Skip to main content

WATAALAMU WA SHERIA: ‘CHIPS KUKU ZISIWE CHANZO CHA UDHALILISHAJI’'

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

WANAFUNZI wa vyuo, skuli za msingi na sekondari za wilaya ya Micheweni, wametakiwa kujiepusha na kupokea zawadi ovyo ovyo zikiwemo chips kuku, kwani huwa ni chanzo za kudhalilishwa na baadhi ya watu.

 

Hayo yameelezwa leo Juni 2, 2025 na maafisa sheria kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la Polisi, Maafisa  ustawi na wanasheria wingine, kwenye kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassaan inayoendelea. 


Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Micheweni Bizume Haji Zume, alisema wapo baadhi ya wadhalilishaji, huanza kuwapa zawadi watoto ikiwemo chakula cha chips na fedha, hivyo ni vyema wakajiepusha navyo.

 Alieleza kuwa, wapo wengi ambao wameshadhalilishwa kwa kuwa rahisi kupokea zawadi ambazo mwisho wake, hudhalilishwa na kufanyiwa ukatili.

 

‘’Wanafunzi, mhakikishe hampendi kupokea zawadi za ovyo ovyo, kama chips na fedha na hata msaada wa usafiri ‘lift’ kwa watu wasiowafahamu, maana athari yake ni mbaya,’’alifafanua. 

Kwa upande wake, Wakili wa serikali Zubeir Awamu Zubeir, aliwakumbusha wanafunzi kuwa, kwa sasa jukumu lao ni kusoma na sio kujiingiza katika vitendo vya uasharati.

 

‘’Kwa muda huu, wanafunzi nyinyi jukumu lenu ni kusoma na sio jingine lolote, maana maisha yenu yanaanzia hapa katika skuli na vyuo,’’alifafanua.

 

Mapema Inspekta wa Polisi kutoka kituo cha Polisi Chake chake Saleh Ame Makame, amewataka wanafunzi kuhakikisha wanawaripoti wale wote wanaoonesha nia ya kutaka kuwaharibia maisha yao.

 



Akizungumzia lengo la kampeni hiyio, Afisa sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Pemba, Ali Salim Hamad, alisema inataka kuwafikia wananchi hasa wa kundi la wanawake, watoto, watu wenye ulemavu na wasiojiweza.

 

Alieleza kuwa, Mama Samia katika ziara zake, aliposhuhudia wapo wananchi kadhaa, wanalilia haki zao na hawajuai wapi wazifuatilie.

 

‘’Baada ya kuona hivyo, ndio maana aliamua kuanzisha kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria, ili wananchi wajue haki na wajibu wao, na kuhakikisha wanapata haki zao,’’alifafanua.

 

Mwanasheri wa Halmashauri ya wilaya ya Micheweni Rukia Khamis Said, aliwakumbusha wanafunzi hao, kuwahimiza wananchi kulipa ada na matozo mbali mbali, ili serikali ipate kujiendesha.

 

Mwalimu mkuu wa skuli ya sekondari ya Mtemani Hamad Bur-han Daudi, alisema ujio wa kampeni hiyo, imesaidia kupata taaluma, ambayo yengepaswa kulipiwa.

 

‘’Leo kupitia kampeni hii, tumejua haki na wajibu wa watoto, haki za binaadamu na hata malengo ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia,’’alieleza.

 


Nae Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Singida kilichopo Wingwi Salim Khamis Bakari, ameiomba timu hiyo kurejea tena katika chuo hicho, ili kutoa elimu zaidi.

Wanafunzi wa skuli hizo, walisema ujio wa kampeni hiyo, imewapa fursa ya kuuliza maswali yao kadhaa ya kisheria, ambayo yalikuwa yakiwakwaza.

 


Mwanafunzi Aisha Haji Machano wa skuli ya Mtemani, alitaka kujua ikiwa mtoto aliyedhalilishwa anaweza kumsaidiaje, ili asiathirike kiakili.

 

Mwanafunzi anayesomea ualimu chuo cha ualimu cha Singida, Jokha Mohamed Said, alitaka kujua ikiwa kwa mtoto aliyebakwa anaweza kumfanyia vipi ikiwa wazazi wamepanga kuimaliza kesi kienyeji.

Mwisho 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...