Na Salma Lusangi Zanzibar
Mkurugenzi Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC) Mwanaisha Ali Said amesema
ZHC imeanza harakati za ujenzi wa nyumba 72 za makaazi katika eneo la Mombasa kwa Mchina Unguja ili kuwaletea wananchi wa
Zanzibar makaazi bora.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na muandishi wa habari hizi, Mkurugenzi huyo amesema harakati za Ujenzi wa nyumba hizo zimeanza Mwezi Machi mwaka huu ambapo shirika hilo limefunga mkataba wa ujenzi na Mkandarasi Simba
Developers Ltd. Hivyo Mkandarasi huyo ameanza kazi rasmi.
Mkurugenzi Mwanaisha amesema ujenzi huo utagharimu shilingi za
Tanzania bilioni tisa nukta nane (9.8) hadi kumalizika kwake kati ya fedha hizo shilingi bilioni tatu
(3) zitatoka katika mfuko wa ZHC na fedha zingine zimetoka katika mfuko wa Serikali kuu kwa maana ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar inayoongozwa na Dkt, Hussein Ali Mwinyi.
Alifahamisha kwamba ZHC
imekubaliana na Mkandarasi huyo katika kipindi cha muda wa miezi 15 kuanzia Machi 2023 nyumba hizo ziweze kamilika ili shirika liweze kuziuza nyumba hizo kwa wananchi mbalimbali ambao watahitaji kununua.
“Lengo letu ni kuziuza nyumba hizo kwa mwenye kuhitaji,
pesa za ujenzi Bilioni tatu tumetoa ZHC na fedha zingine tumepewa na Serikali kuu, nyumba zote zitakua
72 mtu pesa za kwetu”. Alisema Mwanaisha.
Aidha Mkurugenzi Mwanaisha amesema bei ya kuziuza nyumba hizo zitatofautiana kwa sababu kutakuwa na nyumba za vyumba vitatu na zingine vyumba viwili ila kiwango
cha bei itapangwa na Serikali baada ya ujenzi kukamilika.
Naye Meneja Mkuu wa kampuni ya Simba Developers Ltd Nurdin Hussein ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuiamini kampuni yake na kuipadhamana ya kujenga nyumba hizo.
Hivyo ameahidi kwamba kampuni yake itafanyakazi kwa ufanisi na kwa wakati muwafaka kama walivyokubalina na
ZHC.
Kwa Upande wao wananchiwa Zanzibar, akizungumza Bi Asha Ali Kombo (51)
Mkaazi wa Fuoni Uwandani ameishukuru Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Dkt. Hussein
Ali Mwinyi kwa uamuzi wa kujenga nyumba mpya kwani ni wazi kwamba Nyumba za Maendeleo
Zanzibar ni chache na kongwe hivyo hatua hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kwa Shirika la Nyumba
Zanzibar.
Naye Omar Ali Issa (48) Mkaazi wa Raha leo ameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuweka mpango wa kuwauzia watu kwa kulipa fedha kidogo kidogo kwa wenye kipato cha chini.
Alieleza kwamba kutokana na kipato tofauti baadhi ya watu hawataweza kutoa kiwango kikubwa
cha fedha kwa pamoja ila kwa kulipa nusu nusu wataweza.
Mwisho
Comments
Post a Comment