Skip to main content

MSAADA WA KISHERIA WAWAOKOA WATOTO WANAOKINZANA NA SHERIA ZANZIBAR




NA AMINA MCHEZO, PEMBA@@@@

   Msaada wa watoto kisheria, kisera na kimipango ni uwanja mpana huku ikionekana sheria iliopo Sasa ya mtoto sheria namba 6 ya mwaka 2011 inamapungufu hivyo wizara ya Màendeleo ya jamií, jinsia, wazee na watoto Zanzibar inafanya juhudi kuhakikisha sheria hiyo inapitiwa upya.

   Sheria hiyo Kwa Sasa inaonekana bado haitoi ulinzi Bora Kwa mtoto hivyo Kwa Sasa wadau na taasisi za usimamizi wa mtoto wamekuwa wakiisindikiza tume ya marekebisho ya sheria ili kuwe na sheria mpya.
 
    "Kwa Sasa tumeshatoka kwenye hatua nyingi za ukusanyaji wa maoni ya wadau na Sasa nadhani tupo katika hatua ya kuishirikisha tume ya marekebisho ya sheria ili tuone kwamba tunapata baraka za mwisho na kunipeleka mbele ili tuwe na sheria mpya ili mambo yawe mazur Kwa watoto" Amesema mkuu wa wa Division  ya hifadhi ya mtoto kupitia idara ya ustawi wa jamii na wazee.

   Mtoto anaekinzana na sheria ni mtoto yeyote alie chini ya umri wa miaka 18 ambae amefanya makosa ya kijinai ikiwemo kubaka, kulawiti, wizi na makosa mengine.
 
  Utafiti umebaini kuwa watoto wengi wanaokinzana na Sheria ni wale watoto wa mzazi mmoja, ndoa kuvunjika, Kukosa matunzo Kwa wazazi wake, hivyo watoto hao hupelekea kuathirika kiakili Kwa kujiingiza katika  makundi maovu na kufanya makosa ya kijinai.

   Kiuhalisia kutokana na sababu hizo inaonekana wazi watoto wanaokinzana na sheria wengi wao ni wale waliopitia udhalilishaji Kwa namna Moja au nyengine kutokana na Kukosa malezi sahihi na Kukosa haki zake za msingi kama mtoto.

    Msaada wa kisheria Kwa watoto wanaokinzana na sheria umeibua hisia tofauti Kwa wanajamii hasa pale wanapoona makosa ya namna hiyo yakijirudia Kila mara
     
     Wengine wanasema kupatiwa msaada wa kisheria ni sawa tu kwani wale ni watoto mengi wanayafanya Kwa kutokujua.
   
     Huku mitazamo ya wengine yakionekana kubeba hisia Kali na kukataa kabisa watoto wale kupewa msaada wakidai kuwa ni njia Moja ya watoto hao kuendelea kutenda makosa Kila siku.



     "Sioni sababu ya watoto wanaotenda makosa kupewa msaada wa kisheria  kwani nao wanajielewa na wakisaidiwa  kisheria yaani watoto watakuwa wanajiamini Sana" Wamesema baadhi yao.


      Mitazamo hiyo ya baadhi ya wanajamii inaonekana kuwa bado hawajafahamu Zaid namna mtoto anavyohitaji usimamizi Kwa mujibu wa sheria.

      Mtumwa Ameir Ali msaidizi wa sheria kutoka wilaya ya mjini amesema bado baadhi ya  wanajamii hawajaelewa kuhusu kutolewa Kwa msaada wa kisheria Kwa watoto wanaokinzana na sheria.

      Amesema ushawishi wao ni mkubwa Kwa kutafuta wakili wa usimamizi wa kesi za watoto pamoja na wao kumpa elimu na ushauri ili asirudie tena kosa Lile.

     Amefahamisha kuwa kumuacha mtoto aliekinzana na sheria ni kumkosesha haki zake za msingi ikiwemo kusoma pindi tu atakapokaa chuo Cha mafunzo Kwa Kukosa usaidizi wa kisheria.
    
     "Baadhi ya wajamii hawana uwelewa Kwa sababu wanaona yule mtoto ameshatenda Lile kosa kwanini sisi tunakaa tunamtetea lakini jamii hawajui kuwa Lile kosa linaweza kuwa lisiwe lake au amefanya kosa Kwa ule utoto tu." amesema.

     Bi mtumwa amesema ijapokuwa wao sheria inawabana kuingia mahakamani lakini hawawezi kumuacha mtoto aliekinzana na sheria hivyo wanaanza ngazi za awali ikiwemo polisi ili apate haki yake Kwa wepesi na haraka. 

    Jumla ya kesi 129 zimeripotiwa katika mahakama tofauti visiwani Zanzibar kuanzia January Hadi November 2023 zinazowahusu watoto waliokinzana na sheria ,  Kwa mujibu wa kitengo Cha TAKWIMU Dawati la Jinsia Makao Makuu ya polisi Zanzibar.

    Ambapo kesi 70 ni Kwa mkoa wa mjini magharib, 8 mkoa wa kusini unguja, 21 Kwa mkoa wa kaskazini unguja, 16 Kwa mkoa wa kusini Pemba na kesi 14 Kwa mkoa wa kaskazini Pemba.


   Akizungumza na mwandishi wa makala hii mratibu  wa Dawati la  jinsia makao makuu ya polis Zanzibar Sajent Rahma Ali Salum amesema watoto wanaokinzana na sheria wanawaangalia kama watoto wengine hasa katika kuwasaidia Kwa kuwapatia elimu ya kujitambua.

   Amesema  katika usaidizi wao wa kisheria Kwa watoto wa namna hii wanashirikiana na wasaidizi wa sheria, waratibu wa shehia pamoja na ustawi wa jamii  Kwa kusikiliza kesi zao Kwa  pamoja.

     Sagent Rahma amefahamisha kuwa  ni wajibu wa watoto wanaokinzana na sheria kupatiwa msaada kutokana na mazingira yanayojitokeza wakati wanapofanya makosa.

    "Tikifuatilia kesi zao nyingi ni ushawishi wa watoto wezao, wengine kuwa na njaa kutokana na Kukosa chakula nyumbani ilimradi makosa yao mengi ni ya ushawishitu" Amesema Sagent Rahma.

   Amesema Dawati la jinsia wanapopokea kesi za watoto waliotenda makosa wanawaita wazazi wao kuwafahamisha namna ya kukaa na mtoto wake kwani wazazi wengi huwachukia watoto wao kutokana na makosa yao.

   " Msaada wa kisheria Sana wanapewa na wasaidizi wa sheria wanakuwa pamoja na wazazi wao sisi tunawafahamisha namna Yale makosa yalivyo na mtoto akaenae vipi Kwa sababu wazazi wengine  wanakuwa wakali na kimchukia "Amesema.

       Amefahamisha kuwa katika kuwasaidia watoto wamekuwa wakipelekwa katika mahakama ya watoto ili wapate uhuru wa kujieleza mbele ya mahakama.

    Jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA ni jumuiya isiyo ya kiserikali ambayo inatoa msaada wa kisheria Kwa wanawake na watoto imesema Kuanzia January Hadi November 2023 jumla ya kesi 11 za watoto wanaokinzana na sheria  zimefika ofisini kwao na wameanza  kuzishughulikia Kwa kuwapatia msaada wa kisheria na kesi 3 tayar zimeshapatiwa ufumbuzi Kwa kutozwa faini.

   Mwanaisha Mustapha ni mwanasheria kutoka jumuiya ya wanasheria wanawake Zanzibar ZAFELA amesema Kwa watoto wanaokinzana na sheria wamekuwa wakiwasimamia Kwa hali ya juu kwani wengi wao makosa yao ni ya kusingiziwa au ya kulipiziwa visasi Kwa baadhi ya wanajamii waliomzunguka.

    Amesema wao kama wanasheria wanasimama kwenye sheria ya mtoto inavyozungumza katika kumlinda kama mtoto mwengine mpaka pale mahakama itakapomtia hatiani Kwa kosa Lile.

    Amefahamisha kuwa hali ya Sasa asilimia kubwa watoto Kwa watoto wanafanyiana udhalilishaji jambo ambalo wanataasisi zinazotoa msaada wa kisheria wamekuwa macho ili  jamii ibaki kuwa salama.

   "Ni janga kubwa hali ya udhalilishaji na hali ya Sasa hivi iliokuwepo asilimia kubwa watoto Kwa watoto ndio wengi ambao wanafanya haya matukio Kwa iyo tukiwaangali kisheria wote ni watoto na wote wanataka kulindwa na sheria" Amesema mwanasheria.

