NA KHADIJA OMAR, PEMBA@@@@
MJASIRIAMALI wa uchongaji na utengenezaji wa
bidhaa za miti, Mohamed Hamza Khamis wa Kuyuni shehia ya Ngwachani wilaya ya
Mkoani, ameziomba mamla husika kutoa ruhusa ya haraka ya ukataji miti, mara
wanapokamilisha taratibu.
Alisema, inawezekana kufuata taratibu zote
kuanzia kwa sheha hadi Idara ya misitu, kwa ajili ya kukata miti ya mbao ingawa
changamoto ni ucheleweshaji wa utaji wa kibali husika.
Hayo yamelezwa na mjasiriamali huyo, wakati
alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizim kijijini hapo, juu ya
changamoto anazopitia katika kazia yake.
Alisema, jambo hilo la kucheleweshwa kupewa
kibali, humuwawia vigumu na kusababisha migogoro isiyokuwa ya lazima na wateja
wake, kwani wanakuwa hawamuelewi.
Alieleza kuwa, kufanya hivyo wakati mwingine
kunasababisha kumkimbizia wateja kwani, wengi wao hupenda kazi zao zifanywe kwa
haraka mno.
''Changamoto yangu kubwa ni kucheleweshwa
kupewa kibali cha ukataji miti ya mbao, hata kama nimeshakalimisha taratibu
zote zikiwemo kulipia ushuru kwa idara husika,’’alieleza.
Akizungumzia kuhusu vifaa anavyotumia, alisema
hadi sasa anatumia misumeno ya nguvu, shoka, landa yay a kutumia mokono jambo
ambalio humpelekea kuchoka mno.
Alifafanyua kuwa vifaa alivyonavyo sio vya
kutosha, na kumsababisha wakati mwingine hata kuchelewa kumaliza kazi za wateja
wake.
‘’Kama kuna mfadhili japo kwa njia ya mkopo
naomba, na mimi kupatiwa vifaa vya kukatia na kusafishia bidhaa zangu, maana
kwa hakikia napoteza nguvu sana,’’alieleza.
Kuhusu rasilimali anazozitumilia, alisema
anazinunua kutoka miji ya kama vile Kangani, Kengeja ingawa kutokana na gharama
ya usafirishaji hupata gharama ndogo.
‘’Kwa mfano magogo ninayonunua kwa shilingi
milioni 1 na kutengeneza bidhaa kama kabati la milango miwili, gharama zake hadi
kukamilika ni shilling 300,000, na kisha kulazimika kuliuza kati ya shilingi
400,000 hadi shilingi 500,000 na kujipatia faida ya shilingi 150,000,’’alifafanua.
Hata hivyo alisema anaweza kutengeneza vifaa
vyingine kama vile viti, fremu za madirisha, milango na meza ndogo ndogo za
chumbani.
Kuhusu changamoto anazokumbana nazo, mjasiriamali
huyo, Mohamed Hamza Khamis, alisema kuwacheleweshea baadhi ya wateja wake,
kutokana na kukosa vifaa vya kileo.
‘’Mteja anaweza kutoka masafa ya mbali na kuja
kufuata bidhaa zake, lakini akifika akanikuta naendelea kugonga gonga na kuweka
urembo sanwa,’’alisema.
Mmoja katia wateja wa mjasiriamali huyo , Ali
Omar Ali alisema kama atapatiwa vigfaa vya kileo, anaweza kuzalisha bidhaa
nzuri zaidi.
Alieleza kuwa, amekuwa kila wakati ananunua
bidhaa za mbao kwake na wakati mwingine hata kusafirisha kwenda kwa watu
wengine, kutokana na ubora wake.
‘’Ni kweli mimi ni mteja maarufu wa
mjasiriamali huyo, na amekuwa akichonga kitanda, makabati na meza za aina mbali
mbali, lakini changamoto yake hadi leo anatumia vifaa vya nguvu kazi,’’alisema.
Kiwanda cha kuchongea fanicha mbali mbali
kilichopo Kuyuni Ngwachani, mjasiriamali huyo, amekianzishwa mwak 1992 kwa
mtaji wa shilling 70.
MWISHO
Comments
Post a Comment