Skip to main content

KAMPENI YA MAMA SAMIA YA KISHERIA YATANGAAZWA KWA WANAFUNZI MICHEWENI

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@

KAMPENI ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan, imetangaazwa kwa wanafunzi wa skuli ya skondari ya Maziwang’ombe na wale wa Chuo cha kiislamu Micheweni.

 

Wataalamu wa masuala ya kisheria kutoka ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la Polisi, Mawakili wa kujitegemea, Maafisa ustawi wa jamii na wanasheria wa halmashauri, walifika leo Juni 1, 2025 kwenye kampeni maalum inayoendelea.

 


Wakizungumza kwenye mikutano hiyo ya wazi, walisema kampeni hiyo inakuja kuwaelezea wananchi na hasa wanawake, watu wenye ulemavu, waliomo kwenye makundi maalum na wasiokuwa na uwezo, kujua haki na wajibu wao kisheria. 


Inspekta Saleh Ame Makame kutoka kituo cha Polisi Chake chake, aliwataka wanafunzi hao, kuripoti wanapoona viashiria vya udhalilishaji dhidi yao na wasivifumbie macho. 



Alisema, kama lengo la kampeni hiyo ni kuwaelezea haki na wajibu wao, hivyo wahakikisha wanawaripoti wanaowanyemelea kutaka kuwadhalilishaji.

 


‘’Leo kampeni ya msaada wa kisheria imefika kwenu, sasa ni wakati wenu kuzijua haki hizi na kuyajua maeneo ya kuripoti matukio mbali mbali,’’alisema.

 

Nae Mratibu wa kampeni hiyo kwa wilaya ya Micheweni kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, Khamis Bakar Amani, alisema matokeo ya kampeni hiyo ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Alisema, wakati anafanya ziara katika maeneo kadhaa ya Tanzania, alishuhudia wananchi mbali mbali, wakilalamikia kukosa uwezo wa kufuatilia haki zao kwa wanasheria, kwa kukosa gharama.

 


‘’Leo kampeni hii, sasa iko kwa wananchi mbali mbali, na lengo lake ni kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria bila ya malipo,’’alifafanua.



 


Mapema Wakili wa serikali kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba Zubeir Awamu Zuebir, akizungumza na wanafunzi cha Chuo cha Kiislamu Micheweni, alisema moja wapo ya haki za mtoto, ni kupatiwa cheti cha kuzaliwa.

 

‘’Kwa ambae hana cheti cha kuzaliwa, sheria ziko wazi kuwa anatakiwa afuate taratibu ikiwemo kwenda kwa shehe wake na kisha anaweza kulipa ada kidogo, kwa ajili ya kupatiwa,’’alifafanua.

 

Hata hivyo, Mwanasheria kutoka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Pemba Massoud Ali Massoud, amewakumbusha wananchi wa wilaya ya Micheweni, kuzitumia siku tisa za kampeni hiyo, maalum kupata ufafanuzi wa masuala yao ya kisheria.

 


‘’Mabanda yetu yapo Wete eneo la Jamhuri holi, sasa mnaweza kufika na malalamiko yenu ya kisheria, iwe migogoro ya ndoa, ardhi, mipaka, vyeti vya kuzaliwa wanaweza kupewa ufafanuzi bila ya malipo,’’alieleza.

 

Awali Msaidizi Mkuu wa Chuo cha Kiislam Micheweni CCK, Maryam Hemed Said, aliwataka wanafunzi wanaoyemelewa na waalimu kwa matendo ya udhalilishaji, kuwaripoti katika vyombo mbali mbali.

 

‘’Hata kama anayekutaka kimapenzi ni mwalimu wako wa darasa ama mwalimu mkuu, kwa vile ana nia ya kutaka kukuharibia, toa taarifa hapa Polisi, au ustawi wa jamii, ili hatua zichukuliwe,’’alieleza.  

 

Awali kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mkoa wa kaskazini Pemba, ilizinduliwa Oktoba 17, 2024 wilaya ya Micheweni, na kitaifa itamalizika Febuari mwakani.

Mwisho 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

HABARI ZA HIVI PUNDE

 TAARIFA za hivi punde, zilizofikia ofisi ya Pemba Today, zinaeleza kuwa, Jeshi la Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia askari mwenzao, kwa tuhuma za ubakaji ndani ya moja ya kituo cha Polisi kisiwani Pemba Muume wa mwanamke aliyedai kubakwa na Mwanamke mwenyewe, wamedai kutokea kwa tendo hilo, na huku Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, akithibitisha kupokea kwa lalamiko hilo.... Kwa taarifa zaidi ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu, ambao kukuhabarisha ni fahari yetu...