MIAKA 62 YA MAPINDUZI YALIYOIJENGA PEMBA KIELIMU, YAMEONDOA GIZA LA ELIMU HADI KUFIKIA MNARA WA MAARIFA
HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ HAKUNA tukio lililobadilisha mwelekeo wa maisha ya Mzanzibari kama Mapinduzi ya 12 Januari 1964. Mapinduzi haya yaliibadili kabisa falsafa ya maendeleo ya jamii kwa kutambua elimu kama haki ya kila mwananchi. Miaka 62 ya Mapinduzi matukufu Zanzibar nzima Unguja na Pemba inasimama kifua mbele kama ushahidi hai wa Mapinduzi yaliyoamua kuwekeza kwenye akili za watu wake. Kwa mujibu wa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), elimu imekuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa tangu siku za mwanzo za Mapinduzi. ELIMU KABLA YA MAPINDUZI, HISTORIA ISIYOFUTIKA Kabla ya Mapinduzi ya 1964, sekta ya elimu Zanzibar ilikuwa dhaifu na yenye ubaguzi mkubwa. Watoto wa wanyonge hawakuwa miongoni mwa wenye kuipata elimu na badala yake waliopata fursa ya kusoma ni wachache tena wenye uwezo na mamlaka pekee. Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 yalileta mwanga mpya katika s...