia vijana wa jinsia zote, ili kufikisha
ujumbe kwa jamii, kupitia michezo kwa kushirikiana na taisis za kiserikali na
zile za binafsi,"alifafanua.
Aidha kiongozi wa
timu ya vijana ya Elgado Academy Salum Faudh, alieleza kuwa bonanza hilo
limefanikisha katika kukuza umoja na ushirikiano kwa kuwakutanisha vijana tofauti
wa wilaya zote za kisiwa cha Pemba.
Bonanza hilo la siku moja, limewashirikisha vijana 350 wa kike na kiume, huku mchezo wa mpira wa miguu ambao uliwashirikisha vijana chini miaka 17 timu ya Elgado Academy, iliibuka na ushindi na kuzawadiwa jenzi seti moja na timu ya Kukuu Sports Academy mshidi wa pili.
kukabidhiw
zawadibya mipira,huku mchezo wa nage nao kwa wasichana timu ya Kangani Sister
ikichukuwa usingi na kukabidhiwa zawadi.
Mwisho
Comments
Post a Comment