    Shirika la msaada wa kisheria nà haki za binaadam  Zanzibar ZALHO kupitia wakili wake bi Jamila massoud  amesema jumla ya kesi 19 wanazishuhulikia katika shirika lao huku kesi 7 zikiwa zimeshafikishwa mahakamani Vuga zinazowahusu watoto wanaokinzana na sheria.

    Amesema  shirika limekuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano na wanajamii ili kuzungumza nao na kuwafahamisha kwanini watoto waliokinzana na sheria wanatakiwa kupatiwa msaada wa kisheria.

   Amebainisha kuwa pale wanaposhughulikia kesi za watoto wanaokinzana na sheria wanashauri Sana kubadilishiwa makaazi pale anapokuwa tayar ameshakuwa mtoto mwema kwenye jamii ili asirudia tena makosa yale.

    "Tunawapa muelekeo au tunawapa utaalamu kwanini tunawasaidia hawa watoto Kwa sababu hawa ni Victim wa udhalilishaji ukiangalia mtoto anaekinzana na sheria utagundua kuwa nae kadhalilishwa Kwa namna Moja au nyengine" Amesema.


      Mohd Khamis Faki mkaazi wa kazole anaemlea mtoto wa dada yake  ajulikanae Kwa jina Khamis Mwadini Kheir mwenye umri wa  miaka 16 alishtumiwa Kwa kosa la kukashifu mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 mnamo mwezi wa march 2023 huko maeneo ya Daraja bovu wilaya ya maghari A unguja.

     Katika shtaka Hilo lililopekea kufikishwa kituo Cha polisi Mwera na kesi kupelekwa mahakamani Vuga mjini unguja, ndugu Mohd Khamis amesema baada ya kufikishwa mahakamani shtaka la mjomba wake awali walishindwa Kwa Kukosa wakili kutokana na hali yao ya kimaisha.

      "Tulipandishwa mahakamani Vuga tulishindwa kupata wakili kutokana na hali zetu ndipo tukaunganishwa na Mtu kwenye hili shirika hili pale mikunguni linalosaidia watu wasio na uwezo na Kwa uwezo wa Mwnyezi Mungu Lile shirika lilitusaidia mpaka kesi ilipomalizika na alhamdullillah hatukutozwa  ushuru wowote ule" Ameongeza

      Amesema msaada walioupata kutoka shirika la ZALHO ni mkubwa kwani walishindwa na fedha za kuwapa wakili ili kuwasaidia kesi ya mjomba wake na Kwa Sasa mjomba wake huyo yupo huru na amejifunza kutokana na kosa Lile pamoja na kimkataza kufika katika mtaa aliopatia mtihani huo.

     "Kwa Sasa tumempiga Marufuku kufika mitaa ya Daraja bovu ambako ndipo alipo huyo binty kwenye hiyo nyumba aliofika mjomba wangu na Kwa Sasa hata hasogei kwani ulikuwa ni mtihani tu ule kwake" Amesema.

    Wizara ya Màendeleo ya jamií, jinsia wazee na watoto Zanzibar imesema hali ya upatikanaji huduma kisheria Kwa watoto ni ndogo na ndio maana wameona Kuna haja ya kutia mkono sheria iliopo Sasa ili kuboreshwa Kwa huduma.

   Mkuu wa Division ya hifadhi ya mtoto idara ya ustawi wa jamii na wazee ndugu sheikh Ali Sheikh amesema watoto wanaokizana na sheria sheria bado inamtanzama kama mtoto mbali ya kuwa wanatenda makosa lakini sheria inataka kuwalinda pia na kupewa haki zao.

   Amesema kama idara inatoa msaada wa kisheria Kwa kuwasimamia mahakamani hadi pale hukumu zinapotokea ambazo kikawaida ni kutozwa faini tu na sio kufungwa baadae idara inawapeleka vituo vya kurekebisha tabia kwenda kupata ujunzi na kujiweka sawa.

   "Tunamsaidia kama mtoto kama sheria inavyotaka atizamwe Kwa hiyo Kuna maafisa wetu mahakamani kuhakikisha juu ya kesi zao kama watenda makosa lakini mwisho wa siku Sheria inataka iwalinde" amesema.

    Kwa mujibu wa Wizara husika, taasisi za usaidizi wa sheria, waratibu na wadau mbali mbali mbali, suala la usaidizi wa sheria linahitaji kupewa kipaumbele Zaid huku wazazi nao wakitakiwa kusimamia msingi mzima wa malezi Kwa watoto wao ili kupatikana kizazi chenye maadili mazuri.

MWISHO..........0772694778


 


Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo ni vy

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan