NA MARYAM SALUM, PEMBA@@@@
WANANCHI Kisiwani Pemba wametakiwa kuonesha
ushirikiano kwa Serikali, juu ya jitihada zinazofanywa na viongozi wa nchi katika
kusaidiana kuenzi urithi, ili kizazi
kilichopo na kijacho kiweze kufaidika.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud wakati
akizungumza na wanachama wa jumuia ya Urithi Pemba pamoja na wafanyakazi mbali mbali katika kilele
cha maadhimisho ya siku ya Urithi duniani Afrika,ambapo kitaifa kwa pemba
kilele kimefanyika tenis Chake Chake.
Alisema kuwa
Serikali ya Tanzania Bara na ya Zanzibar kupitia Viongozi wake ilifanya
jitihada za makusudi kwa kuandaa kipindi maalum cha kutangaza utalii duniani kama
urithi wa afrika.
Alisema kuwa
kutokana na jitihada zinazonywa na viongozi hao wananchi ipo haja kwa kuunga mkono jitida hizo ili lego liweze
kufikiwa.
“Viongozi wetu wakuu akiwemo Rais wa Jamuhuri
ya Tanzania Dk. Samia na Dk. Huseein Mwinyi kwa kushirikiana wameandaa mpango
maalum wa kutangaza utalii kama urithi wa Tanzania,”alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Mkuu huyo
alieleza kuwa katika kutekeleza kazi hiyo walifika kwenye maeneo mbali mbali ya
vivutio vya utalii kwa Tanzania bara na Zanzibar, kwa lengo la kuonesha wengine
duniani.
Alisema kuwa
kazi iliyofanywa na viongzoi nchini
katika kutangaza utalii imeweza kuleta matunda makubwa, kwani kumekuwa na
ongezeko la idadi ya watalii kutoka nchi mbali mbali kuja Tanzania na Zanzibar.
“Idadi ya
watalii waliokuja Zanzibar kwa mwaka
2022 ni kubwa na kufikia 27,826 kuliko wakati wote katika historia ya nchi
hii,” alieleza Mkuu huyo wa mkoa.
Alifahamsha
kuwa wakati duania inapoadhimisha siku ya urithi duniani Afrika ni wakati wa kutafakari
kwa kina juu ya maendeleo na changamoto ya ya Urithi katika taifa hili.
Alisema kuwa
kuna haja kwa wananchi wapate nafasi yakuweza kutafakari kuhusiana na kazi na
juhudi ya mipango ya maendeleo inayotekelezwa na viongozi knchini katika kutunza
kuhifadhi na kuimarisha urithi walioachiwa na vizazi vilivyotangulia.
“Niwakati
nzuri kwa Jumuia ya urithi Pemba na Wizara husika kuhakikisha wanaangalia penye
changamoto kutatua, na namna bora pale walipofanya vizuri kuendeleza,” alieleza.
Alieleza
kuwa Wizara ya Utalii inaendelea kuimarishwa na kutunza maeneo mengi kama vile ya Urithi,maeneo ya kihistoria na mambo ya kale, ili kuimarisha utalii
kisiwani Pemba.
Hivyo
wananchi wahakikishe wanalinda tamaduni zao, kulinda urithi ambao wameachiwa
ili kurithisha vizazi vyao.
Kwa upande
wake Afisa Mdhamini Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Zuhura Mgeni
Othman alisema kuwa lengo la kuadhimishwa kwa siku ya urithi duniani afrika ni
kuenzi urithi huo.
“Kila
ifikapo Mei 5 ya kila mwaka duniani kote afrika huadhimisha siku hii kwa
matamasha na tamaduni zote za asili ya Afrika,” alisema mdhamini.
Alisema kuwa
Wizara inaendelea kuimarisha na kuenzi maeneo mbali mbali ya kihistoria kwa
kuyafanyia ukarabati likiwemo eneo la kihistoria la Mkumbuu, Chwaka tumbe na
pango la watoro na Mkamandume.
Aidha
kuipongeza Serikali ya Mapinduzi kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho
maneo mbali mbali ya historia, lengo likiwa ni kuimarisha zaidi kiutalii.
Mapema
akisoma risala ya siku ya Urithi duniani Afrika Mwenyekiti wa Jumuia ya
Uhifadhi Urithi Pemba Haji Seif Yussuf, alifahamisha kuwa imeweza
kufanikiwa kwenye mambo mbali ikiwemo, kusaidiana na Serikali kuhakikisha urithi
wa Pemba unakua hai na endelevu kwa vizazi vya sasa na baadae.
“Kutafuta
wadau wa mambo ya kale na urithi kwa ajili ya kufanya tafiti mbali mbali
Kisiwani humu, pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi wa Urithi na mazingira kwa
jamii kwa miaka miwili sasa,” alieleza Mwenyekiti.
Siku ya
Urithi duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 5 ya mwaka duniani Afrika, ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu kwa upande wa Pemba, Uhifadhi wa urithi ndio mafanikio
ya hazina yetu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment