NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MAAFISA mawasiliano na habari wa
Jumuia za wasaidizi wa sheria Tanzania zimetakiwa kujenga ushirikiano wa karibu
na watendaji wenzao, ili kuhakikisha wanakuwa na mifumo sahihi ya utoaji wa
taarifa za jumuia.
Hayo yameelezwa na Mtaalamu wa masoko kutoka LSF Gilsant Mlaseko, wakati
akizungumza na maafisa hao kwenye
mkutano wa kujengewa uwezo kwa njia ya kielektroniki.
Alisema bidhaa ya mwasiliano sio haki ya Afisa Mawasiliano na Habari
pekee kwenye jumuiya, bali anatakiwa kuwa karibu na wakurugenzi, waratibu na
watendaji wengine.
Alieleza kuwa, wakati mwingine ndani ya Jumuiya Afisa huyo anaweza kuwa mwisho
katika utoaji wa taarifa na hasa baada ya kuidhinishwa na kuthibitishwa na
kamati iliyoteuliwa.
‘’Suala la mawasiliano hasa ya kutoka nje ya Jumuiya, linapaswa watoa taarifa
wawe makini na sio jukumu la mtendaji mmoja, bali iwe ni timu ya Jumuiya na
kisha muhusika anateuliwa,’’alieleza.
Akieleza umuhimu wa mawasiliano Mtaalamu huyo, alisema ni kuwaonesha wananchi
kazi zinazofanywa na Jumuiya, kujenga mustakbali na mwelekeo wa Jumjuiya pamoja na kuonesha
kazi zenu.
‘’Wakati mwingine mawasiliano lazima yaangalie kundi la watu fulani,
wakati, aina ya lugha, njia za kuwasiliano nao, eneo husika pamoja na kuhakikisha
kupata mrejesho hapo baadae,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, amwakumbusha Maafisa hao mawasiliano na habari
kuwa wanaweza kutumia nji za mawasiliaono kama vile kuandika, kurikodi sauti na
picha, vipeperushi, mabango, ujumbe mfupi na picha pekee.
Aidha aliwaeleza maafisa hao mawasiliano na habari, kuwa wanaweza
kuitumia mitandao ya kijamii, kuwasilisha taarifa na maelezo yao, kwa jamii ili
kupata taarifa kwa haraka.
Aliwanasihi kuwa, katika eneo hilo ni vyema wakawa makini na kujiridhisha
kabla ya kuweka taarifa zao, kwani faida yake kubwa ni kuwafikia wengi kwa muda
mfupi na ikitokeza kuna mkanganyiko wa taarifa huwafikia wengi.
‘’Mawasiliano ya haraka moja ni eneo la mitandao ya kijamii, iwe face book,
twita, Instagram n ahata tovuti na blog, ingawa athari yake kama hakuna taarifa
rasmi au ukikosea huwa shida kurudi kwa wafuatiliaji wako,’’alifafanu.
Akijibu baadhi ya mawasiliano, mtendaji wa LSF Victoria Mshana, alizishauri
taasisi ziweke utaratibu wa maandishi kutoa taarifa ili kuepusha mkanganyiko
kwa wananchi mbali mbali.
Aidha lisema wawe makini namna ya kuchagua majukwaa ya kutoa taarifa na
kufikisha ujumbe mahasusi kwa walengwa wa kundi fulani ndani ya jamii au taifa
kwa ujumla.
Mmoja wa washiriki hao Abass Famau, alisema mawasiliano ndio kiungo muhimu
na cha lazima kwa taasisi kuhakikisha wanakuwa makini wanapowasiliana na
wananchi mbali mbali.
‘’Inawezekana kila mmoja anataka aonekane kwenye vyombo vya habari, hivyo
mwingine akazungumza hivi na mwingine akazungumza tofauti na mwenzake, na
taasisi ikatafsiriwa vyenginevyo,’’alieleza.
Nao Abass Yussuf Makamba, Bahati Issa Jecha na mwenzake Augusta Chasi
wamesema, changamoto inayojitokeza ni kwa baadhi ya wakati kutokuwepo kwa mawasiliano
na Internet na kusababisha uzoroteshaji wa mawasiliano.
Akiwasilisha kazi za vikundi Shaabani Chande, amesema mafunzo hayo ni
muhimu mno kwao, kwani kwa sasa hakuna mtiririko mzuri wa mawasiliano kuanzia
ndani ya shirika hadi nje.
Nae Augustino Chipamba, wameomba mafunzo hayo yawe mara kwa mara na
kuhakikisha yanakuwa ana kwa ana, ili ufanisi zaidi upatikane kupitia mafunzo
hayo.
Kwa upande wake Saleh Juma, alifafanua kuwa mawasiliani ya kielektroniki
yanasaidia kuwaunganisha na wafadhili waliono nje sambamba na mafunzo hayo
kufanyika kwa njia ya ana kwa ana.
Akiwasilisha mada ya adabu na maadili katika mawasiliano, Afisa Kujengea
Uwezo wa Shirika la Legal Service Facility LSF Victoria Mshana, amesema
mawasiliano yenye heshima, nidhamu na adabu ni muhimu kwa pande zote.
Mwisho
Comments
Post a Comment