NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
UONGOZI wa skuli ya kiislamu Thamaratu-nnisai iliyopo
Machomane wilaya ya Chake chake Pemba, imewakumbusha wazazi na walezi, kulipa
ada zao kwa wakati, ili kurahisisha ufanisi wa usomeshaji skulini hapo.
Akizungumza na wazazi na walezi wenye
wanafunzi skulini hapo, Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Bimkubwa Habibu, alisema
wapo baadhi ya wazazi, bado wamenakuwa wazito kulipa ada za watoto wao.
Alieleza kuwa, hilo linachangia uzoroteshaji
wa skuli hiyo, ikiwemo usomeshaji na hata malipo ya mishahara ya waalimu walipo
skulini hapo, ambao wanazitegemeza ada hizo.
‘’Nyinyi wazazi na walezi, ambao mmewaleta watoto
wenu skulini hapa, jambo la kwanza mhakikishe suala la ada halichelewi, maana
ndio tegemezi kuu, kwa maendeleo yote ya skuli hii,’’alieleza.
Aidha Mwalimu Mkuu huyo amewakumbusha wazazi
na walezi hao kuwa, wakumbuke kuwa, skuli hiyo hina mfadhili, anaeiendesha bali
inategemea mno ada watakazozilipa kwa ajili ya watoto wao.
Akizungumzi kuhusu changamoto inayoikabili
skuli hiyo, Mwalimu mkuu huyo alisema ni ukosefu wa huduma ya umeme, vikalio,
maji safi na salama na madara mingine kubali na vumbi.
Alisema kua wanafunzi wanapata shida kutokana
na miundombinu katika skuli hiyo, kwani skuli bado haijapata ufadhili kwa ajili
ya kuendelea majengo yake na wanafunzi wakasoma kwa utulivu.
"Katika skuli hii hatuna viti vya kukalia
wanafunzi, hatuna compyuta, huduma ya nishati ya umeme, na kwa sasa jingo tunalotumia
linahitajia ukarabati mkubwa, kwa hivyo tunaiomba serekali na wafadhili wingine
kututupia jicho,"alifafanua.
Aidha alisema kua kulingana na muendelezo
mazuri wamatokeo ya wanafunzi wao, wataanzisha darasa la tisa (kidato
cha kwanza) kuanzia mwaka 2024, wakati hapo awali walikua wanafundisha
mwisho darasa la saba pekee.
Hata hivyo alieleza kua kwaupande wa
watoto wa elimu ya maandalizi, watakao wandikishwa mwaka 2024, watasoma madrassa
hapo hapo, pale utakapofika muda wakuondoka skuli wao watabakia kwa ajili ya kusoma
qur-an.
"Tutakua tunawanapatia chakula
cha mchana na baadae wataanza kusoma qur-an kuanzia muda wa saa 8:00 mchana hadi
saa 12:00 jioni na kurejema majumbani,"alifafanua.
Kwaupande wake Msaidizi mwalimu mkuu wa skuli
hiyo Amina Salim alisema kua, wazazi na walezi wajitahidi kuleta kuongeza ushirikiano
baina yao na waalimu kwani, kufanya hivyo kutasababisha kuwatia nguvu na hamasa
waalimu katika ufundishaji wao.
"Kuna ada mbalimbali ambazo wazazi
wanatakiwa kulipa kwa wakati, zikiwemo za kulipia usafiri wagaro, dakhalia, mitihani,
siku ya wazazi ‘parent day’ pamoja na ada ya safari kwa wanafunzi,’’alifafanua.
Aidha alisema kua kuanzia mwaka 2024, wazazi
watatakiwa kulipia ada kupitia mifumo ya kibenki, kwani kufanya hivyo
kunaweza kuepuka usumbufu unajitokeza baina ya wazazi na walimu, hasa juu ya
deni la wamafunzi.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wazazi na walezi
akiwemo Omar Ali, alitaka kujua watakapoanzisha kidato cha kwanza, wanafunzi
watakua na walimu wa kutosha ambao wataweza kuwasaidia katika masomo yao ya
kila siku.
‘’Mimi nataka kujua, maana kila skuli inauhaba
wa waalimu, na sisi Thamarat Nissai, tunao waalimu wa kutosha na watakaosomesha
masomo yote na kwa wakati,’’alihoji mzazi huyo.
Nae mzazin Burhan Said, aliuomba uongozi wa skuli
hiyo, kuanzishwa kwa kamati ya wazazi, ili kusaidia kupanga mikakati mbali
mbali, ili kuihuisha skuli hiyo na chamngamoto kadhaa.
" Tukiwa kama sisi wazazi tutaunda kamati,
ili kila mmoja kama anamtu ambae yupo juu kidogo kimaisha, akamuelezea
changamoto zetu na akazisikiliza basi tutaweza kupata maendeleo mazuri yale
ambayo walimu wetu wanayalilia kwamuda mrefu,"alieleza.
Aidha aliwashukuru walimu wa skuli hiyo ya Thamarat
Nnissai kuweza kufikiria kuweka madrassa ya qur-an ambayo itawasaidia watoto kupata
utulivu wa kutafuta elimu.
‘’Naelewa kuwa, skuli hii na hasa waalimu wengi
ni wanawake, hivyo sasa iwe fahari kwanza, hakuna mchanganyiko na wanaume
lakini sasa iwape kasi na ari ya kufanyakazi,’’’alishauri.
Skuli hiyo ambayo ilianzsishwa mwaka 2014
ikiwa inawanafunzi wanane, wa waalimu wawili wanakwe, hadi sasa inao wanafunzi
206 na walimu 13, ambao wote ni wanawake na madarasa tisa.
Mwisho
Comments
Post a Comment