NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@
BINAADAMU tumeumbwa
na hulika tofauti katika kulipokea jambo na kuishi nalo.
Wapo ambao wanaoweza kukabiliana
na taarifa mbaya na bila kuchukua uamuzi mgumu, na wapo ambao mioyo yao haina uwezo
kulipokea jambo baya na kuishi nao.
Uwezo wa kupokea taarifa mbaya na
nzuri, unaweza kujengwa na kuharibiwa kwa kutumia udhalilishaji wa akili unao
fanywa na maneno yanayo weza kutamkwa kwa mtu fulani.
Leo hii kwenye jamii zetu, tunaona
aina hii ya udhalilishaji wa maneno umeshamiri kwa kiasi kikubwa, ni aina ya
udhalilishaji unaofanywa sana na jamii zetu na kwenye shughuli mbali mbali za
kijamii.
Ni kawaida sana kKwa jamii zetu
kumuona mama mzazi, akimtusi mtoto wake bila kujua kuwa huo ni udhalilishaji wa
maneno, kwa maana unaweza kumuathiri mtoto taratibu kiakili.
Mwanasaikolojia kutoka hospital ya Kidogo
Chekundu Hamida Naufaul Kassim, amesema udhalilishaji wa maneno, umepelekea
waathirika wengi kuchukua hatua ya kujiua.
Au
wengine kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya na wengine hujenga chuki
dhidi ya jamii nzima.
"Aina
hii ya udhalilishaji umefanya watu wengi hasa mabinti kushindwa kufanya
shughuri zao za kiuchumi, kwa kuogopa kufanyiwa vitendo hivi vya udhalilishaji,
kwa kutolewa lugha za matusi na hata kuitwa majina yasiofaa.
Anasema kumeza dawa, kujitupa
husababishwa na vitu mbalimbali ikiwemo kutoweza kukabiliana na matatizo,
ikiwemo maneno makali, mfumo wa ubongo kutofanya kazi uzuri pamoja na kupata
magonjwa yasiotarajiwa.
Akaenda
mbali zaidi kuwa, mtu anayetumia dawa za kulevya, anaweza kupata athari mbali mbali,
ikiwemo kupata magonjwa ya kimwili, kuharibu mfumo wa kupumua na ugonjwa wa
akili pamoja na kutokubalika katika jamii.
Asia Hassan Juma (sio jina lake kamili)
mwenye miaka 23 ambae ni ulemavu wa uwoni, anasema changamoto mbalimbali ambazo
anakutana nazo kutokana na ubaguzi anaokutana nao katika gari za abiria.
‘’Makonda wa dalala wanatabia ya
ubaguzi, kwani wakimuona mtu mwenye ulemavu wa uwoni, hawakubali kupanda gari peke
yake hadi afuatane na mwezake, jambo ambalo linanikera katika maisha yangu,’’anasema.
Anasema udhalilishaji mwingine wa
maneno ni kuitwa vipofu, wapiga deki na mwendo wa bata jambo ambalo linamfanya
ajitenge na wakati mwengine ashindwe kuchangia mada.
Kwa upande wa mtoto Asha Mtumwa wa
Vikokotoni, anasema baadhi ya wazazi wanatabia ya kuwatolea maneno makali
watoto wao, hadi kuwakatisha tamaa, na kusababisha kuchukua hatua mikononi
mwake.
" Nishawahi kugombwa na mama
yangu, kunitolea maneno makali na kunikatisha tamaa, nilipatwa na hasira
nikamua kuchukua uwamizi wa kumeza dawa, nashukuru jirani yangu alikuwepo na
kunichukua kunipeleka hospitali,’’anasema .
Mkuu wa Dawati la Jinsia ya Watoto
Inspector Mohamed Mwadini Kificho, anasema wazazi wanatabia ya kuita watoto wao
majina makali na kuaza kumuathiri, jina hilo pamoja na kufanya ubaguzi katika
malezi ikiwemo kisaikolojia
Anaona jamii haina uwelewa wa
kutosha, na ndio maana wale wanaotolewa maneno machafu au ya kukatishwa tamaa, hayaripotiwi
sana kuliko matokeo ya ukatili na udhalilishaji ikiwemo ubakaji.
Akawataka wazazi na walezi kutumia
lugha nzuri zenye kuleta maendeleo ya mabadiliko ya mtoto wake, ikiwemo
kutekeleza yale anayo ambiwa na kuacha anayokatazwa.
‘’Wanaotolewa lugha za vitisho,
ukatili, udhalilishaji, matusi ni sehemu ya udhalilishaji, waripoti wanapoona
hali hiyo, kwani ni kosa kisheria,’’anafafanua.
Hapa Mkurugezi wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii, Siti Abasi Ali anasema wanatoa elimu mbali mbali katika
kila shehia, kwa lengo la kuondoa udhalilishaji pamoja na baguzi, wasisahau kutaja
lugha chafu kuwa ni udhalilishaji.
"Tunawaita masheha tunawapa
elimu kuhusina na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji pamoja na ubaguzi
ikiwemo kumtolea mtoto maneno machafu, kuwaita majina mabaya watu wenye
ulemavu,’’anabainisha.
Anasema ili kuhakikisha jamii
inaelewa kuwa hata lugha chafu ni udhalilishaji, wamekuwa wakitoa elimu katika
sehemu mbali mbali ikiwemo skuli na madrassa kwa ajili kumlinda mtoto katika
vitendo vya udhalilishaji.
"Tunatoa elimu hadi kwenye vijiwe
vya vijana, baraza za wazee, skulini, kwa lengo la kuwapa nasaha, kutumia kauli
sahihi kwa watoto, ili kuweka mlingano sawa ndani ya jamii,’’anafafanua.
Anasema wanapinga vikali kwa
baadhi ya waalimu kuwazomewa, kuwaita majina yanayoashiria ufahamu wa akili yake
wanafunzi wasiofanya vizuri madarasani, kwani njia hiyo ni udhalilishaji.
Hakuna njia ya kumrekebisha
mwanafunzi kwa njia ya kumzomea ama kumuita majina kama ya kizota, nanga,
mburura bero, kwamba mitihani ijayo anaweza kufanya vizuri.
Suala
la udhalilishaji linahusu pia kada ya sheria, ambayo kupitia kwao haki
hutarajiwa kupatikana, kama inavyofanya juhudi Jumuiya ya Wanasheria Wanawake ya Zanzibar (ZAFELA).
Yenyewe
iko mbele katika kushiriki kupambana na uovu huu, hivyo Mwanasheria wake, Time
Hassan anasema serikali zote mbili zimeweka mazingira mazuri ya kumlinda mtoto.
Kwa Zanzibar,
ipo sheria maarufu nambari 6 ya mwaka 2011, iliyoanzisha mahakama maalumu ya
kushughulikia makosa ya watoto, na moja ya kosa ambalo linapingwa ni kumdhalilisha
mtoto kimaneno.
Hata
sheria ya Kanuni ya Adhabu nambari 7 ya mwaka 2018, inayoeleza adhabu kwa
makosa yanayohusiana na maadili, kama vile ubakaji, kulawiti, kuingilia kinyume na maumbile na
shambulio la aibu.
Ipo
sheria ya Mahkama ya Kadhi nambari 9 ya mwaka 2017, iliyoundwa ili kusimamia masuala ya ndoa
pamoja na maslahi bora ya watoto, pale inapotokea kutelekezwa na kukosa haki
zao za msingi ikiwemo elimu.
Anafafanua kuwa, jamii ndio tiba ya kwanza, ya
tatizo hili la udhalilishaji wa maneno,
maana mzizi wa tatizo hili huanzia kwenye ngazi familia na kisha kusambaa mpaka
nje kwenye jamii nzima.
Mzazi
Aisha Haji Mkema wa Magomeni, anasema lazima jamii ishirikiane kupinga vita
lugha za udhalilishaji kwenye familia, maana ndio kwenye chanzo kikubwa.
Sheikh
Said Ahmada kutoka Ofisi ya Mufti Pemba, anase,a dini ya kiislamu inakataza
kuitana majina mabaya pamoja na kutumia lugha za udhalilishaji kama vile
mzinifu na mlawitiwa.
‘’Uislamu
unataka jamii itumia lugha za kiutu, kiungwana, amani na salama hata kama kuna
mtu amekutikana na kosa mpaka pale mamla zitakapodhihirisha kosa husika,’’anafafanua.
Mkurugenzi
wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, anasema lugha za kibaguzi, udhalilishaji
na zinazokiuka haki za binaadamu huwaathiri wanawake na watoto.
‘’Wakati
mwingine hata kipindi cha kampeni, wagombea wanawake hufufuliwa makosa yao na
kutangaazwa hadharani, au wakati mwingine baadhi ya wazazi kuwapa majina mabaya
watoto wao waliofanya makosa ya kijamii,’’anasema.
Hakimu
wa Mahkma maalum ya kupambana na udhalilishaji mkoa wa kaskazini Pemba Muumini
Ali Juma, anasema zipo kesi chache mno, zinazoripotiwa zikihusisha lugha za
udhalilishaji ama vitisho.
‘’Inaonekana
jamii haina mwamko mkubwa wa kuripotia kosa la lugha za udhalilishaji, na
wanadhani kama vile sio kosa la jinai, na pengine elimu inahitajika,’’anafafanua.
Mwalimu
mkuu wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent ya Mgogoni Chake Chake Pemb,
Mwache Juma Abdalla, anasema kama waalimu watakuwa na utamaduni kuwapa majina
ya ubaguzi na udhalilishaji wanafunzi wanaopata alama za chini, wanaweza
kuporomosha uwezo wao.
‘’Lazima
sisi waalimu tutumie lugha bembelezi, rafiki, laini, shawishi na yenye
kumuhamasisha mwanafunzi kupenda kusoma na sio zile za kumkatisha tamaa au
udhalilishaji,’’anashauri.
Mjumbe
wa Umoja wa Watu wenye Ulembau UWZ Pemba Hidaya Mjaka Ali na Asia Iddi Mahamoud
mwenye ulemavu wa viuongo, amevishauri vyombo vya kusimamia haki, kutoa elimu
ya athari za kuwaita majina mabaya.
mwisho
Comments
Post a Comment