UKWELI WA DK. MWINYI BAADA YA KUINGIA IKULU, SASA WANAFUNZI 1,236 KONDE WATELEZA KWENTE '''TAIZ' WAKIWA GHOROFANI
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KWA sasa wazanzibar wote, wamo katika shamra shamra za miaka sita ya uongozi war ais kipendwa Dk. Hussein Ali Mwinyi, tokea alipowasili Ikulu ya Zanzibara mwaka 2020. Lengo kuu la yeye kuingia Ikulu, ilikuwa ni kumboa mzalendo wa Zanzibar, ili azidi kuwaletea neemaa, baada ya kupokea kijiti za uongozi kutoka kwa mtangulizi wake Dk. Ali Mohamed Shein. Si unajua ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM, iko demokrasia iliyokomaa, kwa kuhakikisha viongozi wanapishana, ili kuomba ridhaa kwa wananchi, kila baada ya miaka mitano. Mwenye Dk. Mwinyi tokea awamu yake ya kwanza n ahata hii ya pili, ambapo sasa ameshatimiza miaka sita ya uongozi, alipita kwa wananchiu kuwaomba ridhaa. Nakumbuka vyema, alipokuwa ndani ya Jimbo la Konde, aliwaomba wananchi kwanza kumpa ridhaa, ili azidi kunogesha maendeleo ya kielimu, ikiwemo ujenzi wa skuli za kisasa. ‘’Nawaombeni kura, nikifika Ikulu miongoni mwa ahadi zangu moja wapo ni kuwajengea skuli ya ghorofa hapa Konde, ...