Skip to main content

MICHEWENI WAKUMBUSHWA KUZISAJILI NDOA ZAO

 


NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@

KADHI wa wilaya ya Micheweni sheikh Mansab Khamis Omar, amewakumbusha waumini wa dini ya kiislam wa wilaya hiyo, kuzisajili ndoa zao, ili kupata cheti kinachotambulika.

 

Kadhi huyo, aliyasema hayo leo Juni 3, 2025 kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wananachi hao, kwenye muendelezo wa mikutano ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa sheria ya Mama Samia, iliyofanyika Tumbe na Chimba.

 


Alisema, unaposajili ndoa, kisha unakabidhiwa cheti ambacho kinaweza kusaidia pindi ikitokezea siuntafahamu katika maisha ya ndoa hapo baadae.

 

Alieleza kuwa, cheti hicho pia husaidia kupatikana kwa uhakika wa maandishi, iwapo mmoja kati ya wanandoa hao amefariki.

 

‘’Cheti cha ndoa ni muhimu mno, maana kinaweza kukusaidia hata, unapoomba vyeti vyingine mfano cheti cha kuzaliwa kwa watoto watakaopatikana,’’ aliwakumbusha.

 

Katika hatua nyingine, Kadhi huyo wa wilaya ya Micheweni, aliwataka wazazi na walezi kusimamia kwa karibu ndoa za watoto wao, na wasiwe chanzo cha kuzivunja.

 

‘’Pale mahakamani tunapokea kesi na kisha ndoa kuvunjika, ingawa ukikaa na wanandoa, wanaeleza kuwa wazazi na wamekuwa sehemu ya kuzivunja ndoa za watoto wao,’’alieleza.

 


Mapema Afisa sheria kutoka Kamisheni ya wakfu Pemba Massoud Ali Massoud, aliwakumbusha waumini hao wa dini ya kiislamu, kuitumia ofisi yao wanapotaka kurithi mali za marehemu wao.

 

‘’Moja ya faida kubwa ya kufika ofisini kwetu na kurithishwa, ni kupewa nyaraka halisi za umiliki, ambazo zinaweza kuongeza thamani ya ardhi, shamba ama nyumba iliyorithiwa,’’alisisitiza.

 

Kwa upande wake Mratibu wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia wilaya ya Ali Salim, alisema ujio wa kampeni hiyo ni maono ya Mama Samia, katika kuhakikisha wananchi wasiokuwa na uwezo na wanawake, wanapata msaada na ushauri wa kisheria.

 

Alisema, tayari kampeni kama hiyo imeshazinduliwa kwa mkoa wa kusini Pemba, na kuwepo kwa kambi maalum pamoja na wataalamu wa masuala ya sheria, kuwafikia wananchi walipo.

 


‘’Hapa ambacho alikusudia Mama Samia, ni kuona hakuna mwananchi analalamikia kukosa haki yake na akidai kukosa gharama za kumtafuta mwanasheria au wakili,’’alisisitiza.

 

Mwalimu mkuu wa skuli ya sekondari ya Shumba Vyamboni Baraka Seif Hamad, alisema kampeni imekuja wakati mwafaka katika skuli yake, kwa vile wanafunzi wake, hawana uwelewa wa mausala ya kisheria.

 

Mwananchi wa Chimba wilaya ya Micheweni Hamida Haji Said, alisema kwa sasa amepata uwelewa wa masuala la mirathi na kujua faida ya kurithishwa serikalini.

 

Nassor Haji Hamdani wa shehia ya Mihogoni, alishauri kuwa, ujio kama huo ufanyike kila baada ya miezi sita, ili wananchi wapate kutoa malalamiko yao.

 

Timu ya wataalamu wa masuala ya sheria kutoka Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka, ofisi ya mwanasheria mkuu, Halmashauri, ustawi wa jamii, wakala wa matukio ya kijamii na ofisi ya kadhi, itaendelea kesho kwa shehia za Konde na skuli zake.

Mwisho  

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kuta...