WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Rahma Kassim Ali amesema kuwepo kwa kituo cha usarifu wa asali nchini kutaimarisha upatikanaji wa bidhaa hiyo na kuondokana kwa tatizo la kukosekana kwa soko la zao hilo hapa Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kusarifu asali huko
Kizimbani Unguja Wilaya ya Magharibi "A"ikiwa ni shamrashamra za
kuelekea miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Alisema ujenzi wa kituo
hicho utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kukuza kipato pamoja na ajira kwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana na wanawake.
Alisema kua ujenzi wa
vituo hivyo ni muhimu kwa upande wa Unguja na Pemba ambapo ni miongoni mwa
jitihada za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kuimarisha rasmi Sekta ya
Uwekezaji kiuchumi ili kuleta tija kwa
wananchi kwa ujumla.
"Vituo hivyo vitasaidia sana kuwawezesha wananchi hasa
wanawake kujikwamua kiuchumi na kuondokana kua tegemezi kwani watakua
wamejiajiri na kuondokana na ugumu wa maisha”Alisema Waziri Rahma.
Aidha alisisitiza umuhimu wa kuyatunza majengo hayo kwa
watendaji katika kuimarisha usafi ili kuweza kufikia lengo lililokusudiwa,
kwani SMZ inamalengo makubwa katika kuwainua wananchi kupitia Sekta ya
Uwekezaji Kiuchumi hivyo haitapendeza baada ya muda mfupi majengo hayo
kuonekana hayaridhishi kimazingira pamoja utendaji kazi.
Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji
Mudrik Ramadhani Suraga aliwataka
wajasiriamali hao kuzalisha asali iliyo bora ili kuweza kuingia katika
ushindani wa kibiashara wa ndani na nje ya nchi kwani SMZ itaendelea kuwawezesha wananchi kiuchumi
kupitia miradi mbali mbali.
“Mkizalisha asali bora itaweza kuingia katika soko la ushindani
wa kibiashara na Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Mhe. Rais wa
Zanzibar na Mwenyeki wa baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi inamipango
mizuri kwa wananchi wake kupitia sekta
hii” Alisema Suraga.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwezeshaji
wananchi kiuchumi Maryam Abdalla Juma
alisema ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka jana mwezi Machi,2022 na umegharimu
jumla zaidi ya shilingi Milioni mia
mbili (236,325,000/= ).
Alifahamisha kwamba katika juhudi ya kuwawezesha wananchi
kiuchumi jumla ya wajasiriamali 753 kutoka Uguja na Pemba wakiwemo wanaume 280
na wanawake 473 walipatiwa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa nadharia na vitendo
ikiwa ni hatua ya kuwajengea uwezo katika utaalam wa kufuga nyuki.
Aidha Katibu Mkuu huyo
alisema kua ununuzi wa vifaa vya ufugaji wa nyuki kwa wajasiriamali
umegharimu jumla ya shilingi milioni mia sita nukta 2.5 (625,000,000/=) ambapo
vifaa hivyo tayari vimeshagaaiwa kwa wajasiriamali wote waliopatiwa mafunzo
Unguja na Pemba kupitia Ofisi za Mikoa.
Naye mjasiriamali wa ufugaji wa asali faraja Ali Hassan
ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Wizara ya Kazi, Uchumi na
Uwekezaji kwa kuwapatia mafunzo hayo
pamoja na kuwajengea kituo cha kusarifu asali hatua itakayowasaidia katika
kujikwamua na hali ngumu ya maisha hivyo aliahidi kuyaafanyia kazi mafunzo
waliyopatiwa kwa vitendo.
Mwisho
Comments
Post a Comment